Upinzani Tanzania una matatizo? Vyama havina Succession Plan hivyo vina Usultani! CHADEMA kuna Usultani? Usultani huu Utakiinua au Utakiangamiza?

Nitajie paskal successesion plan waliyonayo ccm
Ulikuja kutafuta plan au kumtuhumu mbowe hawez kuongoza cdm KWA mafanikio?
 
Uko sahihi kabisa zidumu fikira za mwenyekiti bado zipo sana
 
Tatizo CDM hawaaminiani kila mmoja anamuoneshea mwenzie kidole ndio maana wanaona bora abaki huyohuyo Muasisi awakokote mpaka pale watakapoaminiana
 
Paskali,
Usife moyo endelea huenda ukakumbukwa. Ila nasikitika kusema; Kama unataka kweli kujijenga mwambie wa kwetu asiogope kivuli. Weshamwambia CDM iko ICU hivyo asihofu anayepumulia mashine. Wala asiuondoe mpira wa pumzi bali ajiendee uwanjani aweke uchaguzi huru aone kama kuna taahira atakayekichagua chama kinachopumulia mashine.
Kinyume cha hapo, yu people are just living a wishful thinking life. Chama kongwe hivyo haklifai kuyaishi maisha hayo tena. Mwambiye aweke mpira kati na refa makini ajipime mwenyewe. Hamtakuwa na mithali hizi humu JF.
 
P. Naamini wewe ni mwachama hai wa ccm na usisahau kuwa ccm Ina wenyewe wewe ukiwa sio mmojawapo! Hii slogan ya " ccm Ina wenyewe" inatenda sambamba na cdm Ina wenyewe pia! Kwa maana nyingine acha kutumika kwa Mara nyingine kwa kuitumia kalamu yako kuwabomoa viongozi wa upinzani na vyama vyao Kama ulivyofanya mwaka 2015 kwani hukufaidika kwa lolote zaidi ya kubezwa na kuitwa kuhojiwa ulipotaka kujitambua! Njia hii unayopitia Sasa ili uteuliwe si sahihi hata kidogo kwani naamini hutakuwa tayari kuitwa mpumbavu mbele ya halaiki pale utakapofanya asiyotaka mteuaji!
 
Poor observation! Hivi huwezi hata siku moja kujenga hoja bila kuongoza ukabila! Najua upo kwa special mission ya kuchochea vurugu za ukabila kwani vurugu zinaru kwenye veins zako wewe mrundi! Na utateseka Sana kuikamilisha hiyo kazi ya kuchochea ukabila na vurugu kwani hutoikamilisha!
 
Paskali unashangaza sana hivi kweli hujui vyama vya upinzani vinapitia nini?Mikutano vimezuiwa ila CCM inafanya,kesi ndio mikutano ya vyama vya upinzani kila Mkoa,wilaya wapinzani wako Mahakamani,wengine wamefungwa kwa kuonewa,polisi na wapinzani wanafukuzana,Tume Uchaguzi ,na Wakurugenzi ndio hao,watendaji kata wanakimbia na fomu yote hayo huyaoni?,
 
Kama issue ya msingi ni succession plan basi ni Tatizo kote hata CCM. Kwa maoni yangu ulitakiwa ulizungumzie zaidi ndani ya CCM kuliko upinzani kwa kuwa CCM wameng"ang'ania na kuhodhi madaraka hali ambayo imeadhiri mafanikio na maendeleo ya nchi kwa kila hali.

Mifano mdogo tu.... Kama CCM Wangekuwa na succession plan mtu kama Polepole asingekuwa hapo alipo, Bashiru asingekuwa Katibu Mkuu na huenda No. 1 wa sasa na aliyepata wasingetatanua kwenye lile jumba jeupe.
 
Kama kuna jambo ambalo cdm hawataki kulizungmzia ni kuhusu kubadil katiba kumruhusu Dj aendelee kutawala,

Ikiwa t hawajatawala wanabadil katiba je wakipewa Madaraka?
 
Taratibu za MTU kutoka upinzani kuamia ccm kupewa nafasi ya ubunge instantly plus uwaziri, chadema na ccm hakuna wa kumcheka mwenzake
 
Umeongea point bila ya kuegemea upande wowote, ukiangalia jinsi mpinzani anahamia ccm na kupewa nafas ya kugombea unagundua Luna tatizo mahali, Kwa hy ccm hawawez tupia chadema lawama wote wanafanana
 
Mkuu hawa jamaa wao wapo perfect kwa kila jambo awataki kukosolewa wala kushauriwa ila wao ndio wamejipa majukumu ya kukosoa na kushauri kwa wengine, nahisi ni chama cha MA GENIUS.


Angalizo subiria matusi na kejeri kutoka kwa wafuasi wao.

Mwisho Chadema ni zaidi ya KAOLE
 
Ushauri ni ku expand resources zenu...na mgawane equally mapato...watu hawatang'ang'ania madaraka..anyway this thread is useful kwa wao kufanya reflection...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…