Upinzani Tanzania una matatizo? Vyama havina Succession Plan hivyo vina Usultani! CHADEMA kuna Usultani? Usultani huu Utakiinua au Utakiangamiza?

Hakika Chadema kinawanyima usingizi...Mbowe ni Alama ya mapambano ya kupigania Haki Nchini


Mtaandika ujinga mpaka lini!? Kubalianeni na hali halisi kwa sasa.

Na tunasubiri Bandiko kuhusu mgombea Makamu Mwenyekiti...ambaye ni mpango wa Mungu Mh. Mbunge Ndg. Lissu..

Wacha safu zipangwe...

2020 kuna Jasusi mbobevu ataivusha CCM iliyoharibiwa ya Dk Bashiru hivyo wacha safu zipangwe kimkakati...

Hatari sana..
 
We nae ushagakua mlamba makari..ya ccm...succession plan ya chama chochote kile inaitaji uwanja sawa wa kisiasa.sasa kunavokua hamna unategemea watapataje hao wapinzani succession plan? Play fare uone
 
Kuhusu usultani wa viongozi, hii inatokana na malengo ya kiongozi, hali ya siasa na msimamo wa kiongozi kwa serikali ya ccm, kiongozi akiwa laini ccm watamuunga mkono hata kwa nguvu ya polisi kama lipumba, na hapa wanachama wanyemsimamo ukihama chama, kwa upande was kiongozi asiyeiunga mkono serikali atapigwa vita na serikali ya ccm kwa kila namna ikiwa ni pamoja na kumkwamisha kibiashara sasa hapa kwa wanachama wenye lengo LA kuendelea na mapambano hawatakuwa tayari kubadili kiongozi kisa tuu ameongoza kwa muda mrefu, na hapa atakayeumia ni yule anayedhani kuwa mwana chama ni lazima use kiongozi. Hatuwezi badili mchezaji mzuri uwanjani ili kumjaribu wa bench
 
Ukifuatilia namna hicho kipengele kilivyo-evaporate na ukimya wa hao wabwekaji unapata picha namna kulivyo ndani ya hivyo vyama.

Yaani Slaa,Lisu wote wali-side na Mbowe na wakatetea huo ujinga.

Wenye chama waliogopa nini hicho kipengele kujadiliwa na kufanyiwa marekebisho ama kuondolewa kupitia mchakato halali?

Toka lini kipengele kisipojadiliwa kinajiondoa automatically?
 
Pascal Mayalla Asante kwa bandiko lako bora kabisa na muafaka kwa wakati huu wa siasa za ushabiki na sio hoja.

Tukumbuke kuwa CHADEMA walikuwa hawana mpango wowote wa kufanya uchaguzi mwaka huu.

Mpaka walipoanza kupokea barua mfululizo toka kwa msajili wa Vyama vya siasa akihoji kuhusu katiba yao...

Kwa maana hiyo hiki wanachokifanya ni kiini macho tu kumridhisha msajili,

Sawa na uchaguzi serikali za mtaa Magufuli hakuwa tayari kwa uchaguzi Katiba ya Jamhuri ndio ilimbana...

Pengine udhaifu huu ulikuepo toka muda mrefu ila ulikuwa unafichwa na umahiri wa Dr Slaa,

Sasa Dr Slaa ametoka ndio tunaona rangi halisi ya CHADEMA chini ya Mbowe..

Kukua kwa CHADEMA kutategema na Chuki ya wanachi dhidi ya Magufuli, kinyume na hapo CHADEMA kinaenda kudumaa.

Mbowe ni Dikteta
Mbowe ni Sultan
 
Eti 2020 mshindi ameshajulikana.
Ina maana hatma ya pumzi yake unayo?hivi unajua hadi kufikia2020 nikaribu?bado safari ni ndefu watu wanazidi kuomba mungu.
Naomba niishie hapo tadhali.
 
Ndio maana mtu yoyote ambaye hatakiwi na Mbowe hupewa majina yote mabaya ili mradi kuhalalisha udhaifu wao.
 
Ukimsema Mbowe unaitwa Ccm ukiisema serikali unaitwa msaliti hii nchi inaonyesha jinsi gani ilivyo na watu wengi wanaopenda itikadi na si maslahi ya taifa.
Hii inaonyesha jinsi gani Tanzania tulivyo wanafiki.!
 
Umeongea ukweli mtupu na wapinzani wa ukweli ni watu waliozaliwa miaka ya 2000
 
Asante sana Mkuu. Umefunga kazi.
 
Kwanza wapinzani hasa Chadema mana ndiyo iliyoumiza watu wengi wakiamini kuwa kwa ni chama cha upinzani chenye dira hawajui kuwa Watanzania ndio wanaotaka mabadiliko na sio wenyeviti wao.

Mbowe anafikiri kuwa yeye ndiye anayetaka mabadiliko.
Mbowe na wapambe wake wameihujumu Demokrasia ndani ya Chama na kusababisha Chama kukosa uelekeo.
Chama kilichoonyesha Demokrasia mwanzoni Leo kimekua cha kisultani.
Chama kilichopambana na ufisadi leo hakina agenda.

Tujaribu tu kufuatilia kule Mara, Mbeya ,Shinyanga na kwingine kuna watu wanaonyesha wazi kukerwa na hujuma za Uchaguzi wa serikali za mitaa lakini hata nyumbani kwa Mwenyekiti Mbowe hakuna rapsha yoyote ya kuonekana kuwa wamekerwa. He,hapo kuna dalili yoyote ya Mbowe kujenga Ideology ya chama kwa wapiga kura wa jimbo lake au ni janja janja ya kuwatumia akina Dr Slaa ,Lowasa ,Sugu,Mdee, Marehemu,Ndesamburo,Lema , Mnyika, Msigwa ,Rwakatare, marehemu Wangwe na wengine kwenye majimbo yao na kuonyesha mwamko wa Chama?

Kinachotakiwa kwa sasa kwa watu wenye nguvu ya kiuandishi kama wewe ndugu yangu Paskali Mayalla ni kuwaeleza watanzania kwa bayana madhara ya kubaki ndani ya Chadema chini ya Uenyekiti wa Mbowe.
Leo hii chama chini ya Mbowe kimejidhihirisha kuwa ni chama cha Kiukoo wala sio kikabila mana Wachaga wengi kwa sasa walitamani Mbowe aonyeshe Demokrasia iliyopiganiwa kwa muda mrefu kwa vitendo.
Ndio maana Komu ametishiwa kufukuzwa kwenye chama na kuzuiwa kusema chachote.

Hakuna mtu wa kabila lolote (wakiwemo wachaga wanaosingiziwa kuwa ndio wamiliki wa Chadema) mwenye nia njema na Demokrasia ya nchi hii atakayeendelea kumuunga mkono Mbowe na Chama chake cha ukoo wake na kuendelea kuteseka kwa bila sababu.

Sioni Sababu ya mtu kama Komu mbunge wa Moshi vijiiini ,Jafari Moshi Mjini, Selasini wa Rombo, kuendelea kunaki Chadema na kukosa Ubunge 2020 kwa manufaa ya Mbowe aliyebainisha kuwa wote ni wasaliti isipokuwa yeye peke yake.
Wabunge hao na wengine ni vyema wakachukua hatua ya kumfuata Polepole na kurudi CCM ili 2020 wagombee kupitia CCM na kurudi Bungeni. Kwa hoja zao na michango yao walivyolitumikia taifa hili kupinga ufisadi hakika JPM atawapa nafasi zaidi ya kuwatumikia watanzania.

Watanzania wote tuwakatae watu wanaong'ang'ania madaraka kwani ndio wanaoleta vurugu na udikteta kwenye nchi Changa.

Mbowe ameinajisi Demokrasia kwa Wazi.
Watasema kwa nini sio vyama vingine!! Nawajibu kuwa Chadema kirefu chake ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo.
Mbowe ameshindwa kusimamia maendeleo kwa majimbo waliyoshinda.
Mbowe ameshindwa kuonyesha neno Demokrasia kwa vitenda. Ameinajisi Chadema.
Chadema chini ya Mbowe hakina uhalali wa kupigania Demokrasia na maendeleo ya nchi hii.

Hata Lisu asipoteze muda wake kwa ajili ya Mbowe. Mbowe amekua mjanja sana kuwatanguliza watu maarufu na wanaokubalika kwenye jamii ili watu wakiwafuata na kujiunga kwenye chama aseme kuwa yeye ndio amejenga Chama.
Lisu ndiye mpinzani anayekubalika kwa sasa kuliko mtanzania yeyote. Mbowe anataka amtumie ili likitokea lolote ajitambe kuwa yeye ndiye anayejenga chama kwa fedha zake.
Akina Mdude Chadema wanahatarisha maisha yao kwa maslahi ya Mbowe.

Kama kuna mtu anayeona hatari imayotokana na Mbowe kumiliki chama chini ya mgongo wa Wachaga ni vyema akajitoa Chadema na kuondokana na hisia za ukabila ili Mbowe abaki na familia yake.

Upinzani wa kweli utabaki mioyoni mwa watanzania mpaka watakapokuja watanzania kama Mtei aliyeanzisha Chama na kuweka muda wa ukomo wa uongozi kwa kuonyesha mfano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…