View attachment 3519938
My people,
Kumekuwa na uelewa mbaya au upotoshaji wa makusudi kuonyesha jamii kwamba sisi watetezi wa amani, tunafurahia Mauji yaliyotokea 29 Oct 25
Guys hivi kweli hata kwa akili tu ya kawaida mnawezaje kuwatuhumu watu jambo kama hili? Hivi mnaamini kwamba tumekosa utu kiasi hiki?
Hapana mnatukosea sana,hata kama mmekosa hoja baada ya kuwapiga spana za kutosha lakini hiyo ni tuhuma mbaya sana,hawa ni ndugu zetu na watanzania wenzetu hatuwezi katu kufikia hiyo stage
Hata pale tunapo sema kwamba ilikuwa move mbaya in the first place kuandamana bado haimaanishi kwamba tunafurahia yale yalitokea
Pili, tunatagiwa kwa hoja za kipuuzi sana, kwani ni nani amesema tunakataa umwagaji damu wa maelfu ya watu,nani amekataa kuwa Serikali ilitumia nguvu kubwa kuwadhibiti waandamanaji?
Maana jinsi mnavyoandika mabandiko yenu kana kwamba mnatu tuhumu kuwa tumepinga au kukataa kwa mambo hayo kutokea,hayo yametokea na wote tunafahamu,kwahiyo muache kutupa tuhuma zisizo na msingi
Tatu,kuna uwongo ambao unasemwa semwa sana na mwisho wa siku unaaminika kwamba ni kweli, si kila mtu ambaye yupo upande tofauti na nyinyi au ana mtazamo tofauti na nyinyi basi atakuwa amekuwa amelipwa hela.
Huu ujinga umeshika kasi sana,wakati mwingine tunaitikia tu kwakuwa ndivyo mnavyoamini hivyo, hiyo serikali ina pesa kiasi gani ya kumlipa kila mtu? Je kuna usalama kiasi gani wa kuonana na mtu au kuwasiliana nae au kumpa namba yako ya simu akuingizie hela.
Jiulize we binafsi hivi kwa mazingira haya unaweza tu kushirikiana na mtu kupush ajenda yake bila kumjua ana malengo gani,je kama ni watu wasiojulikana unaweza tu kuongea nae akakuahidi kukupa hela kuisapoti Ccm au Serikali?
Jibu ni hapana,sasa inakuwaje kila mtu anayetofautiana na nyinyi kifikra basi awe amelipwa na CCM au Serikali?
Ebu tumieni akili hata hizo za kuvukia barabara,kuna wengine wanazo kama hizo na zinawasaidi kureason baadhi ya mambo fulani fulani katika maisha yao ya kila siku
Mwisho kama kila anayesapoti amani na utulivu wa nchi hii ni chawa basi mimi nitakuwa The big Chawa and am Okey with that, do you have a problem with that?
Ni hayo tu!