Upinzani mnapoambiwa mwakani hakuna mbunge wa upinzani atakayerudi muwe mnaelewa

Upinzani mnapoambiwa mwakani hakuna mbunge wa upinzani atakayerudi muwe mnaelewa

ibesa mau

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2015
Posts
2,109
Reaction score
1,707
Vyama vya upinzani na wanachama wake wasipochukua hatua kwa serikali na wasimamizi wa uchaguzi Nina maanisha watendaji kata ,vijiji na mitaa mwakani hali itakuwa mbaya sana, hakuna mbunge wala diwani hata mmoja atakayeshinda mwakani.

Waache kufikiria CCM ina huruma, CCM na serikali yake imedhamiria kabisa kuuwa upinzani na kuturudisha kwenye chama kimoja.

Wapinzani watambue kwamba serikali ya CCM ilikuwa inatest mitambo yake kuona kama watendaji wa kata na mitaa na vijiji wataweza, na wameweza, mwakani hali itakuwa mbaya zaidi.

Asiyesikia la mkuu .........., kwa kuwa hawa watendaji ni watu wanao ishi katika maeneo yao ichukuliwe hatua dhidi yao, hata kuwazomea mitaani ,kuwanyima ushirikano na kuwatenga kabisa kwa vitendo vyao waone aibu ili mwakani wasirudie tena kuwanyima watu democrasia wananchi, kwa sababu watu walijipanga kupambana kwenye majukwaa ya siasa kwa hoja,

Kama umeguswa na hali jinsi inavyoenda nchini weka ushauri kwa serikali
 
CCM inarudi kwenye ubora wake ndiyo maana wananchi sasa wameamua kuiunga mkono! Heko Mh. Magufuli kwa kazi nzuri ya kuleta maendeleo!
Wanaiungaje mkongo, wakati mmeweka Mpira kwapani , wangeacha watu washindane kwenye majukwaa ya siasa ili tuone hayo maneno yako,lakini vinginevyo huwezi kuwaaminisha watu kwamba wananchi wameamua kuiunga mkongo ccm
 
Thubutu, Mbowe, Zitto, et.al wanawalisha matango poli wenyeviti wa mitaa tu, wenyewe kwenye kinyanganyiro cha ubunge watashiriki mapemaa! Fomu zao watajaza kwa makini na kuzihakiki kabisa ili kuondoa makosa!
 
Kwa kuwa wametusaidia kuchagua viongoz nasi tutawasaidia kuwaapisha.
 
Upinzani sio wabunge wala wenyeviti wa mitaa. Kama huamini subiri mwaka 2021. Tanzania kutakuwa na upinzani wa ajabu tena wa ndani kwa ndani. Upinzani sio chadema wala ACT Wazalendo bali ni chuki na hasira dhidi ya tabaka utawala usioheshimu haki na utu wa mwanadamu. Kuna waziri mmoja amepost twiter akasema wasiotii sheria ni bora waliwe na fisi/mamba. Bado namtafakari tu. Tena waziri kabisaaaa.
 
CCM inarudi kwenye ubora wake ndiyo maana wananchi sasa wameamua kuiunga mkono! Heko Mh. Magufuli kwa kazi nzuri ya kuleta maendeleo!

Ni kweli, ccm vyombo vya dola ndio huwaita wananchi. Uzuri tunajiamini kwani watu wanajua ukweli ulivyo hata kama wako kimya lakini wanaambiana plan B. Gawaneni madaraka sisi tunabaki na watu tena kwa ushawishi na sio vitisho na mabavu. Hamna muda mtajua nguvu ya umma inamaanisha nini.
 
..Waziri wa Manbo ya Sebuleni na Chumbani alinukuliwa akisema..Mwakani tunanunua magarai yenye kufanaya watu wajikune, kutoka kwa mabeberu, tunayasambaza kila mkoa na kila wilaya, na moja ya idara yetu muhimu tutaiongezea posho.
 
............................................... Kuna waziri mmoja amepost twiter akasema wasiotii sheria ni bora waliwe na fisi/mamba. Bado namtafakari tu. Tena waziri kabisaaaa.
Mtaje tumjue hapa upo salama.
 
Thubutu, Mbowe, Zitto, et.al wanawalisha matango poli wenyeviti wa mitaa tu, wenyewe kwenye kinyanganyiro cha ubunge watashiriki mapemaa! Fomu zao watajaza kwa makini na kuzihakiki kabisa ili kuondoa makosa!

Kwa mwenendo huu nani atawapigia kura? Kwa taarifa yako wananchi ndio wamepuuza huo uchaguzi, hao viongozi wa upinzani inabidi watii wananchi wanachotaka. Ccm haina shida wao amri ya rais itawapa madaraka lakini hawatapata madaraka toka kwa wananchi bali vyombo vya dola.
 
Kwa mwenendo huu nani atawapigia kura? Kwa taarifa yako wananchi ndio wamepuuza huo uchaguzi, hao viongozi wa upinzani inabidi watii wananchi wanachotaka. Ccm haina shida wao amri ya rais itawapa madaraka lakini hawatapata madaraka toka kwa wananchi bali vyombo vya dola.
Magufuli anajiona Mungu wa nchi hii. Alipigwa vumbi la wazee wa Ruangwa na ziara ikaishia hapohapo.
 
Tumerudi kwenye mfumo wa hatari zaidi, mfumo wa chama kimoja. Wabunge wengi ambao watakuwa si chaguo la wananchi, watakufa kabla hawajakalia kiti Cha ubunge kwa miaka mitatu
 
Unachekesha kabisa tembea mitaani utajua uhalisia wa mambo! Upinzani tayari umeshakufa tayari

Unadhani ninaishi kwenye mwezi hivyo huko mtaani siendi? Watu wako kimya maana wanahofia kutekwa, kupigwa risasi nk. Ila wamedhihirisha wanacheka mdomoni lakini ukweli wanao rohoni, nadhani uliona mwitikio wa wananchi kwenye kujiandikisha, na wala hawakushawishiwa na chama chochote cha siasa. Ile ni ishara ya dhahiri umma unajitambua. Tisheni wananchi, watekeni, bakeni box la kura, lakini umma unajitambua.
 
Kwa nchi ambazo upinzani upo hai,hiki kilichotokea tayari jana na leo mitaa kadhaa kwenye miji mikubwa ingekuwa moshi mzito wa matairi umetawala.

Bongo usipoingia mitandaoni Ni kama hakuna kinachoendea nchini.

Hiyo 2020 hata mitandao itazimwa wiki yote ya uchaguzi.
 
Back
Top Bottom