Upotofu, ulaghai na uchafu ndani ya kanisa kiini chake kikubwa ni viongozi wa dini kukwepa haya hizi mbili ndani ya Biblia

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Hallelujah!
Mimi ni mkristo, siandiki hapa kwa lengo la kuufedhehesha Ukristo hapana.
Natamani turudi kwenye Ukristo ule ambao sifa tu inatosha kuleta uponyaji wa kimwili na kuleta bubujiko la kiroho tofauti na sasa sifa ipo tu kama desturi.

Mtu ametoka kuzini jana leo anashika mike kuongoza ibada na wala hakutani na mkono wa Mungu.
Kanisa linabidi liwe 🔥, kiasi kwamba mtu hata kama alifanya dhambi Dar es salaam akifika kanisa la Mbeya hawezi kujificha kwa namna yoyote.

Kiini cha ulaghai ni nini?

Kiini cha ulaghai kilitokea pale viongozi wa makanisa kuanza kuficha sehemu ya changizo (sadaka), tabia ikakomaa baadaye kanisa likahalalisha kuwa sadaka ni Mali ya kiongozi, kwamba yeye ana mamlaka juu ya sadaka zote.

Tabia ikakomaa zaidi wengine wakaanza kutafuta pesa na mali mifukoni kwa waumini.
Kanisa la mitume waliishi hivi 👇👇

Matendo ya Mitume 2:44-45
Screenshot_20241013-195218.jpg

Leo mchungaji atatoa fedha za matibabu kwa muumini wa karibu sana na hata hivyo atahesabu yeye ndiye katoa fedha.

Atasimulia kila mahali kuwa anasaidia watu wenye shiida huku fedha ni sadaka za waumini. Kama muumini hujulikani utakufa kisa umekosa elfu 40 tu ya matibabu huku account ya sadaka ambayo mchungaji anaiita account yake ina milioni 300 .

Mungu hadhihakiwi, hawa walanguzi wa kiimani wote makazi yao ni kwenye ziwa la moto.
 
Hallelujah!
Mimi ni mkristo, siandiki hapa kwa lengo la kuufedhehesha Ukristo hapana.
Natamani turudi kwenye Ukristo ule ambao sifa tu inatosha kuleta uponyaji wa kimwili na kuleta bubujiko la kiroho tofauti na sasa sifa ipo tu kama desturi.
Mtu ametoka kuzini jana leo anashika mike kuongoza ibada na wala hakutani na mkono wa Mungu.
Kanisa linabidi liwe 🔥, kiasi kwamba mtu hata kama alifanya dhambi Dar es salaam akifika kanisa la Mbeya hawezi kujificha kwa namna yoyote.
Kiini cha ulaghai ni nini?
Kiini cha ulaghai kilitokea pale viongozi wa makanisa kuanza kuficha sehemu ya changizo (sadaka), tabia ikakomaa baadaye kanisa likahalalisha kuwa sadaka ni Mali ya kiongozi, kwamba yeye ana mamlaka juu ya sadaka zote.
Tabia ikakomaa zaidi wengine wakaanza kutafuta pesa na mali mifukoni kwa waumini.
Kanisa la mitume waliishi hivi 👇👇
Matendo ya Mitume 2:44-45
View attachment 3124086
Leo mchungaji atatoa fedha za matibabu kwa muumini wa karibu sana na hata hivyo atahesabu yeye ndiye katoa fedha.
Atasimulia kila mahali kuwa anasaidia watu wenye shiida huku fedha ni sadaka za waumini. Kama muumini hujulikani utakufa kisa umekosa elfu 40 tu ya matibabu huku account ya sadaka ambayo mchungaji anaiita account yake ina milioni mia 3 .
Mungu hadhihakiwi, hawa walanguzi wa kiimani wote makazi yao ni kwenye ziwa la moto.

Mungu ni wa Neema sana.wala si mwanadamu.kama akifanya kama unavyofikiri unadhani wewe binafsi utapona?
 
Wenyewe wanaliita hilo lilikuwa kanisa la mwanzo

Uko sahihi mleta mambo mengi kama kanisa tumeyaacha na kudandia mapya ambayo hayafai kabisa
 
Mungu ni wa Neema sana.wala si mwanadamu.kama akifanya kama unavyofikiri unadhani wewe binafsi utapona?
Kwahiyo kwenye issue ya Anania na Safira Mtume Petro alifanya kosa?
Mungu wa neema.
Mungu wa neema ndio maana anawaacha ili watubu si kuendelea kujilimbikizia mali.
 
Yaani angefanya kama unavyotaka dunia ingekuwa haina watu.hapo unaposema ni kanisani inaweza ikawa alishapakataa wala hapo siyo pake wala hapo hayupo kabisa wapo hao wanzizi peke yao
 
Fungua akili yako hakuna kanisa..hakuna yesuu..hakuna dini......fungua akili yako!
 
Mmelazimishwa kwenda kwenye hayo makanisa ama ni nyie wenyewe mnaendaga?

Tukiwaambia dini ni utapeli huwa hamuelewagi.
 
Back
Top Bottom