Hata na majaliwa ni mpigaji, sema yeye ana ulinzi. hata wewe ni mpigajiWaziri mkuu Majaliwa ameiagiza Takukuru kuwakamata wote waliosimamia ujenzi wa Chuo cha Veta Uyui
Majaliwa ameshangaa kuona kibanda cha mlinzi kimegharimu tsh 11 milioni
Source ITV habari
Katika milioni 11 ngapi zimejenga nyumba ya bosi?Nyingine zimejenga nyumba ya Bosi.
Safi sana,machadema yalituchelewesha Sana kupata maendeleoSafi sana, kimetoka bomba
Mimi naona hawajapiga kivile mkuuAisee! I was sarcastic sijui wewe.
Umesikini umesababisha roho mbaya...hakuna wizi hapoAkili za Watanzania ni finyu pamoja na viongozi wetu.
Watanzania wakisikia kuna mtu kasimamishwa kazi au katumbuliwa mioyoni wanapata raha.
Hapa haijaibwa hata mia
Kwahiyo tuendelee kushindana kuiba ?? !!Sema awamu ya tano kulikuwa Kuna majambazi wakubwa nikikumbuka ile TL 1.5 ilivyoibwa kama mvua
Ila hakifiki 11mHicho kibanda kwa muonekano kinazidi laki 5.
Waziri mkuu anahangaika na vijimilion 11 ili hali kuna mabilioni yanatafunwa kila konaTozo ilivyojenga ofisi ya 11,000,000, unaambiwa ni ofisi ya kisasa zaidi.
-
Waziri Mkuu Majaliwa akiwa ziarani Wilayani Uyui, Tabora amekagua ujenzi wa Chuo kipya cha VETA na ameonesha kutoridhishwa na gharama za ujenzi wa kibanda cha Mlinzi ambacho ujenzi wake ni Tsh. Milioni 11 “TAKUKURU chunguzeni gharama za ujenzi wa kibanda hiki”
----
WALIOSIMAMIA UJENZI WA VETA UYUI WAKAMATWE- MAJALIWA
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) Mkoa wa Tabora, Musa Chaulo kuwakamata watu wote wanaohusika na usimamizi wa ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) wilaya ya Uyui mkoani Tabora kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha za mradi huo.
Amechukua hatua hiyo baada ya kukagua mradi huo na kuonesha kutoridhika na gharama za ujenzi wa baadhi ya majengo ikiwemo kibanda cha mlinzi ambacho ujenzi wake umegharimu shilingi milioni 11.
“Sitamvumilia yeyote atakayemuhujumu Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, watafutwe na wachukuliwe hatua.”
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Septemba 8, 2022) baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa chuo cha VETA wilaya ya Uyui mkoani Tabora ambapo amesema hajaridhishwa na ujenzi wa chuo hicho ambacho majengo yake yanejengwa kwa gharama kubwa tofauti na uhalisia kwa kutumia mfumo wa nguvu kazi ya ndani (force account).
Mbali na ujenzi wa kibanda cha mlinzi, pia Waziri Mkuu ameonesha kutoridhishwa na ujenzi wa nyumba za watumishi chuoni hapo ambapo nyumba moja yenye uwezo wa kuchukua familia mbili inajengwa kwa gharama ya shilingi milioni 114 na tayari wameshatumia zaidi ya shilingi milioni 70 na bado haijakamilika.
“Nyumba moja yenye uwezo wa kuchukua familia tatu Wizara ya Afya inajenga kwa shilingi milioni 90 na Ofisi ya Rais (TAMISEMI) wanajenga nyumba za walimu zenye uwezo wa kuchukua familia mbili kwa gharama ya shilingi milioni 57 na wanajenga kwa mfumo wa force account kama mnavyojenga hapa, hii haikubaliki.”
Kutokana na kutoridhishwa na ujenzi wa chuo hicho unaosimamiwa na VETA, Mheshimiwa Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Burian asimamie ujenzi wa chuo hicho ili uweze kukamilika kwa wakati. “Mkuu wa mkoa simamia vizuri ujenzi wa chuo hiki, tunataka ukamilike kwa wakati.”
labda alikuwa anamaanisha mil 5, mlango mmoja tu hapo ni zaidi ya laki 5Hicho kibanda kwa muonekano kinazidi laki 5.
Hiki kibanda thamani yake haifiki milioni 11! Lakini pia huwezi kukijenga kwa laki 5! Labda kingekuwa ni cha mabati na mbao.Yaani ukisikia kula kwa urefu wa kamba yako ndio huku. Ni kujipakulia tu kama unapakuwq ubwabwa.
View attachment 2350427
Naunga mkono hoja. Milioni 5 inaisha kwenye hiki kibanda. Ila siyo laki 5.labda alikuwa anamaanisha mil 5, mlango mmoja tu hapo ni zaidi ya laki 5
Tuendelee kufanya kazi bila ubadhirifu!! Sio kwamba eti kipindi kile walikuwa wanapiga sana kwahiyo sasa waendelee kupiga tu !! Tanzania bila upigaji inawezekana !! Mifano tulishaiona !!Kwa hiyo Una shauri nini?
Nilidhani wewe ni Mzalendo kumbe kweli wewe ni msaka fursa, na hapa nahisi umeamua kuonesha uhalisia wa sura yako baada ya kunusa kuwa lile jambo lako limeshabutuliwa.Watu ambao hawajawahi kujenga ndio watashangaa mimi nikikiangalia hicho kibanda mbona pesa hiyo ni halali!.
JIfunze kuangalia quality kabla hatujakimbilia kupigia kelele wizi na ufisadi, ujenzi wa majengo yoyote ya umma unatanguliwa na BOQ.
- Kuchimba msingi vibarua 500,00
- Kujenga Msingi mawe zege 1,000,000
- Kuinua kuta 1,000,000
- Madirisha 3 ya PVC za Uturuki 3,000,000
- Milango miwili ya Mninga 1,000,00
- Bati ya South 1,000,000
- Tails za mable 1,000,000
- Scatting ya black granite 500,000
- Rangi ile washable 500,000
- Msimamizi 1,000,000
- 10% ya aliyetoa kazi 1,000,000 hapo kuna wizi gani?.
Kwa msio jua quality ya ujenzi, nendeni makaburi ya Kinondoni kuna kaburi pale limegharimu TZS 36.M!.
Mfano mimi natamani tomb stone yangu iwe kama ile ya ku roll, find out how much it costs, tusishabikie tuu ufisadi!.
P