Upinzani mnapoambiwa mwakani hakuna mbunge wa upinzani atakayerudi muwe mnaelewa

Upinzani mnapoambiwa mwakani hakuna mbunge wa upinzani atakayerudi muwe mnaelewa

Nilidhani uko neutral. Kumbe sio. Nikusifu kwa kujificha kidogo.
Tukiwatenga hao watendaji ,Barua za utambulisho kwenda Mamlaka za Serikali inayosimamiwa na CCM tutazipata wapi?
Ukienda kutaka mkopo bank unaambiwa let's Barua ya mtendaji.
Hatutakwama?
Tutakwama
 
Unaposema "wapinzani" mchukue tahadhari hao wapinzani ni nani?

Au kuna watu wao walizaliwa tu kuwa wapinzani?
 
Vyama vya upinzani na wanachama wake wasipochukua hatua kwa serikali na wasimamizi wa uchaguzi Nina maanisha watendaji kata ,vijiji na mitaa mwakani hali itakuwa mbaya sana, hakuna mbunge wala diwani hata mmoja atakayeshinda mwakani.

Waache kufikiria CCM ina huruma, CCM na serikali yake imedhamiria kabisa kuuwa upinzani na kuturudisha kwenye chama kimoja.

Wapinzani watambue kwamba serikali ya CCM ilikuwa inatest mitambo yake kuona kama watendaji wa kata na mitaa na vijiji wataweza, na wameweza, mwakani hali itakuwa mbaya zaidi.

Asiyesikia la mkuu .........., kwa kuwa hawa watendaji ni watu wanao ishi katika maeneo yao ichukuliwe hatua dhidi yao, hata kuwazomea mitaani ,kuwanyima ushirikano na kuwatenga kabisa kwa vitendo vyao waone aibu ili mwakani wasirudie tena kuwanyima watu democrasia wananchi, kwa sababu watu walijipanga kupambana kwenye majukwaa ya siasa kwa hoja,

Kama umeguswa na hali jinsi inavyoenda nchini weka ushauri kwa serikali
Muda utasema
 
Back
Top Bottom