Upinzani bila kubadili siasa mtapata hasara kubwa Kwa Samia..

Upinzani bila kubadili siasa mtapata hasara kubwa Kwa Samia..

Kwahiyo unataka tutoke kwenye mjadala kitaifa turudi kwenye mjadala wa kichama ?
Nambie ni kitu gani ambacho kinawanufaisha wao halafu ni maumivu kwa mwananchi walishawahi kukipinga kwa dhati???
 
Kwa vyovyote kwenye uchaguzi huwa tunachagua story lakini story inayoeleweka na kutekelezeka.

Kama mtu katupigia story miaka 50 na bado tunamwamini huoni kosa ni la kwetu wenyewe kuamini uongo ule ule kwa miaka nenda rudi ?
Hata sioni kosa letu, tunaporwa haki zetu ndio sababu, "chama dola" hakina jipya tena.
 
Hakuna kitu kinaamua siasa kama 'wakati'..
Wanasiasa wazuri ni wale wanaojua nyakati zinavyobadilika na kwenda na wakati uliopo ...

Watanzania walikuwa wamechoshwa mno na siasa za Magufuli...na uongozi wake kiujumla..
Kubanwa Uhuru wa kuongea
Kufokewa na kukaripiwa
Kutoa matamko Kwa ukali..
Kuzungumza Peke yake..
Kutokukosolewa ..
Kukosekana Kwa mijadala na majadiliano..
Na mengi yaliyoenda na hayo..

Ujio wa Samia umebadili siasa Kwa ujumla..
Samia hafoki anaongea Kwa upole na kushawishi ..
Anazungumzia mazungumzo na mijadala..
Hazuii kukosolewa badala yake anakaribisha kukosolewa Kwa serikali yake..

Kikubwa zaidi ni Mwanamke ..
Watu wanamtazama Kwa 'kumhurumia'..
Na kumpa 'all benefits of the doubts'..
Na kuelewa kuwa anapambana na mfumo dume...
Watu wengi wanaju hii nchi ngumu na wanajua Samia atahangaika kuweza kumudu ...still wanafarijika na 'kurudi Kwa Uhuru wa kuongea na kukosoa'..

Sasa kama wapinzani wanafikiri siasa za kumshambulia Rais na serikali yake zinalipa bado kama enzi za JK watakuwa wanakosea sana....
Sana Sana wataonekana 'hawana adabu'
Na wanajaribu 'kumuonea' 'Rais Mwanamke' baada ya 'kidume ' JPM
'kuwakomesha hadi wakaufyata'..

Siasa za kipindi hiki zinahitaji ubingwa wa hoja kwenye mijadala ya kistaarabu..bila
Kuwa 'boa' wananchi ambao walishachoshwa na Magufuli Sana Sana wanataka 'mzunguko' wa hela urudi kama ule wa JK....

Kuleta siasa za ulalamishi..
Siasa za uwana harakati.
Na siasa za Ku target watu na kuwashambulia bila kujua ..'role halisi' ya hao watu ni siasa ambazo zinakuwa 'outdated ' so fast...

Watu wanampenda Samia sio Kwa sababu ni kiongozi bora.. wanampenda Kwa sababu wanaona 'nafuu inakuja'
Upinzani ukicheza siasa za kuleta 'distraction'wakati watu wanasubiri nafuu ije ..hasira za wananchi zinaweza washukia wao.....

Siasa inaendana na nyakati.. wapinzani wanasoma nyakati??
Mbona hujafungua code umeona nini?

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Soma vizuri, hakuna kiongozi aliyewahi kukubalika na watu wote wakati wote, lakini pia hakuna kiongozi aliyekataliwa na watu wote wakati wote.

Kama ulimchoka wewe, hilo una uhakika nalo 100% na atakayekupinga ana matatizo. Lakini kusema alishachokwa na wengine, ni jambo lenye ukweli kwa assumptions na hypothesis, lakini ukubali wapo waliompenda hasa wenye maisha duni na yeye siku zote alijitafsiri kuwa hao ndio kipaumbele chake na hasira zake ziliwashukia wakwepa kodi na wala rushwa na waonevu ikiwemo wanyonyaji mpaka kwenye madini kule.

Sasa u-balance, usilazimishe kuwa kila mtu alimchoka, ulimchoka wewe.
Waliompenda Magufuli ni hasa wale wenye maisha duni? Nikuhakikishie JPM alipendwa na watu wa kada zote, walio duni na wasio duni pia. Ieleweke kwamba hulka ya binadamu ni complex huwezi kumtathmini binadamu kwa vigezo rahisi rahisi kama uwepo wa mzunguko wa hela mtaani. Hakuna viongozi waliokuwa easy-going na walioachia hela mtaani kama Mwinyi na JK, lakini kuna sehemu ya watanzania inawaona kama miongoni mwa viongozi wabovu kuwahi kuiongoza Tanzania. Kinyume chake JPM amependwa na watanzania takribani asilimia kubwa kwa sababu zingine zinazogusa mioyo ya watu. Kuna mambo ya msingi yanayogusa mioyo ya watu zaidi ya pesa, na ni kama vile JPM aliyajua, na ndiyo maana huku mtaani watu wengi wanaamini JPM ni kiongozi bora kabisa wa nchi yetu kupata baada ya Nyerere.
 
Jamaa umeandika vema. Yyte atakaeanza kumkosoa mama watu watamuona ana nongwa na ni muonevu na watahoji kwa nn aliufyata kwa mbabe jiwe? Mfano ni yule dada kule tweeter ambae watu walimbatiza jina la Ferain baada ya kumkosoa mama huku kwa jiwe akiwa ameufyata na vijitivii vyake vya mkononi kupigwa ban.

Wapinzani this time watakua ni loosers. Ishara nyingne niionayo ni bunge. Wabunge washasoma alama za nyakati na sasa wamejitwisha kazi ya upinzani kukosoa serikali na mama kaahidi hilo. So upinzani hautakua na hoja tena maana kila kitu kinafanyika. Mfano ji akina GWAJIMA, NAPE, GAMBO, MAKAMBA MUHONGO N.K
Sema Sababu inajulikana Tz iko na wapumbafu wengi yaani Leo
mBunge wa ccm awe mtetezi wa wananchi badala ya cccm yake na watu wanamuamini

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Ukimkosoa Mama kwa hoja hana ujanja wowote , pamoja na yote huyu ni miongoni mwa walioharibu Katiba mpya hadharani na gizani , faili lake lipo , tunamwangalia tu atakachofanya
Watu wanataka kujificha kwenye kichaka cha uanamke ikiwa mwenyewe kasema hakuna ubongo tofauti Kati ya mwanamke na Mwanaume kinachotakiwa mama afanye kazi afuate sheria zaidi ya hapo atapwaya

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Chama kinachojiita "chama dola" kina hoja gani mpaka wapinzani wapate shida kushindana nacho?

"Mimi ni Rais mwenye jinsia ya kike" sounds confident, nakushangaa mleta mada unamdharau, wanawake siku zote wanapigania haki sawa, kwanini wewe unawashusha?

Samia atapingwa tu, kama alivyokuwa akipingwa Magufuli, na Kikwete, na bahati nzuri Mbowe ameshaonesha hiyo dalili, huyo mama Katiba Mpya imeshamshinda bado unataka abembelezwe!.

Huwezi kumlazimisha mtu abadili "approach" ya siasa zake kwa kisingizio chepesi "wanamuonea mama", ikulu halei watoto, anaongoza taifa linalofuata mfumo wa vyama vingi.

Akishindwa kuvumilia hayo akaanza kuwaweka ndani hatakuwa na tofauti na mtangulizi wake, kama kweli amekomaa kisiasa lazima awe na "thick skin" hizo ndio price you pay for being there at the top, not the other way round like you preach.
Huu ndio ukweli

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Nambie ni kitu gani ambacho kinawanufaisha wao halafu ni maumivu kwa mwananchi walishawahi kukipinga kwa dhati???
Hili swali nimeshakujibu kule juu labda kama umeishiwa maswali mengine ya kuuliza useme.
 
Wengi sasa hivi (ukiwemo wewe na wana CCM wengi tu) wanakiri kuwa Magufuli aliharibu. Nakunukuu:
''Watanzania walikuwa wamechoshwa mno na siasa za Magufuli...na uongozi wake kiujumla..
Kubanwa Uhuru wa kuongea
Kufokewa na kukaripiwa
Kutoa matamko Kwa ukali..
Kuzungumza Peke yake..
Kutokukosolewa ..
Kukosekana Kwa mijadala na majadiliano..
Na mengi yaliyoenda na hayo..''

Mwisho wa nukuu.
Kama wakati wa Magufuli watanzania walikuwa kwenye hali mbaya namna hii (jambo ambalo ni kweli) mbona hawakufanya mabadiliko? Je, hata wakijenga hoja kipindi hiki ni nini kitawafanya watanzania wawasikilize na kuiondoa CCM?
My take: Upinzani hata uwe makini na wenye hoja namna gani, bila wananchi kujielewa na kuacha woga ni kazi bure. Kinachoendelea kuiweka CCM madarakani siyo udhaifu wa viongozi wa upinzani wala uimara wa hoja wa CCM bali wananchi wengi kutojielewa na kuwa woga.
Shukrani sana kwa hii comment unajua kuna watu hawataki kuamini kwamba Nchi hii bado iko na wajinga wengi wasiojua nafasi zao

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Jamaa umeandika vema. Yyte atakaeanza kumkosoa mama watu watamuona ana nongwa na ni muonevu na watahoji kwa nn aliufyata kwa mbabe jiwe? Mfano ni yule dada kule tweeter ambae watu walimbatiza jina la Ferain baada ya kumkosoa mama huku kwa jiwe akiwa ameufyata na vijitivii vyake vya mkononi kupigwa ban.

Wapinzani this time watakua ni loosers. Ishara nyingne niionayo ni bunge. Wabunge washasoma alama za nyakati na sasa wamejitwisha kazi ya upinzani kukosoa serikali na mama kaahidi hilo. So upinzani hautakua na hoja tena maana kila kitu kinafanyika. Mfano ji akina GWAJIMA, NAPE, GAMBO, MAKAMBA MUHONGO N.K
Sawa kinachotakiwa ni hoja kinzani itoke ndani au nje sawa tu. Na mtu ambaye si mbinafsi atasaidia upinzani ukue na unaweza kukua pia.
Watanzania kwa ujumla waowanatakiwa kufahamu hili kwa faida ya nchi na sio kundi...
 
Uko vizuri Mkuu na ushahidi wa hili ni UPORAJI wake wa uchaguzi.
Watu tunamfurahia Mama kwa sababu Tulishamchoka MAGUFULI na Siasa zake za kikatili,
Ukweli ni kwamba CCM imechokwa kuliko kitu chochote duniani.
Kama mtoa mada anaamini Mama anapendwa waruhusu Katiba Mpya na Tume huru ya uchaguzi.

Nakuhakikishia Samia hawezi kwenda kinyume na matakwa ya CCM,na moja ya takwa kubwa la CCM Ni dhuluma kwa kila Jambo.

Mama mtago wake Ni mdogo tu,ama awe upande wa CCM ama awe upande wa wananchi.

Ikiwa Kikwete mwanasiasa nguli ndani ya CCM walimdhibiti suala la Katiba mpya ingawa yeye ndio alielianzisha likamshinda na heshima yake ikashuka sembuse Mama mchanga katika Siasa?

Kama CCM wanajiamini kuwa mama anapendwa waruhusu Katiba na Tume ili chaguzi ziwe za haki waone mziki wa Upinzani.
Mimi nimeichoka CCM katika maisha usione hivi,hata wanipe Lori la fedha ntawasaliti tu.
 
Ni kweli kabisa
It's either walipaswa wakae kimya huku wakisubiri the right time to attack her as i am sure kila mtawala huwa na flaws ambazo hata wananchi wanaweza kuziona
Ila kwa sasa ni mapema sana wao kupinga as mama ameanza vizuri, ni kama anaonekana atarudisha tumaini lilipotea!sasa wao wanavyopinga na kushambulia inaonekana it,s either hawako wise au wameishiwa hoja so they are just trying so hard to survive
Ni mtazamo wangu tu jamani chondechonde wanachadema msinipopoe kwa mawe manake hamkawii,
Unawashaurije Chadema wanapoambiwa wapeleke Hoja zao kwa Shibuda

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Umeongea ukweli..japo sina wasiwasi. Upinzani upo na watu smart sana kama Mbowe
Wakati Magufuli anaingia madarakani tulisikia maneno Kama haya,kuwa Sasa upinzani umekufa na akapewa kila Jina,Tingatinga,mtumbua majipu,mbadala wa Nyerere,kiboko ya mafisadi n.k
Amekufa kaitwa kila Jina baya hapa duniani,Hadi watu wanatamani kwenda kujisaidia juu ya kaburi lake.

Kwa kifupi pamoja na viongozi wake lakini ukweli Ni kwamba CCM imechokwa.

Mama anafurahiwa tu kwa sababu mkatili Magufuli kaondoka.Lakini mama Hana jipya Ni Kama akina Kikwete tu na Mwendazake wote Ni CCM.
 
Wengi sasa hivi (ukiwemo wewe na wana CCM wengi tu) wanakiri kuwa Magufuli aliharibu. Nakunukuu:
''Watanzania walikuwa wamechoshwa mno na siasa za Magufuli...na uongozi wake kiujumla..
Kubanwa Uhuru wa kuongea
Kufokewa na kukaripiwa
Kutoa matamko Kwa ukali..
Kuzungumza Peke yake..
Kutokukosolewa ..
Kukosekana Kwa mijadala na majadiliano..
Na mengi yaliyoenda na hayo..''

Mwisho wa nukuu.
Kama wakati wa Magufuli watanzania walikuwa kwenye hali mbaya namna hii (jambo ambalo ni kweli) mbona hawakufanya mabadiliko? Je, hata wakijenga hoja kipindi hiki ni nini kitawafanya watanzania wawasikilize na kuiondoa CCM?
My take: Upinzani hata uwe makini na wenye hoja namna gani, bila wananchi kujielewa na kuacha woga ni kazi bure. Kinachoendelea kuiweka CCM madarakani siyo udhaifu wa viongozi wa upinzani wala uimara wa hoja wa CCM bali wananchi wengi kutojielewa na kuwa woga.
Waliokuwa wanalalamika sauti zao ziliishia kwenye kibuyu ila sauti za wapambe zilienea kote. Ni watu wachache walipata kujua pande mbili za shilingi. Watu waiokuwa wamechoshwa ni wale waliokua na fursa ya kujua ukweli na kuutafuta na kuuchambua. Wanafiki wenye uelewa walitikisatikisa tu mikia yao hawakuthubutu kubweka.
 
Back
Top Bottom