Update: Siku ya 8 toka nimeacha pombe maendeleo ni mazuri sana

 

Attachments

  • Screenshot_20261026_225110_Bible.jpg
    48.8 KB · Views: 5
Wazo zuri sana,sasa usije ukakosea tu siku moja ukasema ngoja ninywe leo tu,my friend hakuna bia tamu kama ulikaa muda mrefu bila kunywa,hapo utajikuta umerudi tena mazima,umeamua kuacha acha jumla jumla wala usiinuse,pombe ni ibilisi mbaya sana...
 
Dhamira yako ni ya kweli na ni njema, lakini umefanya kosa moja kubwa sana la kifundi.

Kitendo cha kununua pombe na kuziweka ndani ili kuziangalia kama mapambo ili kujifariji kwamba haziwezi kukushawishi tena, ni kosa kubwa, ziondoe machoni pako.

Ni sawa na kufuatilia mienendo ya mke uliyempa talaka, ili uone kama amejirekebisha umrudie, utakuwa unaitesa nafsi yako kisaikolojia!

Achana na tabia ya kuangalia ama kuwaza pombe.

Pia vijiwe vya pombe ulivyozoea vikwepe na namba za simu za members wako walevi wanaokushawishi ziblock.

Tafuta kazi za kufanya ili kuziba pengo la kukaa kuboeka na upweke bila washikaji zako hao.

Tia dhamira ya kweli toka moyoni mwako na uwe na msimamo kwamba, 'mimi pombe sasa basi'.

Kila jambo ukitaka kulifanikisha, fuata vigezo vyake na utafanikiwa.

Wengi tuliyapitia maisha hayo na tukaachana nayo.

Angalizo:
Usije ukathubutu tena, hata uwe umealikwa kwenye sherehe, kuigiza kunywa hata funda moja, utairudia kwa kasi ya 5g na hautakuja kuweza kuiacha tena.

Jibu lako kwa watu kuhusu pombe liwe ni fupi tu 'pombe situmiagi' na usipende kutoa historia ya maisha yako ya unywaji.

Hapo utakuwa umefanikiwa kuufunga ukurasa.
 
kamata mbadala wa pombe chaaaaaaap kuziba gap kamata chaap kwa haraka.

ushauri wangu ;
Omba Mungu akusaidie kuikata kiu ya pombe jumla Mungu atakusaidia kudill na mzizi wa tatizo hoivyo mshirikishe. unaona wenzio wanakwambia unapumzika tu, hawakosei ukitumia nguvu zako utapumzika tu kwa muda ila kuikomesha kiu jumla mtafute Mungu. Then tafuta kampani mpya ya marafiki ama watu wa kujichanganya nao ambao wanawaza tofautiiiiiiii na mawazo ya pombe sijui baa. mfano unaweza kuamua kuwa unashinda kanisani sikuizi ibada kila siku. ukiweza jiunge kwaya jiunge gym, jiunge timu ya mpira na mengineyo wewe mwenyewe utaangalia na mazingira yako. sambamba na hilo ni ku block kampani ya zamani. na watamaind hao lakini sikia saivi, focus kwenye kile unataka kuona kinatokea kwamba unataka kuacha pombe mizigo isiyohitajika kwenye hii safari yote katilia mbali usiangalie sura ya mtu. FOCUS. mtaconnect ukisimama dhabiti pasina shaka na ukaishida pombe

tafuta mbadala wa kitu utatumia ama utafanya pindi tu ukisikia kiu. unaweza kufosi hobbie mpya. mfano unaweza kujiambia saivi nasikia kiu so badala ya kunya pombe nitakuwa napika , ama nitakuwa nachora so badala ya kwenda baa ingia ndani kwako anza kuchora ama kupika ama jifunze kuendesha baskeli, ama kuendesha gari, ama kushobna nguo, ama kuimba, ama kuandika hadithi, ama kuandika kitabu ama chochote
 
Hongera sana kwa uamuzi mzuri! Tutakuunga mkono
 
Acha utani jombaa! Siku nane unajipongeza hadi JF!πŸ™†πŸ™†πŸ™†πŸ™†
Kuna watu waliishakaa miaka minne mpaka akafanyiwa "birthday" ya kiacha pombe, lakini leo anagonga urabu maradufu ya pale acha! Nini siku nane! Ebu njoo hapa Empire karibu na Tema Hotel, Nyegezi, Jijini Mwanza tunywe Konyagi.
 
Kazi za shetani zipo akhera?
 
Akili siyo kuacha pombe . Akili ni kuitawala pombe .. wewe ulitakiwa kuvunja hiyo campani tu na kugonga bia moja au mbili tu pole pole ungeweza kuitawala pombe .. sasa unatumia nguvu kubwa kuiacha pombe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…