karv
JF-Expert Member
- Dec 26, 2019
- 1,802
- 3,253
Huyo apoHivi kwanini hawakumnyang"anya lile koti alilojifunika nalo, daah ametia aibu kwa taasisi na familia yake
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huyo apoHivi kwanini hawakumnyang"anya lile koti alilojifunika nalo, daah ametia aibu kwa taasisi na familia yake
Kama mtu wa maana vile.
Kuna mambo ya hovyo sana yamejificha kwenye hili dhehebu la wakatoliki! Nawajua,nawafahamu na nimeishi nao tena kwenye abasia zao! Uzinzi,ushoga,ufiraji,kutembea na wake za watu, rushwa,udini,upendeleo na wizi kwao ni kitu cha kawaida! Serikali iangalie sana hawa jamaa la sivyo!.........
Hata wakioa ...ndio unatembea na watoto wadogo? Hivi mapadri shida zao ni kuoa tu?Roma wabatilishe kanuni, hawa jamaa waruhusiwe kuoa !! Mungu mwenyewe aliumba Eva alikuwa na maana yake, upinge wewe nani?
Nan kakuambia seminari ndo wanapika vijana KUwa padri??? Wapo vijana wengi tu ni mapadri lakin hawajawah pita seminari kbsa.Mbona anaonekana mpole...
Huyu angeomba huduma Kwa sister hasingenyimwa....
Mtu mpaka kulawiti watoto wa kiume ina maana ni Shoga...
Na kanisani wanajificha mashoga wengi sana.
Nb..Mimi ni mkatoliki pure tena nimesoma seminary...Jimbo la Moshi mnazembea katika malezi ya waseminari na mapadre...
Mnajivunia mapadre wengi ( tunawapongeza Kwa hilo) lakin hamuwapiki vzr waseminari wenu mpaka wawe mapadre... jifunzeni Jimbo la Bukoba ( wanasheria ngumu na wanafatilia kweli kweli ili mtu aruhusiwe kuwa padre) Wana seminary moja ya Rubya lakin ni very displined seminary yenye mapadre wachunguzi wengi..
Moshi kuna seminary nyingi na nyingi za mashirika so kucontrol wanaoingia seminary na kuwa mapadre inakuwa ngumu...
Usichokijua yule padri ni kweli alimtia mimba yule binti ili kuua soo ikabidi ipangwe hivyo, lakini yule binti hadi kesho analelewa na padri,Sijatetea ila nakushauri ipe nafasi akili y'ako kufanya Kaz wakati unasoma taarifa hiyo...Kuna mapungufu mengi..mengi Sana..
Hi issue inafanana na ya yule padre wa himo Moshi pia bae alituhumiwa kumpa mimba mwanafunzi aliuekuwa akimsomesha(familia maskini).kesi ilivuta hisia za wengi...uchunguzi wa kina ukafanyika..mwisho was siku ikaonekana kumbe Mama mzazi alimpanga binti Ili amtaje padri na hivyo walipwe pesa nyingi...mimba ilikuwa ya kajamaaa kengine...na walihangaika Sana wale wazaz kuomba msamaha na kesi ifutwe.. na mpaka leo ile kesi haipo Tena..so hata kwa hi ukweli utajulikana maana rayari gapes zipo kibao kwenye taarifa...
Jamaa sijui alikwama wapi? Kama alifikia maamuzi ya kubaka watoto si bora angetongoza KONDOO kama MKONO WA BAUNSA alivyofanya?
Vijana wa Pengo🤣🤣UPDATES:
Sostenes Bahati Soka, Padri wa Kanisa Katoliki, Parokia Teule ya Mtakatifu Deonis Aropagita, Jimbo la Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro amesomewa mashtaka matatu katika Mahakama mbili tofauti. Padri huyo mwenye miaka 41, amesomeshwa mashataka hayo leo Jumatatu, Septemba 26, 2022 kwa nyakati tofauti akianza na Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi kisha Mahakama ya Wilaya ya Moshi.
Kesi ya kwanza ilisomwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Salome Mshasha ambapo Padri huyo anakabiliwa na shtaka moja la kumbaka mtoto wa miaka 12. Wakili wa Serikali, Kasimu Nasiri amesema upelelezi wa kesi hiyo umekamilika
Mshtakiwa huyo amekana shtaka hilo huku Wakili wa Serikali, Kasimu Nasiri akisema upelelezi umekamilika na Hakimu Salome ameiahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 10, 2022 ambapo atafikishwa kusomewa maelezo ya awali. Mshtakiwa huyo alitakiwa kuwa na wadhamini wawili wakazi wa Kilimanjaro ambao wawe na uwezo wakuweka bondi ya Sh10 milioni, kika mmoja.
Padri Soka amekosa dhamana kutokana na wadhamini kutokidhi vigezo. Katika kesi nyingine, mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Wilaya, Erasto Phily mshtakiwa huyo amesomewa shtaka moja la ubakaji wa mtoto. Kesi hiyo namba 349 ya mwaka 2022, mwendesha mastaka wa Serikali, Verediana Mlenza na Nitike Immanuel wamesema upelelezi umekamilika. Hata hivyo, mshtakiwa huyo amepata dhamana na kesi hiyo itakuja tena Oktoba 12, 2022 kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali.
Aidha, katika kesi ya tatu, padri huyo ameshtakiwa kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka 12, eneo la kanisa alilokuwa anahudumu. Kesi hiyo ya Jinai namba 44 ya 2022, imetajwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Jenipha Edward ambapo padri huyo nadaiwa kutenda kosa hilo Agosti 2022. Waendesha mashtaka wa Serikali, Kambarage Samson na Veridiana Mlenza wameieleza Mahakama hiyo upelelezi umekamilika.
Mshtakiwa ameachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili wa kuweka bondi ya Sh2 milioni. Kesi hiyo imehairishwa hadi Oktoba 18, 2022 ambapo kesi itakuja kwaajili ya kusomewa maelezo ya awali
==============================
Vitendo vya udhalilishaji wa kingono kwa watoto vinazidi kuitikisa nchi na sasa padri mmoja wa Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuwabaka na kuwalawiti watoto zaidi ya 10.
Watoto hao ni wanafunzi wa kuanzia darasa la sita hadi kidato cha kwanza waliokuwa wakihudhuria mafundisho ya komunio ya kwanza na kipaimara.
Inadaiwa kila alipomaliza haja zake, padri huyo humpa kila mmoja kati ya Sh3, 000 na Sh5,000.
Wakati Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa, akikataa kuthibitisha au kukanusha kukamatwa kwa padri huyo, Mkuu wa Mkoa huo, Nurdin Babu amethibitisha uwepo wa tukio hilo alilosema “ni baya linalofedhehesha”.
Tukio hilo ambalo ni la kwanza kusikika likifanywa na kiongozi wa dini mkoani Kilimanjaro, huku likihusisha idadi kubwa ya wanafunzi, limeibua taharuki kwa wazazi na walikuwa wamejipanga kuandamana kwenda kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Wananchi hao walikuwa wamepanga kuandamana kwenda kwa Waziri Mkuu aliyekuwa mgeni rasmi katika Siku ya Amani Duniani ambayo kitaifa ilifanyika mjini Moshi, ili kupaza sauti zao kutokana na kigugumizi cha kukamatwa kwa padri huyo.
Baada ya polisi kupata fununu za wazazi kujipanga kuandamana na mabango kwenda kwa Waziri Mkuu, ndipo jioni ya Septemba 20, siku moja kabla ya kiongozi huyo kuwasili mkoani Kilimanjaro, walikwenda kumkamata.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa alipotafutwa juzi ofisini kwake kuzungumzia uwepo wa tukio hilo, alikataa kuthibitisha au kukanusha kukamatwa kwa padri huyo zaidi ya kusema wanaendelea kuchunguza tukio hilo.
“Siwezi kusema kama tumemkamata au hatujamkamata, ila suala hili tunaendelea kulichunguza ili kujua ukweli wake, kwa sababu tuhuma hizi zinaelekezwa kwa kiongozi wa dini, hatuwezi kukurupuka kutoa taarifa,” alisema Maigwa.
Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali, zinadai kuwa baada ya wazazi, kubaini watoto wao kufanyiwa vitendo hivyo, walitoa taarifa hizo kwenye vyombo husika ikiwemo uongozi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi na Polisi.
Jina la padri huyo na kituo chake cha kazi tunavihifadhi kwa sasa kwa sababu za kimaadili, hasa kwa kuwa hatujapata upande wake wala vyombo vinavyomshikilia.
Jana, gazeti hili lilimtafuta kwa simu Askofu wa Jimbo Katoliki la Moshi, Ludovick Minde na baada ya kuulizwa taarifa za padri huyo, alisema wapo katika kipindi cha sala, hivyo asingeweza kuzungumza chochote kwa wakati huo (ilikuwa saa 7:12 mchana).
Ilipofika saa 10 jioni Mwananchi, lilimpigia tena simu Askofu Minde ambapo ilikuwa ikiita bila kupokelewa.
Hata hivyo, akizungumza na Mwananchi kuhusu tukio hilo, Mkuu wa mkoa Babu alisema tukio hilo lipo na kwamba ameviagiza vyombo vya usalama kwamba mtu yeyote atakayekamatwa kwa matukio hayo na ushahidi upo, hakuna kurudi nyuma wanapaswa kuchukuliwa hatua kali.
“Katika tabia mbaya zisizo za watu waliostaarabika ni hizo, inaonekana mkoa wetu umezidi kuwa na matukio kama haya. Naviagiza vyombo vya usalama kwamba mtu yeyote atakayekamatwa na ushahidi upo hakuna kurudi nyuma,” alisema RC Babu.
“Kwa sababu haiwezekani kiongozi wa dini kama huyo afanye mambo kama hayo yanayofedhehesha hata waumini wake. Mambo kama haya kwa nchi yetu ni ya kuchafua taswira ya mkoa na nchi na nitaomba mahakama impe adhabu kali,” alisema.
Hali ilivyo kanisani
Mwananchi lilifika katika kanisa analohudumu padri huyo na kukuta ofisi zimefungwa, lakini wahudumu waliokuwepo walidai padri huyo aliongoza ibada Jumapili Septemba 18 na baada ya hapo alienda kwenye mafungo.
“Baada ya misa ya Jumapili aliondoka kwenda mafungo na bado hajarudi, lakini Jumapili ijayo (leo) anaweza kuwepo, kama mnamuhitaji mnaweza kuja kumuona,” alisema mmoja wa wahudumu kanisani hapo ambaye hata hivyo hakutaka kutaja jina lake.
Vilevile, Mwananchi lilizungumza na wananchi wa kada mbalimbali wakiwamo madereva bodaboda wa eneo hilo, ambapo walionyesha kulifahamu suala hilo na kueleza kusikitishwa na kitendo kinachodaiwa kufanywa na kiongozi huyo.
Kauli ya wazazi "Tukio limetuumiza"
Mmoja wa wazazi wa watoto wanaodaiwa kufanyiwa kitendo hicho, alisema kitendo hicho kimemuumiza na kimemfanya apoteze imani kwa kuwa kiongozi wao huyo walimuamini na watoto walimchukulia kama baba yao.
Akisimulia namna alivyofahamu tukio hilo, alidai alipigiwa simu na mtu mmoja akimtaka amchunguze mwanaye kwa kuwa wapo watoto wanaodaiwa kubakwa na padri huyo na mwanaye ni miongoni mwa waliotajwa na wenzake.
“Mwanangu anasoma mafundisho kanisani hapo, nilipopata taarifa hizo, nilimbana akanieleza kuwa amekuwa akiingiliwa na padri huyo tangu Januari mwaka huu,” alisema mzazi huyo ambaye aliomba jina lihifadhiwe.
“Aliniambia wanapokwenda mafundisho, huambiwa waingie ofisini kuungama ambapo huingia mmoja mmoja na ndipo huwafanyia ukatili huo na kuwaambia kuwa wasiwe na shida na wamchukulie kama baba yao,” alieleza mama huyo.
“Taarifa hiyo iliniumiza sana, na ndipo nilipoenda kutoa taarifa kanisani na baadaye polisi, ambapo watoto ikiwemo wa kwangu walipelekwa hospitali ya Mawenzi na kubainika ameingiliwa, jambo ambalo mpaka sasa linaniumiza.”
“Kibaya zaidi baada ya kumbana na kunieleza ukweli, aliniambia baada ya kufanyiwa ukatili huo, hupewa Sh3,000 hadi Sh5,000 ambazo huenda nazo shule na sikuwahi kujua haya, mpaka nilipombana baada ya kuambiwa nimchunguze”.
Mzazi mwingine alisema hawezi kuzungumza kwa undani kuhusiana na tukio hilo kwa kuwa limemuumiza moyoni na limemuathiri mwanaye, kutokana na jamii inayomzunguka kufahamu unyama huo.
“Tukio hili limeniumiza sana, maana mwanangu bado ni mdogo amefanyiwa unyama na ukatili huo na aliyefanya ni kiongozi wa dini tuliyemuamini na hata watoto walipokwenda kanisani hatukupata shaka.”
Baadhi ya wananchi katika eneo hilo, walieleza tukio hilo limeibua taharuki kubwa na kuchafua hali ya hewa, kutokana na kudaiwa kufanywa na kiongozi wa kiroho ambaye wanasema ukimtazama ni mtu mnyenyekevu na asiyedhaniwa kufanya unyama huo.
“Watoto waliofanyiwa ukatili huu wameathirika sana, kwani wapo wanaosoma shule za hapa jirani na wanafahamika na baada ya tukio hili hawawezi kwenda shule kwa sababu ya kunyooshewa vidole na wenzao,” alisema.
Mkazi mwingine wa eneo lilipo kanisa hilo, alisema, “jambo hili limetushtua sana wananchi na baadhi ya wazazi tunaambiwa tayari wamewasitisha watoto wao kwenda mafundisho. Tunaiomba Serikali ilifanyie uchunguzi wa kina suala hilo ili kubaini ukweli wake,” alisema.
Akizungumzia tukio hilo mwenyekiti mmoja wa kitongoji jirani na wananchi hao, alikiri kupata taarifa za watoto hao kufanyiwa ukatili huo na kwamba vyombo vya dola likiamo Jeshi la Polisi vinaendelea kulichunguza, hivyo viachwe vifanye kazi.
“Nikiwa mtaani hapa, nilipata taarifa za watoto 10 kufanyiwa ukatili na kiongozi huyo wa dini, naambiwa wazazi tayari walitoa taarifa kwa uongozi wa kanisa na polisi na tayari vyombo husika vimeanza kulichunguza,” alisema.
Matukio ya udhalilishaji wa kingono kwa watoto yanazidi kushika kasi na uchunguzi unaonyesha ndugu, walimu na viongozi wa dini hushiriki.
MWANANCHI
Kuoa siyo jawabu. Shehe mwenye wake wawili huko Morogoro alipatikana na kosa hilo hilo: kulawiti watatu kwenye shule ya madrasa.Kwa nini hawa watu hawaoi sasa , sasa genye wanazitoaje , mwisho Wa Siku ndio wanaanza Fanya huu upuuzi
Ninajua. Huyu shetani amelindwa sana na wakubwa ndani ya kanisa. Sasa amekuwa na mapembe ambayo hayajifichi tena. Hata waumini tunayaona. Uharibifu umeingia ndani ya nyumba. Very sadHili ni moja tu kati ya mengi ambayo hayatangazwi.
Hao viongozi ni wachafu kupitilza!
Bila shaka wew sio mkatoliki....Mam
Nan kakuambia seminari ndo wanapika vijana KUwa padri??? Wapo vijana wengi tu ni mapadri lakin hawajawah pita seminari kbsa.
Upadri ni wito,so kijana akilelewa vizuri anaweza akwa padri bila hata kupita seminar
🪒Aisee.....
Sema hizi kulea watu kiboizi toka primary zina madhara Kwa ex seminarians na mapadre pia.
Kimsimgi malezi ya single sex ni against nature.
Kikosekana Kwa jinsia ya pili inaaffect walelewa kihisia.
Male chauvinism inafanya KAZI sasa...Hadi Kwa watoto[emoji35]
“Aliniambia wanapokwenda mafundisho, huambiwa waingie ofisini kuungama ambapo huingia mmoja mmoja na ndipo huwafanyia ukatili huo na kuwaambia kuwa wasiwe na shida na wamchukulie kama baba yao,”[emoji134]UPDATES: