Upotoshaji wa makusudi dhidi ya wale wanaoitwa machawa kwa kuwa tu wanatofautiana nanyi kifikra

Kwa hivyo majambazi yakivamia nyumba ukauke tu mke wako abakwe ,pamoja na watoto kwa kigezo Cha kulinda amani?
 
Ndugu zako hawakuuliwa oct29 ndo maana huna uchungu na neno ulisemalo
 
Mange aliyewaingiza mkenge aliondoka Tanzania miaka zaidi ya 20 iliyopita, hajui lolote kuhusiana na ukweli kwamba JWTZ wanakula kiapo cha utii kwa Rais kwa mujibu wa katiba.

General Mkunda asimsikilize Rais anayeidhinisha malipo ya mshahara wake ambao unaweza kuzidi tshs milioni 25 kwa mwezi aje amsikilize dada mmoja mchochezi wa kule California.

Ule ujinga wa October 29 ulifeli mapema sana.
 
.....binafsi nasema aliyekosa akamatwe kwa mujibu wa sheria, apelekwe mahakamani kosa lidhibitishwe awajibike.
Wewe unasema, aliyekosea atekwe ateswe, auliwe mwili wake utupwe porini, na atakaye hoji atendwe vivyo hivyo.....

Huo ndo utofauti wetu.
 
Nianze na hoja yako ya hapo mwisho ambayo kidogo imenishtua, ingawa nina uhuru wa kulike chochote na kudislike chochote.

Are sure ni mimi nimefanya hivyo? Unaweza kuscreen shot baadhi tu ya sehemu sehemu.

Tuje kwenye hoja yako ya kwanza,kuhusu polisi kutumia nguvu kupita kiasi, je kabla ya tukio la vurugu na fujo,nasema hivi kwasababu yale hayakuwa maandamano

Je , serikali ilishawahi hapo kabla kuwapiga watu risasi tu bila sababu?

Jibu hapana, ila baada ya matukio ya fujo na vurugu ndio Serikali ikatumia ambayo ilipita kiasi na kuleta yale mauji

Je,hapo utasema Amani hakuna wakati ilitumika nguvu kwa sababu maalumu ya kuwadhibiti watu waliokuwa wanahatarisha amani ya nchi?
 
Kwa hivyo majambazi yakivamia nyumba ukauke tu mke wako abakwe ,pamoja na watoto kwa kigezo Cha kulinda amani?
Huo mfano haufanani na nguvu ya dola,huyo jambazi unaishi naye fresh tu mpaka ajute kwanini alikuja maskani kwako
 
fact
 
Hakuna utofauti kati ya chawa na wasichawa au wasochawa. Sisi wote ni walewale tu. Mlengo wa kimtazamo au nitumie neno "point of focus" ndiyo inayotuonesha kama kuna utofauti.

Unajikita kwenye kutazama nini hasa ndipo panapoleta mgawanyo wa uchawa au usochawa. Nadhani tunapaswa kuihakiki kiyakinifu mitazamo yetu juu ya masuala mbalimbali. Mitazamo hii hutugawa sana na ikitumika vibaya tunagawanyika katika mawanda yote ya kimaisha.

Dedication: "One love, one heart....let us stand together things will be malizia"
 
fact
 
Chawa ni kamdudu kanakokaa sehemu chafu ili kapate ulaji, kama unatetea uchafu wowote ule wewe ni CHAWA! ​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…