Elections 2015 Updates: Mchakato na Matokeo ya kura za maoni ya Ubunge CCM nchini kote

Elections 2015 Updates: Mchakato na Matokeo ya kura za maoni ya Ubunge CCM nchini kote

Mkuu mbona ukijipa nafasi ya kuelewa utamjua mshindi ndani ya hii post au sijamtaja. Hapa nimeandika kwa kumtaja mshindi sema sina idadi ya kura kwa kila mgombea ndo maana nikasema mwenye idadi kwa wagombea wote atuwekee
 
KURA ZA MAONI CCM
1. Mwigulu - Iramba
2. Nape - Mtama
3. Mwakasaka - Tabora Mjini
4. Mama Sitta - Urambo
5. Kadutu - Ulyankulu
6. Bashe - Nzega
7. Ngeleja - Sengerema
8. Seif - Igunga ktk jimbo jipya.
9. Masaburi - Ubungo
10. Patel - Ukonga
11. Prof Kamala - Nkenge, Misenyi
12. Kagasheki -
13. Lukuvi - Isimani
14. January - Bumbuli
15. Muhongo - Musoma vijijini
16. Ndugai - Kongwa
17. Chumi - Mafinga
18. Kigola - Mufindi kusini
19. Mgimwa - Mufindi kaskazini
20. Filikunjombe - Ludewa
21. Mgimwa - Kalenga...
22. Lusinde - Mtera
23. Imani Moshi - Kaliua
24.Mwakasaka -Tabora mjini
25.Fenala Mkangara -Kibamba
26.Mapunda-Mbinga mjini
27.Masele -Kahama
28.Antony Mavunde-Dodoma hizi ndio data
nilizopata

Mkuu tupe Ukonga,Instagram kila mgombea anasema ameshinda hapo Ukonga,tupe uhalisia!!!
Hata kwa yeyote anaejua Hilo jimbo,Mengine sijasikia Utata!!ok na kule kwa kabaka Gaudensia na Matiko Easther sijui nani kashinda
Yeyote mwenye taarifa
 
Jimbo la Masasi Rashid Mohamed Chuachua, Jimbo la Ndanda Mariamu R. Kasembe. Jimbo la,Lulindi Jarome Bwanausi.
 
Kiujumla hali ni mbaya kila kona ya nchi, slogan ya bao la mkono inafanya kazi kwa kasi ya kipekee sana na hii inaonyesha hao wanaofanya hivyo wamepata mbinu hizo kwa wakubwa zao wa chama kwa lengo ili itumike kwenye uchaguzi mkuu oct 25, badala yake wameamua kutumia kwanza wenyewe kwa wenyewe, haki zetu za kumpata kiongozi anayetufaa zapotea hivihivi.

Ushauri wangu: vyama vya upinzani itafute mbinu mbadala ya kupambana na hili bao la mkono mapema kabla haijaleta matafuruku na kuwanyima watanzania haki ya kupata kiongozi wanaomhitaji.
 
Ukichaa mwingine wa baraza la vichaa chadema (Bavicha). Unawaona hao tu. Lowassa vipi?
 
Kamwe ccm hawawezi kumpitisha Bashe kuwania Ubunge, Kama walikata jina lake Lowassa akiwa bado ccm, Watashindwaje kukata hivi sasa alivyohamia Cdm?

Bashe Safari yake Bungeni inaishia Kamati kuu ccm, Kama anataka Ubunge akogombee Somalia,!

BACK TANGANYIKA
 
Wale watuhumiwa 4 wa escrow Chenge, Muhongo, Ngeleja na Tibaijuka wameshinda kwa kishindo kura za maoni kule CCM. Wanaccm waliopiga kura za maoni wamedharau adhabu walizopewa wagombea hao na uongozi wa juu wa chama. Lakini ukweli unabaki palepale hawa ni WATUHUMIWA tu kama alivyo Nape pale Takukuru Lindi!

Yanayojitokeza CHADEMA na UKAWA tumepoteza turufu. Kampeni zetu zingevutia sana.
 
CCM ni chama tawala, na kwa nafasi kubwa sana watawala wa serikali na Dola kwa ujumla wako chini ya viongozi wakuu wa Serikali kupitia chama chao. Hofu yangu, kama mbinu chafu za kuandaa shahada za kupigia kura ziliweza kuandaliwa na zikiwa tayari zimefanyiwa uchaguzi wa baadhi ya wagombea kule Tarime, je Uchaguzi mkuu oktoba 25 si zaidi ya hayo?
 
Tibaijuka swahiba wa lowassa kapita!Chadema haiwezi kuongelea ufisadi.
 
hizo idadi ya kura za maoni CCM hazina uhalisia

ni kweli kiongozi kama jimbo la bumbuli naona makamba jr ameshinda na wapiga kura walikuwa zaidi ya elfu kumi na tatu ....kama wapiga kura wa jimbo awazidi elfu ishirini na tano hapo makamba ameshashinda .....
 
Hizi akili za pro-ufisadi ni za mgando sana. Kama chadema katiks kura za maoni mshindi anashinda kwa kura 56 na waliobaki chini ya hapo. Wakati ccm mshindi anashinda kwa kura 6000 na wansomfuatia ~5000, ~4000 nk. Hivi nani mwenye wanachama wengi hapo?
Huko tarime bwana nyambari kashikwa na karatasi zilizotikiwa kura 2000 cha ajabu nini nyie kura zenu za kubuni siyo halisi
 
Ngeleja lazima akae na arudi kuchuga ng'ombe Wana wa sengerema hatumutaki
Na we hate CCM
 
Ukichaa mwingine wa baraza la vichaa chadema (Bavicha). Unawaona hao tu. Lowassa vipi?
tibaijuka hadi account number ambayo hela iliingia tunaijua ,nitajia akaunti number ya lowassa hela za richmond zilipoingia,ushaambiwa richmond ni kazi ya mikono ya mkuu,subiri kwenye kampeni kila kitu kitawekwa wazi
 
Natabiri (japo sio Sheikh Yahaya) kuwa huu mchakato wa ubunge na udiwani utaigawa zaidi ccm hata zaidi ya mchakato wa urais.
Hebu fikiria mwenyekiti wa ccm mwenyewe JK alivyo declare pale Diamond Jubilee kuwa Prof. Tibaijuka 'amekosa maadili' na 'wakamuomba awapishe' lakini wanachama wamemrudisha.
Na Chenge Andrew naye karudishwa na wanachama.
Sasa katika ukweli kama huu uongozi wa chama na hasa mwenyekiti wanapaswa kuonyesha kuwa hayo majina matano waliyopitisha Dodoma yalikuwa masafi kuzidi yaliyoachwa (walioshiriki mkutano wengi wameshasema kuwa yalikuwa mfukoni mwa mwenyekiti).
Na ni mwenyekiti huyo huyo aliyemsifia sana EL wakati wa kufunga bunge hata zaidi ya waziri mkuu aliyepo!
Kamanda siasa za Tanzania ndivyo zilivyo hata huko Chadema huoni fisadi mnavyomshangilia.
 
Back
Top Bottom