Upweke umewaanza vijana mapema, Uzeeni sijui itakuwaje. Ni janga kubwa

Upweke umewaanza vijana mapema, Uzeeni sijui itakuwaje. Ni janga kubwa

sema Upendo Feki
anaangalia kimya kimya una asset gani ndiyo akupende
anauliza unafanya kazi gani ? ili iweje hasa ?
maswali ya kipuuzi sana

😃
Ndio maana kiislamu ínashauriwa utafute mwenza ukiwa apeche Alolo kama mpango wako ni kuishi na mwanamke
 
Mtume Muhammad alisema kuwa kijana anayeweza kusapoti mke basi aoe!

Haya mambo ya kusubirisubiri sana ndiyo mwanzo wa kuingia ktk ulevi wa kupindukia, utumiaji madawa ya kulevya ili kutafuta furaha.

Ndoa inakupa sense ya juu ya uwajibikaji

Muhamad akaongeza, kama mtu anatafuta mke ni vizuri akatafuta akiwa apeche Alolo
 
Inafikirisha

Hata ukiwa na hivyo vitu uwezekano wa kupitia upweke bado upo

In life, nothing is guaranteed.
 
Binafsi yangu sidhan kama upweke unaweza kuniathiri kwa namna yoyote ile. Nafikiri ni kwasababu nilivyoyafanya tu maisha yangu yawe. Ila huu uzi umenifanya niwafkirie watoto wangu na mama yao kwamba kumbe nina wajibu wa kuwafanya wasijihis upweke licha ya harakat zangu. Na hik ni kitu nafikir wengi huwa hatukiwaz kwa undani huu ndio maana huu uzi umenigusa sana
 
Binafsi yangu sidhan kama upweke unaweza kuniathiri kwa namna yoyote ile. Nafikiri ni kwasababu nilivyoyafanya tu maisha yangu yawe. Ila huu uzi umenifanya niwafkirie watoto wangu na mama yao kwamba kumbe nina wajibu wa kuwafanya wasijihis upweke licha ya harakat zangu. Na hik ni kitu nafikir wengi huwa hatukiwaz kwa undani huu ndio maana huu uzi umenigusa sana

Ukikosa familia au familia ikikuzingua hakika upweke utauona vaapu!
 
UPWEKE UMEWAANZA VIJANA MAPEMA, UZEENI SIJUI ITAKUWAJE. NI JANGA KUBWA.

Anàandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Huwezi sema unafurahia maisha ukiwa pekeako. Mtu mpweke hawezi kuwa na furaha. Mpweke ni tafsiri halisi ya maiti inayoishi.

Utoto ni raha kwa sababu utoto unahusisha ushirikiano wa mtoto na watoto wenzake. Mtoto na wazazi. Mtoto na michezo. Ndio maana mtoto katika umri wa utoto Unaowajibu wa kumfanya ashirikiane na watoto wengine. Na sio uanze kumfungia ndani kama mfungwa.

Upweke ndio hufanya kijana au binti aoe. Mapenzi ni moja ya tiba ya upweke. Ukiwa na mtu mnayependana na kuelewana automatically upweke utakuwa umedhibitiwa.

Njia nyingine ya kudhibiti upweke ni kujihusisha na vikundi vya kijamii, kidini pamoja na michezo. Lakini hivi ni wakati ukiwa nje ya nyumba yako. Nyumbani ukirudi kama huna mpenzi iwe mke au mume ambaye mnapendana. Utaiona siku ni ndefu na mara nyingi utayaona maisha hayana maana.

Vijana wa sasa wapo vile uwaonavyo, ni kama hawana utulivu, wamechanganyikiwa, wengi wao ni kwa sababu ya Upweke. Upweke unaleta Sonona kama sio Depression. Upweke ni chanzo cha Kifo.

Mabinti wengi ninaowasiliana nao na ambao wanapata huduma kwangu wanakabiliwa na changamoto ya upweke. Wanaishi wenyewé. Wengi wao ni kati ya miaka 22-40. Unakuta Mwanamke amepanga chumba au nyumba anaishi mwenyewe au na watoto, hana mume.

Pia vijana nao wengi wenye umri huo wapo single. Na wanaishi vikundi vikundi kwenye Maghetto yao. Licha ya kuishi vijana kuanzia wawili lakini bado upweke unawasumbua. Hii ni kwa sababu. Wao sio familia moja.
Familia ni Mume, mke na watoto.

Kuanguka kwa taasisi ya ndoa kumeongeza Upweke ndani ya jamii. Na hii itachukuliwa kama fursa kwa wamiliki wa mitandao ya kijamii kwani Watu wengi hutumia mitandao kama sehemu ya kudhibiti upweke.

Upweke ubaya wake upo siku za Weekend kwa wale wanaofanya kazi. Lakini pia upweke huonekana Dhahiri nyakati za usiku Watu wanaporudi kupumzika majumbani kwao.
Wapo Watu ambao usiku kwao hauna faida.

Sababu nyingine kubwa ya wanaume kufa mapema zaidi ni hiihii, UPWEKE. Mtu mpweke hulazimika kufa mapema kutokana na matatizo kama ya msongo wa mawazo.
Wanawake kwa upande wao muda mwingi huweza kuutumia na watoto waliowazaa kuwalea kama kuwabembeleza, kuwaogesha, kuwalisha chakula, kupishana nao kelele, kucheza nao.
Lakini vipi kwa mwanaume?
Mwanaume zaidi ya kwenda Bar kutuliza nafsi na kuondoa upweke ambao kimsingi hauondoki hana pengine pamoja kukimbilia.

Jambo moja lazima ulielewe, Taikon kama Mastermind ninakuambia Upweke huwezi uondoa na Watu Baki. UPWEKE unaondolewa na Watu unaowapenda na unaostahili kuwapenda. Upweke unahusu Moyo. Hisia za UPENDO.
Mke au Mume ndio mtu wa kwanza kuondoa upweke wako.
Kisha Watoto wako.
Alafu Wazazi wako.
Ndipo ndugu na marafiki.

Niliwahi kufanya uchunguzi wa kuona ni namna gani mtu Baki anaweza kukuondolea upweke nikagundua kuwa ni ngumu sana. Ni kwa sababu akili italazimisha moyo u-pretend kuwa haupo pweke.

Kama utaenda Kasino ukachukua Kahaba hata wawili au watatu kwaajili ya kukuondolea upweke, utagundua ya kuwa hawawezi kufanya jambo hilo kwa sababu wao wapo kwaajili ya kujifurahisha kimwili na sio kinafsi(Moyo).

Mtu aliyempweke huweza kufanya lolote la hatari. Upweke huathiri mtu kisaikolojia na huweza msababishia mtu kukosa UTU.

Mtu akikosa anayemjali na wanaomjali moyo wa kujali wengine huanza kufa polepole. Na kama utakufa kabisa utu huondoka nafsini mwake.

Ushauri kwa vijana,
Wapende na kaa karibu na Wazazi wako. Husaidia kuondoa upweke.
Tafuta familia, mke au mume, naye huondoa upweke.
Kuwa na watoto kisha fanya wajibu wako kama mzazi kwa hao watoto.
Kukosa familia ni kukosa maana halisi ya maisha.

Acha Nipumzike sasa

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Loneliness is a state of mind. Unaweza ukawa karibu na makundi ya watu uliowataja kwenye hili andiko na bado ukawa mpweke. Hakuna factor moja inayopelekea hali ya upweke.
Upweke unaweza kusababishwa kuhisi kutopendwa "feeling unwanted" au kutokubalika "feeling unappreciated". Kuna njia nyingi za kuondokana na upweke na hutofautiana kati ya mtu na mtu au kundi moja na jingine na si lazima mapenzi au mahusiano.
 
Ukikosa familia au familia ikikuzingua hakika upweke utauona vaapu!
Nakubali, sema ujue nini Taikuni, kuna time huwa napenda kuishi kwa kujihami kwa upweke nikiwa kama mwanaume, maana si unajua hawa watoto wetu huwa wanatutenga sisi baba zao na kuhamishia majeshi kwa mama zao pale tunapokua watu wazima sana, unajikuta baba upo lakin ni kama huonekani licha ya kutimiza wajibu wako kwao kipindi ukiwalea. Hiz kesi zipo nyingi sana
 
Upendo unaanzia ndani.

Si Rahisi kuondoa upweke Kwa Kuoa na kuwa na familia karibu pekee,

Si Rahisi kumpenda mke au mtoto ikiwa huna Amani ya moyo iletwayo na Upendo wa Mungu kupitia Yesu Kristo.

Upendo ni kuwa na YESU maishani, ni kujazwa Roho mtakatifu aliye pendo kuu,

Ukiwa na Upendo wa Mungu ndani Yako, Upendo huo utaambukiza mke, mume na wengine Walio karibu na mbali.

Let Love of God through Jesus Christ lead the way.

Amen
 
Zingatia hapo kwenye bold kubwa.

Duniani hakuna ambaye ktk malengo yake alitegemea kupigwa au kujipiga,wewe unaenda kujipiga nakwambia hakuna awezae kushindana na natural ndiyo maana wewe ulitokana na wazazi walioishi pamoja wewe nani leo uwaone hawana akili?
Akubali tu anapata ngono Ila anakosa uwezo wa kumtunza mke.

Natural inkutaka uoe ujenge familia
 
Upweke ni ugonjwa,

Upweke unapelekea utendaji wa mtu kuwa chini
Upweke unasababisha vifo vya kujitakia

Upweke unapekelekea uasi kwenye jamii
 
tamthilia zinakuharibu

Ibu yule pale, yuko hoi kitandani mke chap kambambikizia kesi, kaondoa na savings zake zote

Davis Mosha, yule pale, mke linamuibia kimya kimya, kuja kusanuka, too late
bado linataka nusu ya mali, pumbav kabisa

jidanganye tu, endeleeni kufuga majambazi
ni swala la mda kabla vilio kusikika
tatizo kwanye kuoa mnaangalia shepu nk na mwisho mnaoa wadangaji na sio wanawake wa ndoa, wanasema kosea vyote usikosee kuoa mana unae muoa ndie anaebeba asilimia za maisha yako unaoa mke toka mwanzo wa penz anakuonesha ana uhitaji wa mali na sio ndoa, ni rahisi maskin kupata mke sahihi ila sio tajiri na mke ukioa pindi una kipato au kipawa flan kumbuka utapendewa hivyo vitu na siku huyo mtu akivimbiwa na kusaza au wewe kuishiwa bas haya unayosema lazima yatokee
 
Kwa kuwa hatuna takwimu za uhakika kama wenzetu, ni vigumu kujua wangapi wamewehuka au wangapi wana depression na idadi ya waliojitoa roho kabisa
Hawa wa kataa ndoa wamo kwenye kundi la mfadhaiko
Na wanaoona simu ndio rafiki wapo kwenye Dunia tofauti
Vijana chapeni kazi
 
Back
Top Bottom