Upinzani bila kubadili siasa mtapata hasara kubwa Kwa Samia..


wapinzani waliingiza emotion issue ya JPM, na wakasahau siasa ni wakati

JPM kaondoka nao😂🙋
 

kaisha lemaa!!! huyo usikute huwa anajipinga pia
 
Unajidangaya sana.
 

Yaani kifo cha JPM kimezika kabisa upinzani

Kisiasa walitakiwa wanyakue agenda zake na kumlazimisha mama aendelee nazo....walikurupuka vibaya

wangekosoa uhuru wao tu wa siasa na wananchi angehamia upande wa upinzani....na kuiacha CCM inajizoa zoa
 
Hapo sasa ndiyo unakosea. Kwa sababu mtu au watu au Watanzania wengi hawakubaliani na wewe hawajielewi au ni waoga. Ni matusi kama haya kwa wananchi ambayo wanawafanya wananchi wasiuchague upinzani. Huwezi kunitukana kuwa mimi sijielewi au mimi muoga, alafu utegemee niwe upande wake. Kutafuta kura lazima unyeyekee, uwe mpole, ubembeleze. Lakini nyie wenzetu mnasjiona ndiyo mnajuwa kila kitu, kumbe kujuwa kwenu hakuwezi kuwafanya mkavuka. Ni wananchi tu watakaowafanye mvuke.

Ebu jiangalieni kwanza. Angalia lugha mnayotumia kwa wapiga kura watarajiwa. Mkishaona makosa yenu, rudini kwa wananchi, mtumie lugha ya kistaha, ili wananchi wawaone kama mna ukomavu wa kuendesha nchi. Mtu yeyote anayetanguliza matusi mbele, mtu yeyote anayeifuata maiti kaburini na kuitukana, huyo mtu kwanza hana hoja na pili bado hajakomaa kupewa uongozi.
 
Kwani aliekwambia tulimchoka magufuli nani?. Ulimchoka wewe tu.
Hapo ndio unashangaa.

Mtu anajiropokea eti watanzania walikua wamemchoka JPM, mara watanzania wanampenda mama Samia. Sasa huo utafiti wa Watanzania kumchoka JPM aliufanya lini na wa Watanzania kumpenda mama Samia ameufanya lini?

Mtu anajiandikia hoja za jumla jumla(generalisation) unajua kabisa huyu akili hana.
 
Kinachoiweka CCM ni woga wa wananchi kupigania haki zao za kuchagua viongozi wanaowataka. Haya mengine mnayoandika huku ni bla bla tu.
Ishu nyingine Mkuu upinzani wetu Upo weak sana! Huu upinzani Wa Akina Mdee, Silinde, Katambi, Slaa, Sugu, Lema hauwezi kutufikisha popote, Opportunists Ndio wamejaa huko upinzani, wanachowaza wapate ubunge wajikusanyie mali! The Only thing inaweza kutusaidia ni CCM kumeguka vipande vipande ( Nusura litokee Hilo 2015, na tunakumbuka shida waliyopata kwenye uchaguzi)
 

unadhani kuna wapinzani hapo mkuu!!!

hilo ni genge la wahuni wenye roho za chuki na hasira.
tizama mpuuzi mmoja anadai ahakikishiwe usalama ndipo arejee,wakati alikiwepo hapa hap miezi kadhaa iliyopita,hakuguswa wala kutomaswa.
 


hapa moja ya kiongozi wa upinzani anajaribu kupaka rangi ukuta,usionekane.

ameshindwa kabisa kabisa kusoma alama za nyakati.matokeo yake michango ya wananchi hapo chini imekuwa migumu sana kwa upande wake.
 
Kwanza elewa. Mimi siko kwenye siasa kwa namna yoyote. Natoa maoni yangu kama raia asiye na chama wala upende wowote kwenye siasa za Tanzania. Upande wangu ni ''haki na fursa sawa kwa kila raia''. Kingine: naamini nchi inaweza kuendeshwa kwa mfumo wa chama kimoja na ikaenda vizuri iwapo wananchi wanajitambua na siyo woga! Kinachotakiwa ni wananchi kujua haki zao. Hili la kusema watanzania wengi ni waoga na hawajitambui ni kitu kilicho dhahiri na siyo tusi hata kidogo. Ni ukweli mchungu. Ila ''chawa'' wanaoishi kwa siasa kama wewe hili ni faida kwako hivyo hutataka liondoke. Bila hata kuzungumzia siasa, kuna haki nyingi za msingi zinakiukwa lakini wananchi wengi wamelala fofofo kama hakuna kinachotokea. Wewe hutakubali kwa sababu ujinga wetu wananchi ndiyo kula yako.
 
Amka utakojoa kitandani
 
Ukimkosoa Mama kwa hoja hana ujanja wowote , pamoja na yote huyu ni miongoni mwa walioharibu Katiba mpya hadharani na gizani , faili lake lipo , tunamwangalia tu atakachofanya
Suala ka katiba mpya binafsi naamini ni suala la wananchi au watu wasio na maslahi kabisa ya kisiasa kama kina Warioba.

Nakuhakikishia, hata leo CHADEMA au ACT wakifanikiwa kuingia madarakani kwa katiba hii hii ya 1977, hawataibadilisha. Zitabaki danadana tu.

Hakuna mwanasiasa mwenye madaraka asiyependa madaraka makubwa kama hayo yaliyomo kwenye katiba ya 1977.

Mimi naamini zaidi kwenye madaraka na maamuzi ya wananchi.
 
Umeongea ukweli..japo sina wasiwasi. Upinzani upo na watu smart sana kama Mbowe
 
Umeongea ukweli..japo sina wasiwasi. Upinzani upo na watu smart sana kama Mbowe
Upinzani siyo chama ni wananchi.

Ukitaka kuwa na upinzani imara zungumza matatizo ya wananchi na wao watakuwa upande wako.

Na mtawala ukitaka kupoteza imani ya watu, endekeza danadana za uongo, chuki, unafiki na usiwasikilize wananchi.
 
Upinzani siyo chama ni wananchi.

Ukitaka kuwa na upinzani imara zungumza matatizo ya wananchi na wao watakuwa upande wako.

Na mtawala ukitaka kupoteza imani ya watu, endekeza danadana za uongo, chuki, unafiki na usiwasikilize wananchi.
Hakuna serikali isiyokuwa na madudu yanayoonekana wazi. Mambo ya kuongelea ni mengi, na mama sio malaika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…