Kuukana uraia wa Tanzania si dhambi - Serikali
2007-01-29 17:46:06
Na Emmanuel Lengwa, Jijini
Serikali imeanza mchakato wa kuwaruhusu Watanzania walioukana Utanzania wao kuwa na uraia wa nchi mbili.
Akihojiwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza, BBC, hivi karibuni, Waziri wa Mambo ya Nje, Bw. Benard Membe, amesema serikali imeona upo umuhimu wa kutunga sheria itakayowaruhusu wananchi hao kuwa na uraia wa nchi mbili ili waweze kushiriki kuleta maendeleo nyumbani.
``Tayari Rais Jakaya Kikwete ameagiza tuanze mchakato wa kuwapatia wananchi wetu uraia wa nchi mbili... tumegundua kuwa tukifanya hivyo wenzetu hao wanaweza kusaidia sana kuleta maendeleo nchini,`` akasema Bw. Membe.
source; https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/1504-uraia-wa-nchi-mbili.html
Hoja ya uraia wa nchi mbili inazugwa tu na unaonekana waziwazi kuwa ni wizi mtupu! Hoja ya Nyerere kuhusu swala hili ilikuwa nzito na haikuweza kupingwa na manabii wa uraia wa nchi mbili wa wakati ule. Hawa wa sasa hawaanzi kwa kuitengua hoja ile na badala yake wanaleta sababu za urahisi wa kuwekeza bila kutueleza nani atafaidika na uwekezaji huo!Shukrani Mwanakijiji,
Its a good reminder.
Ni juzi juzi, tu wakati kombe la dunia likiendelea, tulialikana familia za Kitanzania kuangalia kwa pamoja mechi kati ya Ghana na USA. Well, nilichoshuhudia, ikabidi nijiulize mara mbili mbili kuhusu hii Dual Citizenship watu tunayoipigania.
Anyway, ni vyema watu kusoma hiyo reminder uliyoipost.
Usawa huu kama uko katika position ya kuchukua ganda la watu chukua tu, hapo kipawa minazi mirefu utarudi tu hata bila ganda kama unataka.
Ukisubiri subiri hao jamaa wa bongo watazuga (I don't believe watapitisha) na huku viwanja unaweza kukuta milango imefungwa.
Mimi nataka world citizenship, nilipozaliwa hawakuniuliza nataka uraia wa nchi gani, kwa nini nibambikwe uraia kwa sababu nimezaliwa nchi moja, nikisema nimezaliwa duniani je?
Sheeeesh!
Tough new points system for earning citizenship
03 August 2009
Plans requiring would-be-citizens to earn enough points to stay permanently in the United Kingdom were revealed by the Government today.
...In his characteristically humouristic tone, President Kikwete grinningly said that these opponents of dual citizenship are saying that their fellows who are abroad want to ‘kula huku na huku', which when literally translated means, they ‘want to eat here and there.' It is obvious he was referring to certain ‘Intellectuals at the Hill', that is, those at the University of Dar es Salaam (UDSM) which is still highly regarded as the leading higher learning institution in Tanzania. The president promised, however, that they will keep on educating, as in sensitising the people, about it, that is, presumably about its benefits.
...alaaa kumbee! kwahiyo wanaona bora mzawa mwenye uraia wa nje aje nyumbani kufanya kazi kama Expatriate sio?
Naam wanajukwaa
Nafurahi kujiunga na JF, nachukulia jukwaa hili kama ni sehemu ya kujifunza.
Takwimu za tanzania zinaonyesha kuwa kuna watanzania zaidi ya 1.2m wanaoishi nje ya nchi [rejea ripoti ya Tanzania Law Review Commission]. Naam hii ni karibu 3% ya taifa zima.
Nadhani wakati umefika sasa serikali ikapitisha sheria kuruhusu raia hawa kuweza kufaidi matunda ya uraia wa nchi mbili kwani kwa sasa wengi wanakwazwa na kuwa wakiamua kuchukua uraia mwingine inabidi waamue kuachia uzalendo wao.
Swali hili niliwahi kumuuliza mheshimiwa Sumaye alipokuja hapa Uingereza mwaka jana akakiri kuwa ni muhimu kuruhusu lakini hakuweza kutoa sababu kwa nini hasa mpaka sasa Tanzania imeshindwa kuwa sheria ya kuruhusu uraia wa nchi mbili.
Sasa hivi watanzania wengi wanaoishi Uingereza na nchi nyinginezo za Magharibi wanaweza kupata misaada kadhaa ya kuwekeza nchini mwao lakini kwa vile wengi wameamua kuwa na uraia wa nchi mbili bila kuachia uraia wao wa TZ basi inakuwa hawawezi kuwekeza nyumbani na kama watawekeza wataweka katika mfumo usio rasmi kama vile kuwatumia ndugu na jamaa pesa ili waweze kuwekeza,matokeo yake ni kuwa kwa vile ndugu hana uwezo wa biashara au kutokuwa muaminifu inakuwa ndio hivyo tena hela zinakwenda na hakuna linalofanyika,hii ina athari zaidi kwani mtu huyu hutotegemea akamhimiza mwenzie wa tanzania kuwa kawekeze nyumbani.
Naam mniwie radhi wanajukwaa nadhani ngwe yangu hapa mtandaoni italelemea zaidi katika kuwawezesha na kuwajali raia wote wa tanzania na kwa vile tuna asilimia 3% ya hawa wapo nje basi nao inabidi waainishe hoja zao ikiwemo na matatizo wayapatao,mwishowe waweze kuwa nao ni washiriki wazuri wa shughuli za kiuchumi Tanzania.
Mfano wa China ututoshe:
Kuna wachina 48 milioni nje ya nchi yao.Kuna wizara ya kushughulikia wachina waliopo nje ambayo inakuwa ni kama kiambatanishi cha wizara ya mambo ya nje ambapo wana jukumu la kuhakikisha kila mchina mwenye uwezo wa kutoa mchango kwao anawezeshwa bila vikwazo na pia wachina waliopo nje waweze kuwa wanapata habari na taarifa sahihi kuhusu hali ya uchumi,siasa,jamii nk wakati wote.
Angalia kwetu:
Balozi zetu zipo mbali na watanzania au tusema baadhi zimejitenga sana,ni kwa sababu kuwa karibu au mbali kunategemea na hulka ya balozi husika,kama ni mtu wa watu basi watu 'watajichanganya' kama sivyo basi watu hola! Nukta ni nini hapa? ni kuwa inabidi kuwe na ainisho maalum kwenye kazi za balozi katika kuwashughulikia watanzania.
Inatokea Rais anakuja kwenye nchi husika balozi anamkimbiza asionane na watanzania!
Natumai Ari mpya haitokuwa hivi na mabalozi nao watawajali watanzania hawa. Maoni yanakaribishwa, ''i stand to be corrected''[/Q
Angalia kwetu:
Balozi zetu zipo mbali na watanzania au tusema baadhi zimejitenga sana,ni kwa sababu kuwa karibu au mbali kunategemea na hulka ya balozi husika,kama ni mtu wa watu basi watu 'watajichanganya' kama sivyo basi watu hola! Nukta ni nini hapa? ni kuwa inabidi kuwe na ainisho maalum kwenye kazi za balozi katika kuwashughulikia watanzania
Niliandika email kwenda ubalozini kuhusu Ratiba ya kmwona balozi mwakilishi wake hapa Victoria, Aussie haikujibiwa mwanangu. Hii ina maana kama ulivyosema kuwa mabalozi siyo watu wa kuongea na Mtanzania hana nafasi hiyo.
Njooni. Karibuni sana. Angalau mtakuwa na kauzalendo kidogo ka asili moyoni na kuijali nchi yetu kuliko hawa expats wanaotuletea 'Dead Aid' na 'Loliondogate'!
Law on dual citizenship coming
2008-07-15 10:16:03
By Bilal Abdul-Aziz, Dodoma
The government yesterday said it was in the process of drafting a new law that would allow Tanzanians to have dual citizenship.
Home Affairs deputy minister Khamis Kagasheki told the House that the Union and Zanzibar governments were jointly looking into the matter.
The deputy minister was responding to a question posed by Mwadini Jecha (Wete, CUF) who had wanted to know when the government would table a bill proposing the enacting of a new law on the matter.
``The Union government and that of Zanzibar are carefully looking into the matter. When the process has been completed, my ministry will bring the bill in the House for approval,`` said Kagasheki.
Earlier on, the deputy minister told Parliament that under the Union constitution, dual citizenship was illegal.
He said the law denied the people of Tanzania a chance to possess dual citizenship, and their Tanzanian citizenship ceased once they opted for other citizenship.
Kagasheki said the current laws particularly affected Tanzanian children born outside the country, who on reaching 18 years, were required to denounce the citizenship of one of their parents if they wanted to keep the Tanzanian citizenship.
``The system is not much known by our people. For that reason, at times, children encounter problems when they apply for passports or seek sponsorship for higher education,`` he said.
SOURCE: Guardian
I will not seek the citizenship of another nation for my loyalty remains and will forever be to Tanzania and Tanzania only.
http://www.blog.co.tz/mapambazuko
I am giving the Tanzanian Government until March 1, 2010 to come up with something solid about dual citizenship.
Else, I will be forced by circumstances to apply for American Citizenship.
I will keep you updated.
Hii gharama ya visa imepanda lini tena, the last time nilikuwepo ilikuwa $50 per person.Post yako haina ukweli wowote. Tunaonyesha kuwa kuna watu mbalimbali wa mataifa mengine ambao wangepata
uraia wa Tanzania bila kukana uraia wa nchi walizozaliwa wangeweza kufanya biashara za kulijenga taifa.
Hivyo suala la uraia una pande mbili. Una pande za watanzania (Diaspora) wanaotaka kuchukua uraia wa
nchi nyingine bila kuukana uraia wao wa Tanzania. Na kuna raia wa nchi zingine wanaotaka kuishi Tanzania
kama watanzania bila kuukana uraia wa nchi zao.
Kuhusu faida unazoonyesha haina ukweli wowote. Hoja ni lazima ijengwe na data na sio maneno matamu. Idadi ya watanzania
waliopo nje haionyeshi kuwa watatumia uraia wa nchi mbili kufanya vitendo vya uharifu kwa nchi wanazokaa au kwa nchi waliyozaliwa.
Na vilevile Tanzania ni mwanachama wa mashirika mbalimbali na ina mikataba ya kurudisha waarifu na nchi mbalimbali. Hivyo point yako
haina nguvu.
Kuhusu kujiunga na majeshi. Tanzania ina professional army. Na lile jeshi la lazima lilikuwa kwa wanafunzi
wanaomaliza vyuo. Na miaka ya 90 ni wanafunzi 10,000 tu kwa mwaka. Hii ni idadi ndogo sana kulinganisha na population ya Tanzania.
Kuhusu ada ya visa kutumika kama chanzo cha mapato ya uchumi, hapo umechemsha sana. Hakuna hata nchi moja duniani inayotegemea
ada ya visa kama chanzo cha mapato yake. Ada ya Visa ni kama kodi ya ushuru. Unapoongeza ushuru, watu wanapunguza matumizi ya vitu.
Ada ya visa inapokuwa kubwa, watu wanaacha kutembelea nchi yako. Na wakitembelea watabadana matumizi.
Mtu mwenye familia ya watu wanne akitaka kutembelea Tanzania itabidi alipe dollar 400 kwa ajili ya visa. Kama akipata visa bure atatumia
pesa hizo kwa matumizi akiwa Tanzania. Matumizi yana direct and indirect positive impacts katika uchumi wa nchi kuliko ushuru wa Visa.