Binafsi naona awamu iliyopita haikufanikiwa kuua upinzani hata kama juhudi zote zilizofanywa kuanzia 2015 mpaka 2020 na ndio maana ndio maana kulihitajika msaada mkubwa wa tume na dola ili kupata kiti
Upinzani unatokana na madhaifu yanayotokana na mtawala ambapo kwa hapa kwetu bado mtawala ana madhaifu mengi sana ambayo hata hafahamu anaanzia wapi kuyarekebisha
Kwahiyo penye chaguzi huru na haki bado mtawala anaachia nchi kwa upinzani huu huu ambao mnadhani kua ume expire
Uko sawa kuhusu mapungufu ya watawala sana tuu, lakini kwa mimi ambaye nilishiriki uchaguzi na kuufuatilia ki utafiti na kwa vigezo, naona bado sana kwa upinzani kipigiwa kura za ushindi.
Nilitumia muda wa kutosha kupita kanda ya Magharibi na kuungana na watafiti wengine Kaskazini ambako ni nyumbani.
Matokeo:
Mwendazake katika utawala wake aliweza kuaminiwa na kuwaunganisha vizuri kanda ya Magharibi, Mara, Mwanza, Simiyu,Shinyanga, Geita, Kagera, kigoma, Tabora, Rukwa, Katavi na Songwe, Ruvuma, Mtwara, Iringa, Morogoro. Na alifanikiwa kuwaunganisha watanzania wanaoishi sehemu mbali mbali nchini mwetu lakini wana asili ya Mikoa hiyo. Kama ilivyo kawaida ya kisiasa upinzani kwa hizo jamii bado upo.
Maeneo yaliyokuwa na upinzani kabla:
Tunadanganyana sana humu kwenye mitandao, lakini wapiga kura waliokuwa wanaishi mkoa wa Kilimanjaro walikuwa na mawazo tofauti na sisi tunaishi nje ya Mkoa wa Kilimanjaro lakini tuna asili ya huko.
Wao walihamishia kura zao CCM, sisi tukiwa bado upinzani na tulio wataka wawe wabunge, huko majimboni, wao walikuwa hawawataki na hii ilikuwa wazi kwenye majimbo mengi tu.
Na hata maelezo ya wizi wa kura wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro ambao wanaishi Kilimanjaro hawaelewi hilo. Na hili ni kuanzia Same mpaka Siha.
Upinzani lazima upiganie kura za Mwendazake uzirithi ili kuchukua nchi. Tutabeza, tutadhihaki lakini ukweli unabaki kuwa kuna kura za kupoteza kama hatuto tupia jicho na kuzipata kura za Mwendazake.
Sent using
Jamii Forums mobile app