Ligogoma
JF-Expert Member
- Aug 27, 2010
- 3,502
- 6,460
Ninachoona hapa ni Watanzania wenyewe tumepumbaa kuendana na aina ya siasa tunayofanya!Vyama vya upinzani na wanachama wake wasipochukua hatua kwa serikali na wasimamizi wa uchaguzi Nina maanisha watendaji kata ,vijiji na mitaa mwakani hali itakuwa mbaya sana, hakuna mbunge wala diwani hata mmoja atakayeshinda mwakani.
Waache kufikiria CCM ina huruma, CCM na serikali yake imedhamiria kabisa kuuwa upinzani na kuturudisha kwenye chama kimoja.
Wapinzani watambue kwamba serikali ya CCM ilikuwa inatest mitambo yake kuona kama watendaji wa kata na mitaa na vijiji wataweza, na wameweza, mwakani hali itakuwa mbaya zaidi
Asiyesikia la mkuu .........., kwa kuwa hawa watendaji ni watu wanao ishi katika maeneo yao ichukuliwe hatua dhidi yao, hata kuwazomea mitaani ,kuwanyima ushirikano na kuwatenga kabisa kwa vitendo vyao waone aibu ili mwakani wasirudie tena kuwanyima watu democrasia wananchi, kwa sababu watu walijipanga kupambana kwenye majukwaa ya siasa kwa hoja,
Kama umeguswa na hali jinsi inavyoenda nchini weka ushauri kwa serikali
Tunafanya siasa za Uchama na kuacha Utaifa, ikiwa na maana kuwa chama hata kifanye jambo gani baya kwa taifa kwa kuwa wewe ni shabiki/mwanachama tu wa chama hicho utaona sawa tu. Na hii ndiyo advantage ya wanasiasa wa Tanzania, wanadanganya raia kuwa kuna vyama haviwajibiki na madai yao ukikiwajibisha hicho chama hakuna tena Tanzania.
Hii ni hatari mno!
Watumishi wa serikali ndiyo hasa walipaswa wawe na utaifa uliopitiliza lakini wao ndio makondoo wa kufa mtu.
Hii ni hatari kwa sababu, siasa za sasa tunaziona na hakuna wa kumuwajibisha mwenzake sababu ya uchama. Ingekuwa nchi ambazo raia wana utaifa, tungekuwa tunazungumza mengine.
Eti mtu anahubiri kabisa iwe mvua iwe jua iwe mchana iwe usiku mimi ni chama fulani daaaah! Ndiyo matokeo yake hayo, watu wanateua viongozi raia wamekaa kimya kisa ni chama fulani kinafanya hivyo. Hwawazii taifa lao linakwenda wapi!
Tuanze kuhubiri utaifa, vijana waelewe kuwa vyama vinabadilika lakini taifa letu lipo pale pale. Chama kikiboronga tupa kule weka kingine, nacho kikiboronga pia weka pembeni mpaka kitapatikana chenye afadhali na hata wanasiasa wakiona hivyo nao watabadilika.
Tusimame na Tanzania yetu, vyama tupa kule