Gwappo Mwakatobe
JF-Expert Member
- Nov 22, 2019
- 1,730
- 2,230
Ushauri mwanana kabisa!
Mimi nilsikiliza mahojiano ya wote wawili Prof. Lumumba na Lissu wakihojiwa na Chaka Ssali; kila mmoja wao alijibu maswali waliyoulizwa kwa ufanisi kama walivyoweza na wote walikuwa watulivu na makini.Tundu ana jambo muhimu la kujifunza toka kwa Prof. Lumumba kama anataka kuondoka kwenye kuwa activist na kuwa mwanasiasa wa kuheshimika na watanzania na sio watu wa nje ya Tanzania.
Tanzania kama nchi ina mila na desturi ambazo wanasiasa lazima kuziheshimu kwani watu wanaowaongoza wanazihesimu mila na desturi hizo. Magufuli ametangulia Mbele ya haki hivyo sio vizuri kutumia lugha ya matusi dhidi yake sio ustaarabu. Marehemu alikuwa na wafuasi wengi sana kama ilivyodhihilika wakati wa msiba wake na hao hao ndio wapiga kura ambao Tundu Lissu atajaribu kuwatongoza kuwa waje kuwa wafuasi wa chama anachokiongoza!! Lakini anapomtukana na kutumia lugha isiyo ya kistaarabu dhidi ya hayati kipenzi chao anazidi kuweka uzio ambao utamzuia kuwashawishi hawa kuwa yeye Tundu Lissu ni kiongozi bora kuliko hayati mpendwa wao na hivyo kuwakosa wafuasi hao. Mwanasiasa mzoefu asingefanya hivyo. Hilo ni somo moja ambalo Prof. Lumumba alimsihi Tundu Lissu ajifunze!!!