Upinzani bila kubadili siasa mtapata hasara kubwa Kwa Samia..

Uko sawa kuhusu mapungufu ya watawala, lakini kwa mimi na kushiriki katika kufuatilia ki utafiti wa chaguzi, naona bado sana kwa upinzani kipigiwa kura za ushindi.

Nilitumia muda wa kutosha kupita kanda ya Magharibi na kuungana na watafiti wengine Kaskazini ambako ni nyumbani.

Matokeo:
Mwendazake katika utawala wake aliweza kuaminiwa na kuwaunganisha vizuri kanda ya Magharibi, Mara, Mwanza, Simiyu,Shinyanga, Geita, Kagera, kigoma, Tabora, Rukwa, Katavi na Songwe, Ruvuma, Mtwara, Iringa, Morogoro. Na alifanikiwa kuwaunganisha watanzania wanaoishi sehemu mbali mbali nchini mwetu lakini wana asili ya Mikoa hiyo. Kama ilivyo kawaida ya kisiasa upinzani kwa hizo jamii bado upo.

Maeneo yaliyokuwa na upinzani kabla:

Tunadanganyana sana humu kwenye mitandao, lakini wapiga kura waliokuwa wanaishi mkoa wa Kilimanjaro walikuwa na mawazo tofauti na sisi tunaishi nje ya Mkoa wa Kilimanjaro lakini tuna asili ya huko.

Wao walihamishia kura zao CCM, sisi tukiwa bado upinzani na tulio wataka wawe wabunge, huko majimboni, wao walikuwa hawawataki na hii ilikuwa wazi kwenye majimbo mengi tu.

Na hata maelezo ya wizi wa kura wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro ambao wanaishi Kilimanjaro hawaelewi hilo. Na hili ni kuanzia Same mpaka Siha.

Upinzani lazima upiganie kura za Mwendazake uzirithi ili kuchukua nchi. Tutabeza, tutadhihaki lakini ukweli unabaki kuwa kuna kura za kupoteza kama hatuto tupia jicho na kuzipata kura za Mwendazake.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unamaanisha Kua CCM ilipata kura za halali chaguzi ya 2020 ngazi ya madiwani mpaka raisi?
 
Unaposema unahitaji kuleta utawala bora lazima uanze na katiba.

Unaposema uboreshe mifumo ya haki za binadamu lazima uanze na katiba.

Katiba inasema nchi ni ya ujamaa na kujitegemea unatekeleza vipi sera za kibepari bila kuondoa kwanza hiyo blah blah ?

Ndiyo maana ccm wanaendesha nchi kwa mihemko na matamanio binafsi ya rais kwa sababu sera zao zote hazina msingi wa kikatiba.

Unaposema utaleta taasisi imara utaunda vipi taasisi imara bila kuwa na katiba inayoweka misingi ya taasisi imara ?
Kumbuka kuna mambo yanasemwa kwasababu wako nje ya system au hayana manufaa kwao. Nambie ni kitu gani chenye manufaa kwao na kinaumiza wananchi walichowahi kukipinga kwa dhati??

Wakiingia hakuna namna yoyote unaweza kuwalazimisha wayatekeleze.

Kitu pekee kinachoweza kupelekea baadhi ya mabadiliko ni mgongano wa maamuzi hasa ikitokea mtawala hana majority ndani ya bunge.
 
Kumbuka kuna mambo yanasemwa kwasababu wako nje ya system au hayana manufaa kwao. Nambie ni kitu gani chenye manufaa kwao na kinaumiza wananchi walichowahi kukipinga kwa dhati??

Wakiingia hakuna namna yoyote unaweza kuwalazimisha wayatekeleze.

Kitu pekee kinachoweza kupelekea baadhibya mabadiliko ni mgongano wa maamuzi hasa ikitokea mtawala hana majority ndani ya bunge.
Ufisadi.
Haki za binadamu
Kodi na mifumo ya kodi isiyo rafiki
 
Unamaanisha Kua CCM ilipata kura za halali chaguzi ya 2020 ngazi ya madiwani mpaka raisi?
Siko tayari kuzungumzia sehemu ambazo siku ya kupiga kura na kehesabu kura sikuwepo. Lakini bila tashweishi yeyote ile naweza zungumzia jimbo lá Hai, ambapo zimepigwa kura na kuhesabiwa nikiwepo.
Na nikutaarifu hivi sisi Kilimanjaro tuna network ya ukweli kwenye uchaguzi sababu tupo pamoja kuhusu Wabunge. Tuna wasiwasi kidogo Jimbo la Moshi Mjini ambapo wazawa 68% Wanyika ni 32%.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kodi? Wapinzani wabunge hawalipi kodi
Umewahi wasikia wakisema wabunge walipe kodi?
Kwenye uchaguzi mkuu walikuwa na ajenda ya kodi sasa hivi wapinzani hawako bungeni.

Pili bunge lililopita kulikuwa na mapendekezo ya wabunge na mafao kukatwa kodi mojawapo ya watu walioikubali hoja hiyo ni Upendo Peneza.

CCM wote walipinga.
 
Ufisadi.
Haki za binadamu
Kodi na mifumo ya kodi isiyo rafiki
Kwamba upinzani ukiwa madarakani hakutakuwa na ufisadi?!

Hivi mkuu unadhani ufisadi ni kwamba pesa huwa zinaliwa na upepo au watu kutoka nje ya nchi??

- Ufisadi ni watawala wao wenyewe kutafuna pesa za umma kwa manufaa yao, hata vyama vya upinzani wamekuwa na tabia hiyo sana hasa linapokuja suala la Ruzuku. Ruzuku imeleta migogoro mikubwa sana ndani ya vyama vya siasa.

Nyalandu aliwahi kuwa Waziri wa mali asili na utalii, akaunda umoja wapigaji akiwemo Yeye, Lembeli ( M/kiti kamati ya bunge maliasili na utalii ), Msigwa ( waziri kivuli). Tena Msigwa akikuwa anamtetea mnoo kwasababu wanapiga wote.

Hapa muhimu ni kuwepo mifumo ya kuwajibishana, sasa unafikiri mtawala anaweza kuweka mfumo wa kujiwajibisha??

- Kuhusu haki za binadamu pia ni hitaji la wananchi lakini kwa jinsi watawala walivyo tayari mpaka kuua ili kulinda madaraka, usitegemee sana mwanasiasa kuwa fair kwa kiwango hicho.

Mfano mzuri ni baadhi ya madaraka ndani ya vyama, hakuna asiyeona namna watu wanaojaribu kutaka kugombea nafasi za juu wanavyopata tabu. Sasa imagine yakiwa madaraka ya nchi ( keki ya taifa ) ambayo wangekuwa hata na uwezo wa kukwepa kuwajibika?

- Kodi ndio Afya ya serikali yenyewe. Muhimu ni kuongeza wigo wa kodi ili zilipwe na watu wengi kwa unafuu kuliko kuwaongezea kodi watu walewale kila mwaka.

Usitegemee mtu umemkabidhi bakuli ajipakulie, ataacha salama hilo bakuli ili siku nyingine alikose.

Mimi naamini mabadiliko halisi yanatokana na wananchi wenyewe ambao ndio wawe na power ya kuwaendesha wanasiasa watakavyo tofauti na sasa tunavyosubiria kwa matumaini kutoka kwa mtawala au chama fulani!!
 
Kodi? Wapinzani wabunge hawalipi kodi
Umewahi wasikia wakisema wabunge walipe kodi?
Umeamua kuchagua eneo dogo tu la wao kulipa kodi je hukusikia juu ya wao kupiga sera na sheria za kodi rafiki kwa wananchi ?
 
Mimi naamini mabadiliko halisi yanatokana na wananchi wenyewe ambao ndio wawe na power ya kuwaendesha wanasiada watakavyo tofauti na sasa tunavyosubiria mtawala au chama fulani!!
Kama hoja yako ni mfumo tunarudi kwenye hoja yao ya msingi ya system overhaul jambo ambalo wamelipigania for years
 
Nimekukatalia kutumia wishful thinking tusiwanyime fursa ya kuongoza simply ccm wanaiba na wao wataiba kwa kigezo kuwa ni wanasiasa tu.

Hoja yako unalenga kuipa uhalali ccm wa kuiba na kuendelea kutawala kwa misemo ya kijuha ya heri zimwi likujualo.
 
Umeamua kuchagua eneo dogo tu la wao kulipa kodi je hukusikia juu ya wao kupiga sera na sheria za kodi rafiki kwa wananchi ?

Eneo dogo kivipi?
Kama mpaka Mama ntilie wanalipa kodi
Wao wabunge wasilipe na unaona ni jambo dogo?
 
Nimekukatalia kutumia wishful thinking tusiwanyime fursa ya kuongoza simply ccm wanaiba na wao wataiba kwa kigezo kuwa ni wanasiasa tu.
Sijasema mtu anyimwe nafasi ya kuongoza. Ninachosema ni kuwa dalili ya mvua ni mawingu.

Hakutakuwa na jipya sana kama ukubwa wa madaraka utabaki mikononi mwa mwanasiasa, haijalishi wa chama gani hasa linapokuja suala la madaraka na pesa.

Ripoti ya CAG ni uthibitisho wa hilo. Mwenye kingi katafuna sana, mwenye kidogo naye katafuna vile vile.

Mfano CDM yasemekana kuna mtu sijui kanunua gari binafsi kwa pesa za ruzuku na hajulikani mpaka sasa na hakuna ufafanuzi.
 
CDM wao hata kwenye uchaguzi walizunguka nchi kuomba kura wakiingia madarakani wapunguze madaraka ya raisi wayarejeshe kwa wananchi.

Wamekuwa wakipigania kupunguza chain ya wanasiasa kwenye utawala kwa kuondoa mfumo wa wakuu wa wilaya wa kuteuliwa na wakurugenzi waajiriwe na halmashauri zenyewe on merits badala ya wanasiasa.

Wewe huoni hili lingeleta tija kwenye usimamizi wa raslimali za wananchi?
 
Mkuu hizo ni stori za kuombea kura tu. Hata CCM walisema watagawa milioni 50 kwa kila kijiji na ahadi lukuki.

Hao wakuu wa wilaya na wakurugenzi are working against their favours ndio maana hawapendi.

Ingekuwa mkurugenzi au mkuu wa mkoa anapatikana kama wanavyopatikana Mameya wasingewapinga yaani maana na wao pia wangekuwa na uwezo wa kuweka wa kwao.
 
Tusiwahukumu kwa makosa ya ccm.

Hii hoja yako ni fallacious huwezi ukamhukumu John A kisa anafanana na John B aliyetenda kosa.
 
Mkuu hizo ni stori za kuombea kura tu. Hata CCM walisema watagawa milioni 50 kwa kila kijiji na ahadi lukuki.

Hao wakuu wa wilaya na wakurugenzi are working against their favours ndio maana hawapendi.

Ingekuwa mkurugenzi au mkuu wa mkoa anapatikana kama wanavyopatikana Mameya wasingewapinga yaani maana na wao pia wangekuwa na uwezo wa kuweka wa kwao.
Na wao wanapigania hao watu wawe wakuchaguliwa ili wawe na uwezo kuwajibika moja kwa moja kwa wananchi
 
Kwamba upinzani ukiwa madarakani hakutakuwa na ufisadi?!

Hivi mkuu unadhani ufisadi ni kwamba pesa huwa zinaliwa na upepo au watu kutoka nje ya nchi??

- Ufisadi ni watawala wao wenyewe kutafuna pesa za umma kwa manufaa yao, hata vyama vya upinzani wamekuwa na tabia hiyo sana hasa linapokuja suala la Ruzuku. Ruzuku imeleta migogoro mikubwa sana ndani ya vyama vya siasa.

Nyalandu aliwahi kuwa Waziri wa mali asili na utalii, akaunda umoja wapigaji akiwemo Yeye, Lembeli ( M/kiti kamati ya bunge maliasili na utalii ), Msigwa ( waziri kivuli). Tena Msigwa akikuwa anamtetea mnoo kwasababu wanapiga wote.

Hapa muhimu ni kuwepo mifumo ya kuwajibishana, sasa unafikiri mtawala anaweza kuweka mfumo wa kujiwajibisha??

- Kuhusu haki za binadamu pia ni hitaji la wananchi lakini kwa jinsi watawala walivyo tayari mpaka kuua ili kulinda madaraka, usitegemee sana mwanasiasa kuwa fair kwa kiwango hicho.

Mfano mzuri ni baadhi ya madaraka ndani ya vyama, hakuna asiyeona namna watu wanaojaribu kutaka kugombea nafasi za juu wanavyopata tabu. Sasa imagine yakiwa madaraka ya nchi ( keki ya taifa ) ambayo wangekuwa hata na uwezo wa kukwepa kuwajibika?

- Kodi ndio Afya ya serikali yenyewe. Muhimu ni kuongeza wigo wa kodi ili zilipwe na watu wengi kwa unafuu kuliko kuwaongezea kodi watu walewale kila mwaka.

Usitegemee mtu umemkabidhi bakuli ajipakulie, ataacha salama hilo bakuli ili siku nyingine alikose.

Mimi naamini mabadiliko halisi yanatokana na wananchi wenyewe ambao ndio wawe na power ya kuwaendesha wanasiasa watakavyo tofauti na sasa tunavyosubiria kwa matumaini kutoka kwa mtawala au chama fulani!!
Naona umeandika vitu vingi vingine umepatia vingine umekosea.

Ufisadi; hii hoja yako ime-base kwamba palipo na watawala lazima wizi uwepo, kwako kama CCM wanaiba, na upinzani lazima wataiba pia, ukazungumzia utafunwaji wa ruzuku ku-justify hii hoja yako.

Hivi yule CAG anavyotoa hati safi kwa baadhi ya vyama huwa ni maigizo yale?, siamini hilo. CAG anakuwa ameridhishwa na matumizi ya ruzuku ndio maana anafanya vile, sasa kama hawa jamaa wana hati safi, nini kinawashinda wakiongoza nchi wasiwe clean pia? wapewe nafasi badala ya kuwahukumu kabla.

Tena umezungumzia kiongozi wa upinzani kukaa madarakani muda mrefu kama kigezo kingine cha kutafuta upigaji, hapa nako nakupinga, kiongozi anakaa muda mrefu madarakani kwa kuchaguliwa na wajumbe wa chama chake, kama ana sifa mbovu kwanini wamchague?

Ukweli ni kwamba wanaridhishwa na utendaji wake ndio maana wanaendelea kumchagua, au kama una ushahidi wa kiongozi "aliyepiga" na bado anaendelea kuchaguliwa niambie, sio rumours za mtaani, hizo hazikosekani.

Hapo kwenye haki za binadamu napo umetumia mfano wa wengine kuwahukumu wengine, this to me is not fair, kwa mawazo yako haya ni sawa na una "play some sort of mind games" kuwaambia watu kuliko kuwapa hao wapinzani bora tubaki na hii CCM yetu, nop.
 
Mkuu hizo ni stori za kuombea kura tu. Hata CCM walisema watagawa milioni 50 kwa kila kijiji na ahadi lukuki.

Hao wakuu wa wilaya na wakurugenzi are working against their favours ndio maana hawapendi.

Ingekuwa mkurugenzi au mkuu wa mkoa anapatikana kama wanavyopatikana Mameya wasingewapinga yaani maana na wao pia wangekuwa na uwezo wa kuweka wa kwao.
Kwa vyovyote kwenye uchaguzi huwa tunachagua story lakini story inayoeleweka na kutekelezeka.

Kama mtu katupigia story miaka 50 na bado tunamwamini huoni kosa ni la kwetu wenyewe kuamini uongo ule ule kwa miaka nenda rudi ?
 
Back
Top Bottom