Elections 2015 Updates: Mchakato na Matokeo ya kura za maoni ya Ubunge CCM nchini kote

Mkuu mbona ukijipa nafasi ya kuelewa utamjua mshindi ndani ya hii post au sijamtaja. Hapa nimeandika kwa kumtaja mshindi sema sina idadi ya kura kwa kila mgombea ndo maana nikasema mwenye idadi kwa wagombea wote atuwekee
 

Mkuu tupe Ukonga,Instagram kila mgombea anasema ameshinda hapo Ukonga,tupe uhalisia!!!
Hata kwa yeyote anaejua Hilo jimbo,Mengine sijasikia Utata!!ok na kule kwa kabaka Gaudensia na Matiko Easther sijui nani kashinda
Yeyote mwenye taarifa
 
Jimbo la Masasi Rashid Mohamed Chuachua, Jimbo la Ndanda Mariamu R. Kasembe. Jimbo la,Lulindi Jarome Bwanausi.
 
Kiujumla hali ni mbaya kila kona ya nchi, slogan ya bao la mkono inafanya kazi kwa kasi ya kipekee sana na hii inaonyesha hao wanaofanya hivyo wamepata mbinu hizo kwa wakubwa zao wa chama kwa lengo ili itumike kwenye uchaguzi mkuu oct 25, badala yake wameamua kutumia kwanza wenyewe kwa wenyewe, haki zetu za kumpata kiongozi anayetufaa zapotea hivihivi.

Ushauri wangu: vyama vya upinzani itafute mbinu mbadala ya kupambana na hili bao la mkono mapema kabla haijaleta matafuruku na kuwanyima watanzania haki ya kupata kiongozi wanaomhitaji.
 
Ukichaa mwingine wa baraza la vichaa chadema (Bavicha). Unawaona hao tu. Lowassa vipi?
 
Kamwe ccm hawawezi kumpitisha Bashe kuwania Ubunge, Kama walikata jina lake Lowassa akiwa bado ccm, Watashindwaje kukata hivi sasa alivyohamia Cdm?

Bashe Safari yake Bungeni inaishia Kamati kuu ccm, Kama anataka Ubunge akogombee Somalia,!

BACK TANGANYIKA
 

Yanayojitokeza CHADEMA na UKAWA tumepoteza turufu. Kampeni zetu zingevutia sana.
 
CCM ni chama tawala, na kwa nafasi kubwa sana watawala wa serikali na Dola kwa ujumla wako chini ya viongozi wakuu wa Serikali kupitia chama chao. Hofu yangu, kama mbinu chafu za kuandaa shahada za kupigia kura ziliweza kuandaliwa na zikiwa tayari zimefanyiwa uchaguzi wa baadhi ya wagombea kule Tarime, je Uchaguzi mkuu oktoba 25 si zaidi ya hayo?
 
Tibaijuka swahiba wa lowassa kapita!Chadema haiwezi kuongelea ufisadi.
 
hizo idadi ya kura za maoni CCM hazina uhalisia

ni kweli kiongozi kama jimbo la bumbuli naona makamba jr ameshinda na wapiga kura walikuwa zaidi ya elfu kumi na tatu ....kama wapiga kura wa jimbo awazidi elfu ishirini na tano hapo makamba ameshashinda .....
 
Huko tarime bwana nyambari kashikwa na karatasi zilizotikiwa kura 2000 cha ajabu nini nyie kura zenu za kubuni siyo halisi
 
Ngeleja lazima akae na arudi kuchuga ng'ombe Wana wa sengerema hatumutaki
Na we hate CCM
 
Ukichaa mwingine wa baraza la vichaa chadema (Bavicha). Unawaona hao tu. Lowassa vipi?
tibaijuka hadi account number ambayo hela iliingia tunaijua ,nitajia akaunti number ya lowassa hela za richmond zilipoingia,ushaambiwa richmond ni kazi ya mikono ya mkuu,subiri kwenye kampeni kila kitu kitawekwa wazi
 
Kamanda siasa za Tanzania ndivyo zilivyo hata huko Chadema huoni fisadi mnavyomshangilia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…