Pre GE2025 Uongozi ni karama ya kuzaliwa, Paul Makonda anaendelea kulithibitisha hilo

Pre GE2025 Uongozi ni karama ya kuzaliwa, Paul Makonda anaendelea kulithibitisha hilo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Makonda anajua siasa za nchi hii... ni hatari sana kwa siasa za majukwaani. Wapinzani wana shughuli nzito.
 
Mimi binafsi kwa miaka 7 iliyopita nimeshiriki kumtukana makonda kwa matusi yote nayoyajua ila baadae nimekuja kugundua nilikua brainwashed na propaganda za walamba asali, Makonda is a good guy.

Makonda anastahili nafasi ya uwaziri mkuu atunyooshee watu wapumbavu nchi hii.
 
Huhitajiki kua Rais ili uwe Kiongozi Bora Bali kuielewa tafasiri halisi ya Uongozi inatosha kabisa kuwekwa Moyoni mwa Wananchi.

Mpango, Majaliwa, Mko wapi?? Mbona Uthubutu alonao Makonda, ni mkubwa kuliko hata Nafasi yake?.

Ni sahihi kusema Makonda amezaliwa kua Kiongozi?.

Katibu Mwenezi tu, lakini kazi anayopiga, Uthubutu alonao , kwanini asipendwe ?.

Inawezekana akawa wa Maneno tu, pengine utekelezaji ukawa Mdogo kwakua watekelezaji ndio wanaomkwamisha ..Lakini kitendo Cha Uthubutu wake ,bila kujali nafasi yake, kunatosha kabisa kumpa Sifa ya Ubora wa Uongozi.

Ziara za Makonda, zinaendelea kuonyesha ,nini Wananchi wanataka, watu wanajisikia Amani, wanaona wanajaliwa, wanakua na tumaini .

Laiti kama Kuanzia Wenyeviti wa mitaa , mpaka mawaziri , Watumishi wote wa umma, wangezijua nafasi zao , Ni wazi , Ziara za Makonda zingekutana na malalamiko kidogo.

Mungu akulinde sana Mh Paul Makonda . !!.
Tanzania bado sana kijana wa leo anaangalia kuwa kuna mtu hajafanya kazi yoyote mbali ya kuwa chawa anakaa katika kamati kuu ya chama cha serikali tawala. Huyu kijana utamwambia aende shule akasome atakubali ? Utamwambia ajitume afanye kazi yeyote hata ya kubeba zege atakubali ? Hivi vitu kama serikali hawavifikirii, kizazi kinateketea. Hii nchi watu wote waliokuwepo hapo juu wapo hapo kisa uchawa na sio kitu kingine. Hawajangalia elimu au uwezo wa uongozi. Wanachoangalia ni kama wanaemteua anafaa kuwa kikaragosi cha Rais.
 
Hadi amefikia hapo karata zake anazicheza vizuri
No anafeligi tu watu wanakuwa hawampi full trust. Ila nikimpanga walahi next president ni makonda nipo serious sitaki serious nataka kumuelekeza vitu fulani tu atakuja kunishukuru one day
 
Huhitajiki kua Rais ili uwe Kiongozi Bora Bali kuielewa tafasiri halisi ya Uongozi inatosha kabisa kuwekwa Moyoni mwa Wananchi.

Mpango, Majaliwa, Mko wapi?? Mbona Uthubutu alonao Makonda, ni mkubwa kuliko hata Nafasi yake?.

Ni sahihi kusema Makonda amezaliwa kua Kiongozi?.

Katibu Mwenezi tu, lakini kazi anayopiga, Uthubutu alonao , kwanini asipendwe ?.

Inawezekana akawa wa Maneno tu, pengine utekelezaji ukawa Mdogo kwakua watekelezaji ndio wanaomkwamisha ..Lakini kitendo Cha Uthubutu wake ,bila kujali nafasi yake, kunatosha kabisa kumpa Sifa ya Ubora wa Uongozi.

Ziara za Makonda, zinaendelea kuonyesha ,nini Wananchi wanataka, watu wanajisikia Amani, wanaona wanajaliwa, wanakua na tumaini .

Laiti kama Kuanzia Wenyeviti wa mitaa , mpaka mawaziri , Watumishi wote wa umma, wangezijua nafasi zao , Ni wazi , Ziara za Makonda zingekutana na malalamiko kidogo.

Mungu akulinde sana Mh Paul Makonda . !!.

Unamwambia Mungu amlinde mtu asiyeamini katika Mungu?

Muumba na muaji, wapi na wapi? Au unamaanisha miungu ya mizimu ya kwao?

Hivi kuwa muuaji, nayo inaitwa ni karama? Huyu unayemsifia kwa kweli ana ujasiri wa pekee. Kuna watu hata kumchinja tu kuku wanaona taabu, na kuna wakati wanaingiwa na huruma. Huyu bwana ana ujasiri, lakini ujasiri wa kishetani wa ajabu. Kuwaua binadamu wenzake kama unavyomwua nyoka, kuwateka na kuwatesa binadamu wenzake, na wengine kuwapoteza moja kwa moja, lazima ana roho ngumu sana, roho ya kishetani kupindukia.
 
Huyu mwamba huyu!

Itoshe tu kusema Mungu amsaidie na kumlinda maana hakuna vita ngumu kama kupambana na mkoloni mweusi a.k.a mafisadi.

Kama unafuatilia ziara ya Katibu Mwenezi wa CCM, Mh. Paul Christian Makonda, utagundua mikutano yake imekuwa inafurika watu wengi sana kutokana na kile anachokifanya. Makonda amejitanabaisha kama mtetezi wa Watanzania wa hali ya chini na wanyonge ambao kwa bahati mbaya sana ndo wengi hapa nchini.

Aidha amekuwa akisisitiza watendaji wa serikali na sekta binafsi hasa wanaoshughulika na wananchi moja kwa moja kuhakikisha wanawajibika ipasavyo kwa akili ya kuwatumikia wanachi hawa wanyonge.

Ni mafisadi tu na wenye roho mbaya ambao watakuwa kinyume na Mh. Paul Christian Makonda kwa hii kazi nzuri anayoifanya.

Japo ni ukweli ulio wazi kabisa kwamba hawezi na hatoweza kumfikia kila mhitaji katika nchi hii, lakini kwa hiki anachokifanya kwa kweli anastahili pongezi. Ni mfano mzuri na angalau wananchi watapata sehemu ya kukimbilia tena baada ya Rais wao waliyemchagua kwa kura nyingi kuwaacha katika mazingira ya kutatanisha!

Ee Mungu wa Mbinguni, mlinde PCM na umjalie Hekima mtumishi wako anaposhughulika na kuwatumikia watu wako,

Amin.

Hakuna siku muuaji na mporaji alikuwa na huruma na watu wa chini. Anachokifanya huyu bwana ni ulaghai kwa watu wasio na uelewa.

Huyu ni jitu katili la ajabu. Mioyo ya watu inaendelea kuumia kwa masikitiko na majonzi kupotea kwa Sanane, Azory Gwanda; Lisu kawa mlemavu wa kudumu, kutokana na uharamia wa hili jitu.

Kwa uovu wa mtu huyu, tunamwomba Mungu wa kweli, Mungu wa Ibrahim, Mungu wa Isaka, na mtakatifu wake Masiha Kristo, amwoneshe huyu bwana kuwa kuna Mungu asiyehadaiwa.
 
You are not supposed to be so blind Kwa sababu ya unafiki that you can't face the reality!!.

Ukweli ni Kwamba, Makonda ni Nyota ya Asubuhi.

Uthubutu alonao, licha ya nafasi hiyo , ni wazi kwamba katika Nafasi kubwa, TAIFA LITAJAA HAKI .

Makonda mwenyewe siyo mtu wa haki, amejaa dhuluma na uporaji, atawezaje kusimamia haki? Hivi unamjua Makonda au unamsikia kwa mbali? Hapo Mwanza tu alimpora kiwanja jamaa Capripoint, kisa tu yupo karibu na Magufuli. Ukitaka akufanyie appointment kwa Magufuli alikuwa anataka apewe kati ya 100 na 400m shillings. Baba yake mzazi akiishiwa pesa alikuwa anampigia simu na kumwambia nenda kwa mfanyabiashara fulani. Halafu anampigia yule mfanyabiashara na kumwambia, akija baba yangu hapo mpe milioni 40, halafu wewe nitakutengenezea mambo yako vizuri kwa Rais.

Hapo alikuwa RC tu, je akiwa na cheo kikubwa zaidi atafanya nini?

In short Makonda na mtu mwovu kupindukia, na ni tapeli mzoefu. Mtu hawezi kuwa tapeli kama hana uwezo wa kuwahadaa watu wamwamini. Na ndicho anachokifanya Makonda sasa hivi.
 
..kama tumefikia kuamini Makonda anafaa kuwa kiongozi hapa nchini basi tuna tatizo kubwa sana.

Hii nchi nina hakika ina vichaa na punguani wengine. Hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kutamka eti hili jambazi linafaa kuwa kiongozi. Labda tuamini tu kuwa hawa watu ni sehemu ya ujambazi wa huyu bwana. Wametumwa kuja kumpamba humu ili kuwalaghai wasio na akili.
 
Kwako unaona bora Samia kuwa Rais kuliko Makonda?Nakupa pole kwa chuki zako,zisizo na sababu.

Hivi nchi imekosa watu wote mpaka ikaongozwe na jambazi. Jitu liuaji, litekaji, lilikuwa linapoteza watu? Jitu lililokuwa linapora mali za watu kwa vile tu ni RC na yupo karibu na Rais?

Ni aheri mara 1,000 kuongozwa na Samia au hata Tulia kuliko Makonda au muuaji mwingine yeyote. Makonda ni jambazi linalosubiria siku ya kupelekwa gerezani.

Damu alizozipoteza zitaendelea kulilia haki, mpaka huyu bwana atakapohukumiwa sawasawa na uovu wake.
 
..kama tumefikia kuamini Makonda anafaa kuwa kiongozi hapa nchini basi tuna tatizo kubwa sana.
Hawa ni chawa wanaolipwa. Huko anakopita anatisha Watendaji walete watu katika mikutano
Kwa mfano, hivi Mganga mkuu wa Mkoa anakuwaje katika mkutano wa CCM!

Pili, hivi si alikuwa Mkuu wa Mkoa wa DSM. Kipi alichofanya kikafanikiwa!
-Wanaume walazimishwe kupima tezi dume! utterly stupid
  • Wanawake wataje waliowapa mimba ! Hatujui iliishia wapi
  • Idadi ya wauza Unga- hakuna hata mmoja aliyepigwa faini ya Tsh 20/=
Orodha inaendelea

Kubwa zaidi, atuambie walipo watu wetu na wale wa Viroba ni akina nani
 
Back
Top Bottom