Uchaguzi 2020 Upinzani ukimweka Membe itakuwa tofauti kubwa na ilivyokuwa kwa Lowassa! Watashinda

Uchaguzi 2020 Upinzani ukimweka Membe itakuwa tofauti kubwa na ilivyokuwa kwa Lowassa! Watashinda

Mnambua

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2020
Posts
246
Reaction score
233
Lowassa pamoja na kupendwa sana kwa kweli alikuwa dhaifu mno 2015. Tena mno, kimawazo (hakuwa na mvuto wa hoja) na hata kiafya (enzi za siha njema zilishampita). Kwangu mie hata JK kuhakikisha Lowassa hawi Rais ilikuwa ni kumsaidia rafiki yake ambaye alikuwa anajua undani wake. Lowassa asingeweza kuongoza vizuri na pengine hata afya yake ingetetereka zaidi na zaidi iwapo angekuwa Rais. Ni afadhali anavyoenenda kwa namana hii.

Ninawahakikishia Membe akibahatika kugombea kupitia upinzani - kuna uwezekano mkubwa sana wa upinzani kushinda uchaguzi ama kupata asilimia zaidi ya 40 za kura zote kwa Mwaka huu. Membe anakuja na approach nzuri, yaani analenga kupata msimamo wa kimataifa kuhusu chaguzi bora na zilizo huru (Fair and Free Election). Membe ameshaanza kuieleza Jumuiya ya Kimataifa kuwa Tume ya Uchaguzi ya Chama sio huru. Yaani ni MCCM halafu anajisema kuwa chombo cha kumpa ushindi yeye mwenyewe iwapo akipitishwa na CCM kugombea hakipo huru.

Ajabu sana kwani amekuwa akisema hili kwa muda tu na sio jana tu. Inawezekana kabisa huko huko Tume wanamtonya kuwa "Mkuu hatuko huru!". Sasa ukushaanza kuongelea kuwa Tume sio huru na kuvuta Jumuiya ya Kimataifa kwa jambo hilo ujue kuna watu unawaeleza siri zako za ndani na unawakaribisha waingilie. Kwa vyovyote vile iwapo Uchaguzi huu yatatokea maafa sio mbaya utawala huu kuja kuwajibishwa na vyombo va kimataifa hata kwa mauaji ya kimbari. Membe amelenga mbali sana - naamini akipata nafasi akaanza kuongea kwenye Kampeni atabadilisha sana upepo.

Membe akiongea kwa kukosoa Chama Chake kuhusu ujenzi wa mamiundo mbinu bila kujali hali za kipato kwa wananchi na kutamka wazi wazi wafanyakazi wamenyanyasika ni nani hatamsikia. Membe akitoa hadi njema kwa wananchi dhidi ya habari za kujenga mamiundombinu za awamu hii nani atasikiliza mambo ya mamiundo mbinu. Membe akieleza kwa ufasaha kuhusu zao la korosho lilivyodukuliwa na kuwasababishia wananchi wake ni nani hatamwelewa?

Membe akiongelea kupotea kwa akina Ben Saa Nane kwa kutoa siri anayoijua kuhusu hilo nani hatavutiwa naye? Membe akiongelea na kuwataja walimtwanga Tundu Lissu mirisasis kibao, ni nani hatamwelewa? Kumbukeni unaweza kutenda mema mengi lkn ukatenda baya moja tu likakuangusha katika maisha yako yote ya kutenda mema. hebu mchuku askofu aliyeponya wat na watu, siku ikatokea bahati mbaya tu akambaka muumini si na uaskofu wake anaweza kuukosa?

Mie ninaamini kabisa sasa CCM inaelekea kudondoka kwa kishindo kikubwa sana. Iwapo CCM itashinda mwaka huu basi itakuwa imeshinda kwa mbinde sana. Na isiposhinda itakuwa imejitakia yenyewe kwani asiyesikia la mkuu huvunjika guu. Wananchi walikuwa wana mengi ya kusikilizwa na awamu hii - yamepuuzwa kwa kiburi cha kufikiri ni awamu inayopendwa kumbe ni hovyo kabisa na imejawa na udikiteta lukuki.
 
Mkuu Lowasa alikuwa ni national figure yule nje na hapo alikuwa na majority suport ya mikoa mitatu [kama unaakili utanielewa] hata kabla ya kampeni

Kiufupi itahitaji miaka mingine hamsini upinzani kupata mgombea mwenye ushawishi kama mzee lowasa
 
Mkuu lowasa alikuwa ni national figure yule nje na hapo alikuwa na majority suport ya mikoa mitatu [kama unaakili utanielewa] hata kabla ya kampeni

Kiufupi itahitaji miaka mingine hamsini upinzani kupata mgombea mwenye ushawishi kama mzee lowasa
Alikuwa akipendwa tu tu yaani nyota yake ilikuwa kali. Huyu Membe huyu atakuja na ushawishi pamoja na kupendwa kidogo. Ila inakusudiwa atachofanya ndiyo kitaupandisha upinzani.
 
Alikuwa akipendwa tu tu yaani nyota yake ilikuwa kali. Huyu Membe huyu atakuja na ushawishi pamoja na kupendwa kidogo. Ila inakusudiwa atachofanya ndiyo kitaupandisha upinzani.
kuna uwezekano upinzani wakawa wamejipanga vizuri zaidi mwaka huu kuliko wakati wa 2015
 
Ishu ni wakati akiwa sisiemu ilikua fair...dah! Siasa bhana! Na watu wanamuamini kabisa..
 
Uchambuzi mzuri lowasa nyota yake ilikuwa kali mno na alitokewa tu kupendwa ila hakuwa na nguvu ya hoja personally hasa kulingana na Afya yake alitegemea sana ushawishi wamapenzi na mizizi aliyokwisha isimika pamoja na yote he was a man alitikisa sana japo nguvu haikutosha....

Membe nadhani anatakiwa kuja na nguvu zaidi ya hoja maana nyota yake kisiasa ni ya kawaida na hana mizizi na nguvu sana kama alivokuwa nayo lowasa.....yeye hoja dhidi ya ccm ndio inayoweza mnyenyua walau akaleta ushindani
 
Uchambuzi mzuri lowasa nyota yake ilikuwa kali mno na alitokewa tu kupendwa ila hakuwa na nguvu ya hoja personally hasa kulingana na Afya yake alitegemea sana ushawishi wamapenzi na mizizi aliyokwisha isimika pamoja na yote he was a man alitikisa sana japo nguvu haikutosha......membe nadhani anatakiwa kuja na nguvu zaidi ya hoja maana nyota yake kisiasa ni ya kawaida na hana mizizi na nguvu sana kama alivokuwa nayo lowasa.....yeye hoja dhidi ya ccm ndio inayoweza mnyenyua walau akaleta ushindani
Good!
 
Alikuwa akipendwa tu tu yaani nyota yake ilikuwa kali. Huyu Membe huyu atakuja na ushawishi pamoja na kupendwa kidogo. Ila inakusudiwa atachofanya ndiyo kitaupandisha upinzani.
Membe huyuhuyu au mwingine? unafikiri CCM ni wajinga kumvua uanachama? hana impact yoyote kabisa kwa CCM ndiyo maana wakamvua uanachama. Wapinzani wakimuchukua Membe basi watakuwa wamesaidia wenyewe kuufuta upinzani afadhali waendelee na wagombea wao akina Lissu,Mbowe na Zitto.
 
Yaani umebugi kusema lowasa hakuwa na mvuto.Mkuu haijawahi tokea Tanzania mgombea mwenye mvuto kama lowasa.Mi nadhani labda mvuto kwako mkuu ni ule wa mapenzi tu.
 
Swala la CCM kutawala milele halipo na CCM haina muda mrefu itaondoka madarakani kwani vikwazo kama tume huru/katiba mpya vitapatikana ndani ya miaka isiyozidi kumia kuanzia sasa hata kwa kutumia mbinu za kulazimisha CCM wakubali hili.
Duh...!. Haya!.
P
 
Back
Top Bottom