Upigaji Uyui: Waziri Mkuu ashangazwa kibanda cha Mlinzi VETA kujengwa kwa Tsh. milioni 11, aagiza waliyosimamia ujenzi kukamatwa

Upigaji Uyui: Waziri Mkuu ashangazwa kibanda cha Mlinzi VETA kujengwa kwa Tsh. milioni 11, aagiza waliyosimamia ujenzi kukamatwa

Nilidhani wewe ni Mzalendo kumbe kweli wewe ni msaka fursa, na hapa nahisi umeamua kuonesha uhalisia wa sura yako baada ya kunusa kuwa like jambo lako limeshabutuliwa.
Duh... Mkuu Mbogi, yaani nyie watu wa kitengo mmetapakaa hadi humu, yaani kumbe unayomatokeo!. Nimepata pressure nimeshindwa kuendelea....
 
Je ni lazima TAKUKURU waagizwe kufanya uchunguzi? Wasipo agizwa maana yake ndio imetoka?

Sijajua hii taasisi inafanya vipi kazi ila no mambo ya kushangaza sana. Daily utasikia waziri aagiza TAKUKURU ifanye uchunguzi mara Mkuu wa mkoa aagiza TAKUKURU sasa je wao kama wao ni lipi wanacho kifanya ofisini? View attachment 2350563
Huu upuuzi ni jambo la kushangaza.
 
Rushwa ya Tanzania ni maagizo ya wakubwa. Hata ukipiga bilioni 10 kama na wakubwa wamepewa mgao hakuna rushwa hapo
 
Kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake,ILISHARUHUSIWA........Kuwakamata nikuwaonea
 
Duh... Mkuu Mbogi, yaani nyie watu wa kitengo mmetapakaa hadi humu, yaani kumbe unayomatokeo!. Nimepata pressure nimeshindwa kuendelea....
P. hilo la "jambo lako" lilikuwa chomekeo tu! Lakini nikuulize kiuhalisia, hivi wewe kweli kwa ukweloli wako wa nafsi milioni 11 ni sawa kwa chumba kimoja cha sqm 9?
 
Inaonekana mtoa Mada hajawahi kujenga au alijenga miaka ya '90 wakati Bati inauzwa 1,250/-

Bei ya Bati 28G saivi ni 43,000 - 47,000
Bei ya Tiles ya 50x50 ni 39,000
Mlango huo unaweza kufika 850,000 pamoja na frame

Ikumbukwe hiyo kazi amefanya Mkandarasi, naye ameajiri na analipa watu Mishahara kwahiyo lazima aweke Faidi ambayo inaweza kuwa 10% ya gharama za Mradi.

Ingekuwa kinajengwa Kwa njia ya Force account walau gharama yake ingeshuka hadi 6.5M hivi kutokana na hadhi ya kibanda chenyewe.

Wazir mkuu kasema force account....

All in all sheria za manunizi bado chenga sana hakuna fair price kabisa apo ukute mtu ka quotation ya mfuko wa 50k buti 70 tiles 100k ndoo ya rangi 250k lazima ifike uko manunuz yanaua sanaaa aisee
 
Hakika tumbua tumbua ambayo ingetokea pale Tabora Uyui isingekuwa ya kitoto

Mungu amlaze Peponi Shujaa Magufuli
Wala sioni shida hapo kwanza wamekula kidogo sana, sio kwamba wamekula zote milion 11 maana wamejenga kitu hata kama kidogo. Huyo unayemtaka aje alipiga 1.5 Trillion ! Huoni tofauti ya kuumiza na kuua hapo ??
 
Hata nao wasingejaribu kufanya hivyo,walikua wanajua moto wake,alikua hakufumbii macho,tofauti na sasa,ambapo unasikia mtu anasema eti NAJUA MNAKULA,anawasihi WASIVIMBIWE na WASIGOMBANIE SAFARI,wapangiane tu,nani aende,nani ataenda.
Eti anataka NIDHAMU ya kutoka MOYONI,ataki waogope kutenda maovu kisa wataadhibiwa.
 
Wala sioni shida hapo kwanza wamekula kidogo sana, sio kwamba wamekula zote milion 11 maana wamejenga kitu hata kama kidogo. Huyo unayemtaka aje alipiga 1.5 Trillion ! Huoni tofauti ya kuumiza na kuua hapo ??
Kwahiyo tu-justify upigaji kisa inasemekana zilipigwa?
Two wrongs...?
 
Back
Top Bottom