Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 98,439
- 145,410
Unaelewa tofauti ya Lissu na "Kina Lissu" ?
Maridhiano anayataka na nani? Na serikali inayoongozwa na gubegube Magufuli?
Mbowe made himself Magufuli's bitch right now.
Mbowe kasema, direct quote.
"”Rais una nafasi ya kipekee kuweka historia ya maridhiano katika taifa letu kwani kuna wengine wanalalamika wanaumia. Rais tumia nafasi hii ukaliweke taifa katika hali ya utengamano,” amesema Mbowe.
Hakumuomba rais maridhiano hapo?
Mbowe anajua kwamba watawala hawa concede power kwa kuombwa, bali kwa mapambano?
Anategemea kumuomba Magufuli maridhiano halafu Magufuli aone huruma?
Ndiyo matarajio ya Mbowe?
Magufuli akimpuuza atafanya nini?
Kwanza maridhiano [reconciliation] ya nini? Hatujafikia hali ya kuwa na maridhiano sisi.
Mwaka 2005 Liberia waliunda tume ya Ukweli na Maridhiano. Sababu za kuunda tume hiyo ni dhahiri.
Afrika Kusini nao walikuwa na tume kama hiyo baada ya Apartheid.
Majuzi tu hapa huko Msumbiji, Frelimo na Renamo wamesaini makubaliano ya amani na maridhiano ya kitaifa. Sababu zinaeleweka kabisa.
Rwanda nao baada ya mauaji ya kimbari walifanya hivyo hivyo.
Kenya baada ya uchaguzi wa 2007 ilibidi waunde tume ya maridhiano.
Sisi hatujafikia hata fraction ya walichokipitia Wakenya mwaka 2007 halafu kuna watu wanataka maridhiano!
Tuseme hao wapinzani wanafanya maridhiano na CCM. Nini kinachofuata sasa?
Wataiunga mkono CCM kwenye uchaguzi wa mwakani?
Mazingira yetu bado hayajalazimu kuwepo na maridhiano nchini, at least kwa Tanzania bara.