Lowassa pamoja na kupendwa sana kwa kweli alikuwa dhaifu mno 2015. Tena mno, kimawazo (hakuwa na mvuto wa hoja) na hata kiafya (enzi za siha njema zilishampita). Kwangu mie hata JK kuhakikisha Lowassa hawi Rais ilikuwa ni kumsaidia rafiki yake ambaye alikuwa anajua undani wake. Lowassa asingeweza kuongoza vizuri na pengine hata afya yake ingetetereka zaidi na zaidi iwapo angekuwa Rais. Ni afadhali anavyoenenda kwa namana hii.
Ninawahakikishia Membe akibahatika kugombea kupitia upinzani - kuna uwezekano mkubwa sana wa upinzani kushinda uchaguzi ama kupata asilimia zaidi ya 40 za kura zote kwa Mwaka huu. Membe anakuja na approach nzuri, yaani analenga kupata msimamo wa kimataifa kuhusu chaguzi bora na zilizo huru (Fair and Free Election). Membe ameshaanza kuieleza Jumuiya ya Kimataifa kuwa Tume ya Uchaguzi ya Chama sio huru. Yaani ni MCCM halafu anajisema kuwa chombo cha kumpa ushindi yeye mwenyewe iwapo akipitishwa na CCM kugombea hakipo huru.
Ajabu sana kwani amekuwa akisema hili kwa muda tu na sio jana tu. Inawezekana kabisa huko huko Tume wanamtonya kuwa "Mkuu hatuko huru!". Sasa ukushaanza kuongelea kuwa Tume sio huru na kuvuta Jumuiya ya Kimataifa kwa jambo hilo ujue kuna watu unawaeleza siri zako za ndani na unawakaribisha waingilie. Kwa vyovyote vile iwapo Uchaguzi huu yatatokea maafa sio mbaya utawala huu kuja kuwajibishwa na vyombo va kimataifa hata kwa mauaji ya kimbari. Membe amelenga mbali sana - naamini akipata nafasi akaanza kuongea kwenye Kampeni atabadilisha sana upepo.
Membe akiongea kwa kukosoa Chama Chake kuhusu ujenzi wa mamiundo mbinu bila kujali hali za kipato kwa wananchi na kutamka wazi wazi wafanyakazi wamenyanyasika ni nani hatamsikia. Membe akitoa hadi njema kwa wananchi dhidi ya habari za kujenga mamiundombinu za awamu hii nani atasikiliza mambo ya mamiundo mbinu. Membe akieleza kwa ufasaha kuhusu zao la korosho lilivyodukuliwa na kuwasababishia wananchi wake ni nani hatamwelewa?
Membe akiongelea kupotea kwa akina Ben Saa Nane kwa kutoa siri anayoijua kuhusu hilo nani hatavutiwa naye? Membe akiongelea na kuwataja walimtwanga Tundu Lissu mirisasis kibao, ni nani hatamwelewa? Kumbukeni unaweza kutenda mema mengi lkn ukatenda baya moja tu likakuangusha katika maisha yako yote ya kutenda mema. hebu mchuku askofu aliyeponya wat na watu, siku ikatokea bahati mbaya tu akambaka muumini si na uaskofu wake anaweza kuukosa?
Mie ninaamini kabisa sasa CCM inaelekea kudondoka kwa kishindo kikubwa sana. Iwapo CCM itashinda mwaka huu basi itakuwa imeshinda kwa mbinde sana. Na isiposhinda itakuwa imejitakia yenyewe kwani asiyesikia la mkuu huvunjika guu. Wananchi walikuwa wana mengi ya kusikilizwa na awamu hii - yamepuuzwa kwa kiburi cha kufikiri ni awamu inayopendwa kumbe ni hovyo kabisa na imejawa na udikiteta lukuki.