Uongo wa wazee wa zamani wa Tanzania kuhusu mpira

Taja hiyo zamani ipi? maana katika nukuu zangu umeona nimeandika miongo 70's, 80's na 90's.

Uzuri wa mpira wa miguu ni sanaa ambayo watu wanacheza na kushuhudiwa na watazamaji...
Kwahiyo mzee unataka kusema video za mpira Europe miaka 70s hazipo
 
Hata sisi baadae tukiwa wazee,tutasema hivo hivo mleta mada kaa kwa kutulia.
 
Hawa madogo wahuni tu, usikute linabisha kwa hisia tu hata hao kina Gaga hajawaona.
Hata kwenye top team ya kata tu huko kijijini kwetu kuna wachezaji walikuwa vizuri hakuna wa kulinganisha huko Simba na Yanga
 
Acha makasiriko kijana wa zamani uliyeanza kushabikia na kuangalia mpira 2020. Wachezaji wa miaka iliyopita walisakata boli Sana . Hivi unajua wachezaji Hawa hawakuwa na namba kwenye Timu Yao Yani wachezaji wa Benji
1. Louis Nani
2. Chicharito
3. Barbatov
4. Samir Nasri

Haya nitajie wachezaji wa Sasa unayeweza kumfananisha na
Rooney , au Rayan gigs , Au Didier Drogba , Au Arjen Roberi au inesta, au xavi au Messi na Ronaldo wa kipindi hicho... Kwa tukifanikiwa kuangalia Soka hata la Epl miaka ya 2010 kurudi nyuma to 2005 na Sasa tunaona saivi hakuna wale wachezaji hatari
 
Hasa wazee wa Kariakoo ndio wanaongoza kwa kamba, karibia wote walikuwa wanakaa nyumba ya tatu kutoka yalipo makao ya Yanga na Simba.
 
Kwa kujua stori za jaba za wazee wa zamani huwa zinawashika sana Watanzania Clouds waliona fursa wakamuajiri Mbwiga Mbwiguke.
 
Nguruwe kama wale wa yule bwana wa Dom?
 
Unaakili timamu Messi iniesta roben drogba na Ronaldo ni kizazi Cha zamani naona kama umechanganya mafaili kichwani unajielewa kweli mzee
 
Kwahiyo mzee unataka kusema video za mpira Europe miaka 70s hazipo

Naona unapoteza lengo la mjadala wetu...

Wewe unalinganisha kitu ambacho hujakiona zamani na unachiona sasa...

Umeanza kushuhudia mchezo wa kabumbu miaka ipi?
 
Wewe kweli ni kijana wa hovyo.

Iko siku utasema Jay Jay Okocha na wenzake hawakuwa na kiwango cha kumzidi Osimhen pale Nigeria. Utasema kwamba golikipa Onana ni mkali kuliko Thomas N'kono pale Cameroon.

Kwa ujinga ujinga huu huu utasema Vinicius Jr ana balaa kuliko Romario, Tyson Fury ni mkali sana kuliko Mohammed Ali, Dullah Makabila anamzidi Michael Jackson kwenye Pop kwa mbali sana. 😆🤣
 
... kwenye ELIMU kushuka wapo sahihi!
... nimeshuhudia wasomi wa UDSM wanakariri notes, kwa broken English, kabla ya mitihani nikabaki hoi, ... yaani wanayemuita MKALI naye anaimba notes asizoelewa na 'zero uchambuzi'!
 
Nitashangaa sana kama mzee wako hautamjumuisha kwenye kundi la hao wazee wengine
 
Hahahahaha kuna siku moja nilikua na wachezaji wa zamani wanajisifu kuwa wao walikua bora wkt hawana Kombe lolote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…