Uongozi serikali ya mtaa babati mjini kwa hili vumbi mnalotulisha wapiga kura wenu ni haki?? Mkurugenzi na timu yako mjitathmini

Uongozi serikali ya mtaa babati mjini kwa hili vumbi mnalotulisha wapiga kura wenu ni haki?? Mkurugenzi na timu yako mjitathmini

Doyi

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2011
Posts
1,578
Reaction score
1,894
Tunafahamu kuna ujenzi wa daraja maeneo ya msasani barabara ya kuelekea stendi mpya inaendelea na ni sehemu ya juhudi za serikali katika kuboresha miundo mbinu,ila kosa la kwanza mlilofanya ni kumpa tenda mkandarasi asiye na weledi kabisaa kabisaa,kwa maarifa yangu madogo alipaswa ajenge njia ya kuchepusha magari yapite pembeni wakati shughuli za ujenzi wa daraja hilo zikiendelea,lakin yeye hakufanya hivyo na badala yake ameelekeza magari yapitebarabara za mtaani kuanzia hangoni,kwere hadi maeneo ya mruki ambapo ni makazi ya watu na bahat mbaya njia hyo ni dhaifu kwa kupitiwa na magari makubwa kwa maana kuna vumbi linaingia kwenye makazi ya watu.ni mwezi sasa watu wanaugua vifua na mafua makali,watoto kwa wazee wanakohoa mpaka damu na hatuna la kufanya.
Kosa la pili ni kutomwagia maji YA KUTOSHA njia hii ya makaz ya watu angalau kupunguza vumbi,Mnamwaga maji ni kama ilimrad bas tu maana mnamwaga mara 1 kwa siku kitu ambacho kinapunguza vumbi kwa chini ya saa 2 tu katika saa 24.Hili si sawa kabisa maana na sisi ni binadamu tunahitaji kuvuta hewa nzuri,najiuliza kama ingetokea mkurugenzi au mbunge au kiongoz yeyote akawa anaishi huku mngefanya haya kweli?? Nadhani njia bora ni engineer wenu atengeneze njia mbadala ya magari kuchepushwa hapo hapo kwenye ujenzi unapoendelea maana huku mtaani mumeshindwa kuwajibika ipasavyo.anyway hamuwez kuwaza nje ya box kwa kuwa nchi zetu za kiafrikahazina sheria kali za kuithibiti serikali za mitaa linapotokea suala kama hili hivyo kutulisha vumbi masaa 24 mnaona ni sawa tu.Nawaomba kwenye vikao vyenu mfikirie upya namna ya kutekeleza hili..kama ni maji mnapaswa kumwaga walau kila baada ya masaa 3 hadi 4. Maji babati yapo ya kutosha na magari ya kumwagilia mnayo sasa shida nini?? Tuweke mawe makubwa barabarani kuzuia magari yasipite ili tuonekane wakorofi??? ...Tanzania aliyeturoga sijui kaburi lake liko wapi,wasomi wamekuwa wajinga hawawafikirii kabisa watu wanyonge.ngoja niishie hapa ila fanyieni kazi hili.asante.
NB:naomba msiniletee gari zenu nyeusi mkaniteka maana hampendi kabisa kukosolewa mnapozingua mie ni mkulima tu wa mbaazi huku kona ya mrara😅😅 nimejaribu kufikisha kilio cha wengi
 
Hizo changamoto za huko babati ni toka miaka ya 90 kumbe mpaka leo bado zipo? Tlaatlaah
 
Kura yako haina thamani, maana wajinga ni wengi wataichagua CCM, hata wakiikataa bado Mkurugenzi ataipitisha, hivyo kama taifa bado sana, labda Mungu aingilie kati
 
Back
Top Bottom