Upinzani bila kubadili siasa mtapata hasara kubwa Kwa Samia..

Upinzani bila kubadili siasa mtapata hasara kubwa Kwa Samia..

Magufuli ametufundisha mengi,ametuonyesha madhara ya ubabe,na huko cdm ubabe ndoo uliko,mwenyekiti hawezi kubadilika amekuwa wa kudum,Sasa huyo akishika dola tutamtoaje? wapinzani wetu ni wabinafsi.afadhari hiyo hiyo ccm kuliko wapinzani tulio nao

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
 
Wenzetu wana "political strategists" wanaolipwa pesa nyingi kusaidia kwenye nyakati za mashaka kama hizi.

Wasome vizuri upepo, ili tanga walielekeze upande sahihi. Naona kina Maria wameanza kupotea, hawajui washike lipi na kwa nini? Making unreasonable demands left right and centre.
 
Hakuna kitu kinaamua siasa kama 'wakati'..
Wanasiasa wazuri ni wale wanaojua nyakati zinavyobadilika na kwenda na wakati uliopo ...

Watanzania walikuwa wamechoshwa mno na siasa za Magufuli...na uongozi wake kiujumla..
Kubanwa Uhuru wa kuongea
Kufokewa na kukaripiwa
Kutoa matamko Kwa ukali..
Kuzungumza Peke yake..
Kutokukosolewa ..
Kukosekana Kwa mijadala na majadiliano..
Na mengi yaliyoenda na hayo..

Ujio wa Samia umebadili siasa Kwa ujumla..
Samia hafoki anaongea Kwa upole na kushawishi ..
Anazungumzia mazungumzo na mijadala..
Hazuii kukosolewa badala yake anakaribisha kukosolewa Kwa serikali yake..

Kikubwa zaidi ni Mwanamke ..
Watu wanamtazama Kwa 'kumhurumia'..
Na kumpa 'all benefits of the doubts'..
Na kuelewa kuwa anapambana na mfumo dume...
Watu wengi wanaju hii nchi ngumu na wanajua Samia atahangaika kuweza kumudu ...still wanafarijika na 'kurudi Kwa Uhuru wa kuongea na kukosoa'..

Sasa kama wapinzani wanafikiri siasa za kumshambulia Rais na serikali yake zinalipa bado kama enzi za JK watakuwa wanakosea sana....
Sana Sana wataonekana 'hawana adabu'
Na wanajaribu 'kumuonea' 'Rais Mwanamke' baada ya 'kidume ' JPM
'kuwakomesha hadi wakaufyata'..

Siasa za kipindi hiki zinahitaji ubingwa wa hoja kwenye mijadala ya kistaarabu..bila
Kuwa 'boa' wananchi ambao walishachoshwa na Magufuli Sana Sana wanataka 'mzunguko' wa hela urudi kama ule wa JK....

Kuleta siasa za ulalamishi..
Siasa za uwana harakati.
Na siasa za Ku target watu na kuwashambulia bila kujua ..'role halisi' ya hao watu ni siasa ambazo zinakuwa 'outdated ' so fast...

Watu wanampenda Samia sio Kwa sababu ni kiongozi bora.. wanampenda Kwa sababu wanaona 'nafuu inakuja'
Upinzani ukicheza siasa za kuleta 'distraction'wakati watu wanasubiri nafuu ije ..hasira za wananchi zinaweza washukia wao.....

Siasa inaendana na nyakati.. wapinzani wanasoma nyakati??
Nakubaliana na wewe kwa asilimia 100
 
Siku Mbowe akiwa smart, nitarudi upinzani kabla jua halija chomoza.

Wewe mwana siasa uliye pevuka lazima ufahamu kuwa Mwendazake alikuwa na constituency yake, na kwa hiyo kisiasa lazima uirithi.
Chadema ina mpango gani kisiasa kufaidika na kifo cha Mwendazake?

Mwendazake, aliichukua Constituency ya Chadema, watu wa chini wote kimaisha na kibiaashara lakini hakuwapa manufaa ya kuridhisha, hapo ndio chama kinazoa wanachama na wafuasi.
Una maanisha nini kusema"constituency"?
 
Soma vizuri, hakuna kiongozi aliyewahi kukubalika na watu wote wakati wote, lakini pia hakuna kiongozi aliyekataliwa na watu wote wakati wote.

Kama ulimchoka wewe, hilo una uhakika nalo 100% na atakayekupinga ana matatizo. Lakini kusema alishachokwa na wengine, ni jambo lenye ukweli kwa assumptions na hypothesis, lakini ukubali wapo waliompenda hasa wenye maisha duni na yeye siku zote alijitafsiri kuwa hao ndio kipaumbele chake na hasira zake ziliwashukia wakwepa kodi na wala rushwa na waonevu ikiwemo wanyonyaji mpaka kwenye madini kule.

Sasa u-balance, usilazimishe kuwa kila mtu alimchoka, ulimchoka wewe.
Hawa wanaosema watu walimchoka ni watu gani? Wakati asilimia kubwa ya wapiga kura, wanyonge na maskini walimkubali... hata huku mtaani hilo linajidhihirisha. Kuna mabaya yalifanyika sikatai lakini kuwa watu walimchoka jamaa awe specific watu gani haswa....
 
Wakati Magufuli anaingia madarakani tulisikia maneno Kama haya,kuwa Sasa upinzani umekufa na akapewa kila Jina,Tingatinga,mtumbua majipu,mbadala wa Nyerere,kiboko ya mafisadi n.k
Amekufa kaitwa kila Jina baya hapa duniani,Hadi watu wanatamani kwenda kujisaidia juu ya kaburi lake.

Kwa kifupi pamoja na viongozi wake lakini ukweli Ni kwamba CCM imechokwa.

Mama anafurahiwa tu kwa sababu mkatili Magufuli kaondoka.Lakini mama Hana jipya Ni Kama akina Kikwete tu na Mwendazake wote Ni CCM.
Umemaliza Mkuu 🙏 You have spoken my mind
 
Nadhani haupo sahihi.. constituency ni majimbo yanayotoa wawakilishi wa kwenda bungeni. Sio political meaning..Mzee umeanza kamba [emoji23]
Constituency - a group of people with shared interests or political opinions.

Tulikuwa na Machinga upande wa upinzani kabla ya Mwendazake chini ya 2015, lakini Mwendazake akawabadilisha 2020 na kuendelea wako upande wa CCM.
 
Wenzetu wana "political strategists" wanaolipwa pesa nyingi kusaidia kwenye nyakati za mashaka kama hizi.

Wasome vizuri upepo, ili tanga walielekeze upande sahihi. Naona kina Maria wameanza kupotea, hawajui washike lipi na kwa nini? Making unreasonable demands left right and centre.
Kwani Maria ni nani kwenye siasa za Tanzania ?
 
Hakuna kitu kinaamua siasa kama 'wakati'..
Wanasiasa wazuri ni wale wanaojua nyakati zinavyobadilika na kwenda na wakati uliopo ...

Watanzania walikuwa wamechoshwa mno na siasa za Magufuli...na uongozi wake kiujumla..
Kubanwa Uhuru wa kuongea
Kufokewa na kukaripiwa
Kutoa matamko Kwa ukali..
Kuzungumza Peke yake..
Kutokukosolewa ..
Kukosekana Kwa mijadala na majadiliano..
Na mengi yaliyoenda na hayo..

Ujio wa Samia umebadili siasa Kwa ujumla..
Samia hafoki anaongea Kwa upole na kushawishi ..
Anazungumzia mazungumzo na mijadala..
Hazuii kukosolewa badala yake anakaribisha kukosolewa Kwa serikali yake..

Kikubwa zaidi ni Mwanamke ..
Watu wanamtazama Kwa 'kumhurumia'..
Na kumpa 'all benefits of the doubts'..
Na kuelewa kuwa anapambana na mfumo dume...
Watu wengi wanaju hii nchi ngumu na wanajua Samia atahangaika kuweza kumudu ...still wanafarijika na 'kurudi Kwa Uhuru wa kuongea na kukosoa'..

Sasa kama wapinzani wanafikiri siasa za kumshambulia Rais na serikali yake zinalipa bado kama enzi za JK watakuwa wanakosea sana....
Sana Sana wataonekana 'hawana adabu'
Na wanajaribu 'kumuonea' 'Rais Mwanamke' baada ya 'kidume ' JPM
'kuwakomesha hadi wakaufyata'..

Siasa za kipindi hiki zinahitaji ubingwa wa hoja kwenye mijadala ya kistaarabu..bila
Kuwa 'boa' wananchi ambao walishachoshwa na Magufuli Sana Sana wanataka 'mzunguko' wa hela urudi kama ule wa JK....

Kuleta siasa za ulalamishi..
Siasa za uwana harakati.
Na siasa za Ku target watu na kuwashambulia bila kujua ..'role halisi' ya hao watu ni siasa ambazo zinakuwa 'outdated ' so fast...

Watu wanampenda Samia sio Kwa sababu ni kiongozi bora.. wanampenda Kwa sababu wanaona 'nafuu inakuja'
Upinzani ukicheza siasa za kuleta 'distraction'wakati watu wanasubiri nafuu ije ..hasira za wananchi zinaweza washukia wao.....

Siasa inaendana na nyakati.. wapinzani wanasoma nyakati??
Shetani anamshauri malaika.
 
Constituency - a group of people with shared interests or political opinions.

Tulikuwa na Machinga upande wa upinzani kabla ya Mwendazake chini ya 2015, lakini Mwendazake akawabadilisha 2020 na kuendelea wako upande wa CCM.
Nikwambie ukweli 2020 Magufuli hakuwa na constituency yoyote zaidi ya kuwa na polisi, tume ya uchaguzi na waratibu wa wizi wa kura.

Machinga hao hao aliowatoza kitambulisho cha 20k ndiyo hao hao waliomtandika kwenye sanduku la kura.

Magufuli alitumia miaka mitano kuumiza watu na kujenga barabara na madaraja hiyo constituency aliipata wapi ?

Unazungumzia kura za uchaguzi ulioporwa from the start kama kipimo cha kukubalika kwa Magufuli, are you insane ?
 
You guys have you ever had an engagement on policy issues with politicians of Tanzania? .

I am a very close friends to many in opposition ? I also have many politicians pro government, for smooth operation of my businesses, I seldom engage both on political issues and governance .

This engagement has led me to believe that, there is a thin line separates both.

Together tuimarishe serikali yetu, nafikiri sio kweli kabisa tutakuwa salama opposition wakitawala.
Tulichagua opposition Hai, uongozi wote kwa miaka 20, Kwa tulioyapitia leo wakazi wanaoishi Hai wanamwita Sábaya kijana wao.

Watanzania echos zimebadilika sana.
Unaleta mfano wa Sabaya kwenye hoja nyeti za kitaifa ?

You are not serious
 
Naamini kama ungekuwa na close personal engagement na pande zote mbili na ukawa mkweli naamini usingeandika uliyo andika. Kuna taabu kubwa. Njia aliyoitumia Mwendazake sikuipenda, lakini nia na ujasiri wake kutaka kupunguza matatizo ya integrity namuunga mkono.

Wengine hatuzungumzi kwa kufikiri au kushawishiwa, tuna mabinti na vijana wa kuwazaa katika highest echelon in government leadership.

We have to revisit our ethos.
Unazungumzia ETHOS hakuna utawala ulikuwa wa hovyo kimaadili kama utawala wa JPM.

yeye mwenyewe hakuwa na maadili ya kiuongozi mbele ya umma.

Hakuzingatia haki za binadamu, isipokuwa kulikuwa na haki za wanaccm wanaomuunga mkono.

Aliongoza kuteua viongozi wasio na maadili kwa jamii Masalia yake bado yapo jana tumesikia mkuu wa wilaya akimtukana mwananchi, yeye ametukana wananchi for 5 good years.

Kuna wakuu wa wilaya walikuwa wanachapa viboko watu hadharani.

Kuna watu walipotea kama sindano.

Hizi ndiyo ethos unazopenda wewe ?
 
Back
Top Bottom