Upinzani utakuwa na pande mbili zilizo rasmi, ambazo ni “Radical” pamoja na “Moderate” wings!

Tuonyeshe woga wake umeuona kwenye nini? Ni hatari sana (kama sio ujinga) kujadili jambo lililopita uwezo wako wa ufahamu. Haina tofauti na mtu asiye na elimu yeyote ya dini kujadili na kubishana juu ya maandiko matakatifu.
..woga wa Kwanza kupiga magoti kuomba maridhiano wakati wenzako wanaongoza mitaa na vijiji nchi nzima woga wa pili kuomba maliziano baada ya kuona maji yamezidi unga kisutu!..ikumbukwe lisu kapigwa lisasi mchana kweupe lakini hakuna ata mtuhumiwa aliekamatwa kavuliwa ubunge kibabe wakisema hawajui aliko alafu bado mwenyekiti anaenda kuomba maridhiano kisa aponyeshe Jimbo lake!!! Usiwe mpumbavu wa kusifia kila kitu mbowe kakosea kabisa huo ndio ukweli
 
Kwa maoni yangu, upinzani sasa utakuwa na sera ya “carrot and stick”.

Kwenye siasa, mambo hubadilika. Hata Maghufuli jana alikiri hilo pale alipokuwa akizungumzia kuhusu misamaha kwa wale waliokuwa wanashitakiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi. Alisema kabisa “nyakati hubadilika”, na “kila mwaka una mambo yake”

Zitto alikuwa kwenye nafasi ya tofauti kwenye nyakati unazozitolea reference.

Ninapozungumzia upinzani, Nina wajumlisha wote Zitto na Mbowe kama watu wenye lengo moja lakini tofauti iko kwenye namna ya kudeal na ukandamizaji wa kidemokrasia unaozungumziwa.
 
jmushi1,
Zitto anamjua vizuri sana Mbowe....... Hawa ni marafiki wa muda mrefu.

Maridhiano anayoyataka Mbowe yana maswali mengi kuliko majibu na hasa unapowataja Tundu Antipas Lisu na Joshua Nassari!
Nassari kahusika vipi?
 
Zitto kisiasa hawezi kuwa radical na wala hajawahi na hataweza hata siku moja. Zitto ni mbinafsi anayetaka credit zimwangue yeye kwanza kabla hazijawaendea wengine. Kwa Tundu Lissu naweza kukubali lakini siyo Zitto.
Lakini hizo pande mbili tayari zimeshaanza kuji “demonstrate” ama kujipambanua.
 
jmushi1 ,

..inabidi kupata maelezo toka kwa Mbowe kwamba maridhiano anayoyataka yanahusisha nini.

..what if yanahusisha mambo kadhaa ikiwemo wote walioumizwa kupata HAKI yao?

..pia rejea interview ya TL aliyoifanya akiwa Nairobi hivi karibuni. TL amebainisha kwamba tatizo siyo maridhiano / mazungumzo bali mnaridhiano kuhusu nini na mnaridhiana na nani.
 
Mimi niwe wazi sijaridhishwa na Mbowe au hiyo inayosemwa ni maamuzi ya kamati kuu. Kwa mtazamo wangu Magufuli sio mtu wa maridhiano bali ni mtu anayetaka kunyenyekewa. Ifahamike Magufuli ana msimamo wake tofauti na wengi humo ccm, kutokana na madaraka yake makubwa hakuna wa kumdhibiti kwenye utashi wake huko ccm. Magufuli ameonyesha wazi hataki upinzani na hasa chama asichokipenda ni cdm na hatakaa akipende, na hilo liko wazi, labda kitii atakacho na sio maridhiano.

Kwahiyo alichokifanya Mbowe ni kutaka maridhiano lakini kwa njia ya kushitaki kwa umma, lakini sioni Magufuli akiwa na mahesabu hayo, kwani hana muda wala uvumilivu wa siasa za ushindani. Sana sana uhudhuriaji wa cdm kwenye ile hafla, ni kama umeenda kufukia madai yao yote halali ya cdm dhidi ya uonevu wanaofanyiwa. Katika mbinu waliyochemsha cdm ni hiyo ya kutaka maridhiano na mtu anayewafanyia atakavyo bila wao kufanya lolote. Maridhiano huombwa hasa na anayekandamiza baada ya misuguano isiyoisha dhidi ya wale anaowakandamiza, na sio kinyume chake. Pale cdm walienda kutafuta huruma ya Magufuli na sio maridhiano.
 
Mbowe kachukua approach ya Raila Amolo.
 
Kuna watu maridhiano hawataki kuyasikia kwa sababu yataondosha ulaji wao

Haya makundi nufaika yako serikalini na kwenye vyama.

Kuna vitengo vinavyoratibu mauaji kuteka , kutesa, kuzuia harakati za wapinzani, ikitokea maridbiano yakawepo watapoteza uhalali na kazi yao pia vivyo hivyo upande wa opposition.

Sasa wasiojulikana watakula wapi ikiwa maridhiano yatafanyika
 
Tuache yote, ile kamati kuu ya chadema iliyoamua kushiriki uamuzi wa kwenda kushiriki sherehe za Uhuru imefanya jambo La maana sana.
 
Kwani mbowe alijipeleka mwenyewe? Hata lissu alisema wako tayari muda wowote kukutana Na serikali.upinzani sio vita.siasa za uhasama hatuzitaki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…