Upigaji Uyui: Waziri Mkuu ashangazwa kibanda cha Mlinzi VETA kujengwa kwa Tsh. milioni 11, aagiza waliyosimamia ujenzi kukamatwa

Upigaji Uyui: Waziri Mkuu ashangazwa kibanda cha Mlinzi VETA kujengwa kwa Tsh. milioni 11, aagiza waliyosimamia ujenzi kukamatwa

Waziri mkuu Majaliwa ameiagiza Takukuru kuwakamata wote waliosimamia ujenzi wa Chuo cha Veta Uyui

Majaliwa ameshangaa kuona kibanda cha mlinzi kimegharimu tsh 11 milioni

Source ITV habari
Hata na majaliwa ni mpigaji, sema yeye ana ulinzi. hata wewe ni mpigaji
 
Nyie mkipandisha bei za mafuta , Vifurushi na Transaction za benki tunawaelewa Ila nyie mkiongezewa Hela kidogo mwe ye miradi yenu mnaanza kulia lia
 
Screenshot_20220908-204249.png
 
Na hapo fundi aliyefanya kazi unakuta hata laki 4 hazijafika na bado anasubiria mkandarasi alipwe ndio ampe chake
 
Tozo ilivyojenga ofisi ya 11,000,000, unaambiwa ni ofisi ya kisasa zaidi.

-
Waziri Mkuu Majaliwa akiwa ziarani Wilayani Uyui, Tabora amekagua ujenzi wa Chuo kipya cha VETA na ameonesha kutoridhishwa na gharama za ujenzi wa kibanda cha Mlinzi ambacho ujenzi wake ni Tsh. Milioni 11 “TAKUKURU chunguzeni gharama za ujenzi wa kibanda hiki”

View attachment 2350408
PICHA: Kibanda cha Mlinzi kilichojengwa kwa Tsh Milioni 11
----
WALIOSIMAMIA UJENZI WA VETA UYUI WAKAMATWE- MAJALIWA


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) Mkoa wa Tabora, Musa Chaulo kuwakamata watu wote wanaohusika na usimamizi wa ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) wilaya ya Uyui mkoani Tabora kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha za mradi huo.

Amechukua hatua hiyo baada ya kukagua mradi huo na kuonesha kutoridhika na gharama za ujenzi wa baadhi ya majengo ikiwemo kibanda cha mlinzi ambacho ujenzi wake umegharimu shilingi milioni 11.
“Sitamvumilia yeyote atakayemuhujumu Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, watafutwe na wachukuliwe hatua.”

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Septemba 8, 2022) baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa chuo cha VETA wilaya ya Uyui mkoani Tabora ambapo amesema hajaridhishwa na ujenzi wa chuo hicho ambacho majengo yake yanejengwa kwa gharama kubwa tofauti na uhalisia kwa kutumia mfumo wa nguvu kazi ya ndani (force account).

Mbali na ujenzi wa kibanda cha mlinzi, pia Waziri Mkuu ameonesha kutoridhishwa na ujenzi wa nyumba za watumishi chuoni hapo ambapo nyumba moja yenye uwezo wa kuchukua familia mbili inajengwa kwa gharama ya shilingi milioni 114 na tayari wameshatumia zaidi ya shilingi milioni 70 na bado haijakamilika.

“Nyumba moja yenye uwezo wa kuchukua familia tatu Wizara ya Afya inajenga kwa shilingi milioni 90 na Ofisi ya Rais (TAMISEMI) wanajenga nyumba za walimu zenye uwezo wa kuchukua familia mbili kwa gharama ya shilingi milioni 57 na wanajenga kwa mfumo wa force account kama mnavyojenga hapa, hii haikubaliki.”

Kutokana na kutoridhishwa na ujenzi wa chuo hicho unaosimamiwa na VETA, Mheshimiwa Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Burian asimamie ujenzi wa chuo hicho ili uweze kukamilika kwa wakati. “Mkuu wa mkoa simamia vizuri ujenzi wa chuo hiki, tunataka ukamilike kwa wakati.”
Waziri mkuu anahangaika na vijimilion 11 ili hali kuna mabilioni yanatafunwa kila kona
 
😅😂 acha ujinga wewe ktk miradi mingi wakat wa Magu hivyo vibanda vilijengwa kwa zaidi ya million 10, Magu alishindwa kugundua upigaji huo kwasabab ni ngumu unapokagua mradi kufuatilia kibanda badala ya mradi mkuu... Kilichotokea sasa hivi hivyo vibanda vinagundulika watu wedhurumiana pesa kwenye ukandarasi kwahio wanaunguza picha kwa kiongoz anaekuja kukagua mradi aangalie na vibanda bei yake...
 
Watu ambao hawajawahi kujenga ndio watashangaa mimi nikikiangalia hicho kibanda mbona pesa hiyo ni halali!.

  1. Kuchimba msingi vibarua 500,00
  2. Kujenga Msingi mawe zege 1,000,000
  3. Kuinua kuta 1,000,000
  4. Madirisha 3 ya PVC za Uturuki 3,000,000
  5. Milango miwili ya Mninga 1,000,00
  6. Bati ya South 1,000,000
  7. Tails za mable 1,000,000
  8. Scatting ya black granite 500,000
  9. Rangi ile washable 500,000
  10. Msimamizi 1,000,000
  11. 10% ya aliyetoa kazi 1,000,000 hapo kuna wizi gani?.
JIfunze kuangalia quality kabla hatujakimbilia kupigia kelele wizi na ufisadi, ujenzi wa majengo yoyote ya umma unatanguliwa na BOQ.
Kwa msio jua quality ya ujenzi, nendeni makaburi ya Kinondoni kuna kaburi pale limegharimu TZS 36.M!.

Mfano mimi natamani tomb stone yangu iwe kama ile ya ku roll, find out how much it costs, tusishabikie tuu ufisadi!.
P
Nilidhani wewe ni Mzalendo kumbe kweli wewe ni msaka fursa, na hapa nahisi umeamua kuonesha uhalisia wa sura yako baada ya kunusa kuwa lile jambo lako limeshabutuliwa.

Pascal naamini unajua vizuri muongozo wa "Force account" nilidhani maelezo yako yote yangezingatia muongozo huo ila tu kwa maksudi umeamua kupoza hasira zako dhidi ya jambo lako Ndiyo maana umeandika haya uliyo yaandika.

Tukirudi kwenye hoja ni kwamba.
1. BOQ za majengo ya serikali hazina chaguo la matakwa ya mtu binafsi, bali zimeainishwa kwa kuzingatia hali ya mahitaji ya kawaida na siyo anasa zaidi, hivyo ukiweka matamanio yako Ndiyo ubadhilifu wenyewe hata kama ni bora.

2. Mchakato wa ujenzi wa Force account ni wa bei huria kwa maana ya fundi na mzabuni wa vifaa kwa jumla ya ukamilifu wa kazi ya mradi, hivyo Basi hizo bei ulizoziandika ziwe za fundi au vifaa haziwezi kufikia huko kama kulikuwa na ushindani huria na sahihi wa zabuni.

3. Kwa Kila hatua ya mchakato wa mradi maofisa wa vifaa (pmu) hushirikishwa kukagua idadi ya vifaa na bei halisi kuona kuwa viko ndani ya bajeti au laa. Hivyohivyo ofisi ya mkandarasi naye hukagua Kila hatua kuona kuwa pamoja na ubora wa kazi lakini pia asiombe fedha zaidi ya mkataba wake kwa Kila hatua.

4. Veta kupata fursa hii ya kusimamia mradi ilikuwa ni fursa nzuri kwao kudhihirisha ubunifu wao katika kutumia fedha kidogo kupata kitu bora maana ufundi ndiyo taaluma yao. Serikali, Wananchi na wadau wa ujenzi walitarajia kuona wao wanatumia fedha kidogo kupata ubora stahiki na siyo fedha nyingi zaidi kama unavyotaka watu waamini.

5. Hivyo basi; pamoja na kusikika kwa mhusika mmoja katika ujenzi huu, ukweli ni kwamba, uzembe utakuwa umefanyika katika ofisi tatu ambazo ni Ofisi ya uhasibu (pmu), Ofisi ya mhandisi na Ofisi ya Mkuu wa chuo.

6. Pascal ktk hoja hii nakubaliana na waziri mkuu hicho chumba kimoja hakiwezi kugharimu milioni 11. Wewe una lako.
 
Je, ni lazima TAKUKURU waagizwe kufanya uchunguzi, wasipo agizwa maana yake ndio imetoka?

Sijajua hii taasisi inafanya vipi kazi ila ni mambo ya kushangaza sana. Daily utasikia waziri aagiza TAKUKURU ifanye uchunguzi, mara Mkuu wa Mkoa aagiza TAKUKURU. Sasa je, wao kama wao ni lipi wanachokifanya ofisini?
Screenshot_20220908_212924_com.facebook.katana.jpg
 
Back
Top Bottom