Upweke umewaanza vijana mapema, Uzeeni sijui itakuwaje. Ni janga kubwa

Ndoa zilikuwa zamani
Sasa Ni Utapeli , Ni Ujambazi na ni Wizi mtupu
Wacha wajinga wapigwe
Nashukuru walau ndani mwako umeadmitt na uko concious kuhusu umuhimu wa ndoa katika jamii. Kwa kusema ndoa zilikuwa zamani, ina maana ni jambo unajua umuhimu wake, ila kitu pekee kimekuvunja moyo ni mienendo ya jamii ya sasa ndani ya ndoa.

Hili linachangiwa na mambo mengi kwenye jamii yetu, utandawazi na "ubusy" wa maisha katika kutafuta fedha, tunajikuta tunasahau wajibu wetu wa msingi katika makuzi pia.

Kama jinsi unavyoumia wewe na kuona ndoa ni utapeli, wako wanawake ambao nao waliwekeza muda na mali kwa wale waliowapenda, lakini mwisho wakaangukia pua.

Hivyo ni suala la unampata mtu sahihi katika maisha yako ili muweze kujenga familia?
 
Ni kweli ila kwenye suala la mwanaume kuwahi kufa haihusiani na upweke kwa namna nyingi.

Mkuu jitathmini, mada zako zinapoteza ubora siku hadi hadi siku, jitahidi kufanya tafiti zaidi, kuna uzi uliandika hata tafiti hukufanya kabisa na ulikiri hilo kwenye kureply comments za wadau.

Upweke ni tatizo kubwa kwa sasa, single maza wengi hawana wenza, wanajitegemea. Wanaume wanaogopa kuoa singo manza, matokeo yake huyu anaishi kipweke kule na huyu anaishi kipweke huku.

Wanawake wanajua njia za kusaka pesa, wanajipangishia wanalipa bills ila ahueni ya upweke haipo, anahisi hahitaji mwanaume ila deepdown anahitaji sana.
Mwanaume anaondoa upwiru wa siku moja ila upweke hauondoki, anatoa nyege tu ila sonona haisepi kindezi, kila siku anaona hali ngumu, imagine mtu siku 2 hajacheka hata mara moja, hajafurahi hata mara moja, sonona haimuondoki mtu huyu.

Kingine ni aina ya kazi zetu, kuna kazi ambazo ni 'kamati ya roho mbaya" yaani ili uendelee kua na hiyo kazi basi yakupasa uwe bandidu, uso wa mbuzi, usicheke na kima, ukauzu zaidi ya dagaaa. Hizo kazi huwezi pata faraja wala ahueni kihisia.
 
Kijana wa 28 zamani yuko nyumbani ila sahivi ana miaka 5 mitaani
 
Kingine ni aina ya kazi zetu, kuna kazi ambazo ni 'kamati ya roho mbaya" yaani ili uendelee kua na hiyo kazi basi yakupasa uwe bandidu, uso wa mbuzi, usicheke na kima, ukauzu zaidi ya dagaaa. Hizo kazi huwezi pata faraja wala ahueni kihisia.



Mfano....
 
Ni nyingi ila baadhi ni..
Mgambo wa jiji
Viwandani, huku ndo kuna kamati za roho mbaya..
 
Upweke ni mbaya sana, binafsi naamini kabisa 99.99999% ya CHAPUTA ni wapweke..... 😀😃
 
Nimesema kazi ndio tiba ya upweke

Habari ya upendo, furaha na kuishi sijazungumzia ndugu
Nakubaliana nawewe nikiwa kama shuhuda kazi ni dawa nilipitia hii situation kazi pekee ndiyo iliniokoa sana sana nikirudi ghetto nipo hoi nafikia kulala nikishtuka kumekucha.
 

Upweke unaua mkuu. Hiyo ipo kisayansi na kitaalamu
 
Kuna watu wamezungukwa na watu ila bado ni wapweke vile vile
 
mzee shikamoo...

wewe si umeishi kwenye ndoa muda mrefu,

inaondoa upweke kweli?
marahaba kijana wangu
sitaki kusema mojakwamoja kwamba ndoa huondoa upweke lahasha ila ila ni moja ya tiba pia
mimi ni muumini wa kuondoa upweke kwa kufanya shuhuli kama sivyo huwa na desturi ya kutembea kwa mguu kama kilometa 7 narudi nyumbani na kujipumzisha
 
Hii mada nimeisoma kwa makini nikaishia tu kusema i wish....Huwezh tena mtu kurudisha nyuma wakati. Ila pia childhood trauma inapelekea hali ya upweke baadaye utu uzimani.
 
Mimi najitolea mfano katika hili. Muda mwingine inalazimu kukesha humu jf at least kupiga gumzo na watu tusiojuana ili tu ku cover ile gap ya loneliness.
 
Kuna watu wamezungukwa na watu ila bado ni wapweke vile vile

Upendo ndio huondoa upweke.
Unaweza ukawa na mke au mume hamkai karibu labda kutokana na kazi lakini kutokana na kukujali na kukufuatilia ukajiona upo karibu naye
 
Vijana wengi ni bomu la kesho.
Mlonwake kwa siku ni wankubanaisha na energy na half cake! Leo umwambie awe na mke.
Wanawake hawahawa baada ya siku chache huna mshiko unapigwa vita hadi uende.

Mauaji mengine tuyasikiayo ni kwa sababu ya mashida zinaoibuliwa na wanafamilia au wanandoa shida kubwa pesa!!. Mwanaume unategemewa kila kitu na si ajabu kama wazazi wako Hai nao ni kwako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…