UPDATE: Padri afikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kulawiti watoto 10 Moshi

Kuna kitu nitakielezea siku moja kuhusu haya mambo miaka hiyo nikiwa nafanya kazi za ufundi fulani kwenye taasisi hizi za kidini hasa roman kwa watawa.

Sitaki kuchafua hali y hewa ngoja siku zipite za hizi kashfa za ulawiti na ubakaji inasikitisha sana kwa kweli, ila upweke kwa wanaadamu kamili haujawahi kuwa na uvumilivu wa moja kwa moja, ni lazima ale au aliwe.

Sorry Dotnata member wa humu sikukusudia wewe ila nilikusudia yule aliyekuwa muigizaji simuoni na sijui yuko na mishe gani siku hizi.

CC: Dotnata
 
Natamani wanachokifanya polisi kwa panyaroad wangekifanya kwa hawa wabakaji pia.

Li mtu linaumiza watoto na bila aibu linaenda kuendesha misa. Wakatoliki mnafeli wapi ruhusuni mapadri waoe
Hili lishughulikiwe/liangaliwe kama kosa la mtu binafsi na siyo kikundi. Kila binadamu ana madhaifu yake bila kujali yuko katika kundi gani.
 
Eleza tu, hkn siku hyo tabia itakoma.
 
Hivi imani na tamaduni zetu za mababu zetu haya mambo yalikuwepo kweli..

Dini hizi zilikuja kuharibu jamii zetu..

Kuhusu huyo padri naona maelezo hayajotoshelezi rpc anakanusha hafahamu na mara rc anajua.

Anyway vitendo hivyi vya kipuuzi.

#MaendeleoHayanaChama
 
“Siwezi kusema kama tumemkamata au hatujamkamata, ila suala hili tunaendelea kulichunguza ili kujua ukweli wake, kwa sababu tuhuma hizi zinaelekezwa kwa kiongozi wa dini, hatuwezi kukurupuka kutoa taarifa,” alisema Maigwa.
Kiongozi wa dini!!!!? Au mhuni aliyejificha kwenye dini?
Dini gani hiyo inaruhusu kulawiti watu?
 
Kamanda katoa boko,
eti hizi tuhuma zinamuhusisha kiongozi wa dini hivyo hatuwezi kukurupuka kumkamata!!

kumbe kwa watuhumiwa wengine wasio wa kidini huwa mnakurupuka na kukamata!!
 
It is sad that the clergy has done this shit. Ninapenda kuwa mdadisi zaidi...alisomea wapi na wapi mpaka akawa padri?
Ana miaka mingapi ya upadri? Kanisa linavunja moyo waumini
 
Kwa nini waalimu wa Kanisani na madrasa ,wasiwe wanawake,hakuna zuio la kidini katika dini,mwalimu kuwa mwanamke.
 
Padri Sostenes Soka wa Jimbo la Moshi amefikishwa Mahakamani.Sheria ichukue mkondo wake.Hamna longolongo wala visingizio.
 
Yaani Mkuu wa Mkoa kashindwa kumtaja jina huyo Padri!

Kamanda wa Polisi yeye ndio kaamua kabisa kukana kama kuna hilo tukio!

Askofu wa Katoliki kapotea kabisa na hataki kujibu chochote!

Gazeti limegoma kabisa kutaja jina au kuweka picha ya huyo padri, hata parokia inayohusika haijatajwa!

Mpaka sasa sijaona member yoyote hapa JF aliyeweza kufungua codes ili kutaja jina, picha au parokia ya huyo padri anayetuhumiwa!

Nini mantiki?
Kuna watu au taasisi zinaogopwa, haziguswi na jamii haiko serious kupambana na ubakaji. Baada ya muda hii issue itapotezewa na hakuna kesi yoyote itafunguliwa.
 
Malezi mabovu ndani ya seminary yanachangia. Zamani kuwa padri haikuwa rahisi rahisi. Siku hizi everything is relaxed....na boss kasema who am I to judge?

Mnatukwaza sana waumini. Mapadri mbadilike. Kinachoendelea kinasikitisha upande wa maadili
 
Roma wabatilishe kanuni, hawa jamaa waruhusiwe kuoa !! Mungu mwenyewe aliumba Eva alikuwa na maana yake, upinge wewe nani?
Hata wakioa...kama hakuna maadili mema yatakuwa yaleyale
 
Ni habari ya kusikitisha,hivi katika mafunzo ya dini,haiwezekani kuwekwa mwalimu wa kike?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…