Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

''Sisi watanzania'' hao kina sisi unamaanisha nani na nani??? Maana unajumuisha watu as if tulikaa watz wote tukaamua huyo ugoro wako ulouleta...siku nyingine andika wewe na mke wako na familia yako sio..''SISI WATANZANIA''
Watanzania wote wamemchoka jiwe

Huenda wewe ni mrwanda
 
Ccm ipi? Mwenyekit gan atampitisha kwenye KAMATI KUU?
CCM imeshagawanyika vipandevipande,kuna CCM maslahi (ya Magufuli) na CCM original isiyompenda Magufuli kwa ukatili wake na udikteta na jinsi anavyoharibu maisha ya watu,nyie mnaopenda Magufuli mna akili za watu wa sayari ya Pluto.
 
Halafu uzuri wa membe taarifa za kutekwa kwake anazipata mapema, spymaster.
Mambe hana resource nyingi kuliko alizokuwa nazo Marehemu Kombe ambae alikuwa Chief wa Spymasters.
Msimponze Membe akajaribu kupinduka sarakasi kwenye wild fire huku kavaa spandex ya nailoni.

Mirija yote na masalia ya awamu mbili zilizopita imekatwa huko kwenye mfumo. Hawana informer yeyote huko jikoni.
 
CCM imeshagawanyika vipandevipande,kuna CCM maslahi (ya Magufuli) na CCM original isiyompenda Magufuli kwa ukatili wake na udikteta na jinsi anavyoharibu maisha ya watu,nyie mnaopenda Magufuli mna akili za watu wa sayari ya Pluto.
Jidanganyeni, tu, ikiwa upinzan unakufa ,je kwenye urais ndio mtatoboa?
 
Mkuu Jana niliandika na Leo narudia muujiza wa Members kuwa rais,ni mpaka JPJM atangaze kuwa hatagombea urais means 2020.
Lakini JPJM akigombea,mwaka 2025 Members umri utakuwa umemtupa mkono.
Hawa CCM Kila wakati wanaleta rais kijana kuliko aliyemaliza muda wake.
Nyerere alikuwa mkubwa kwa Mwinyi,Mwinyi alikuwa mkubwa kwa Mkapa .Mkapa alikuwa mkubwa kwa Kikweye.Kikwete alikuwa mkubwa kwa Magufuli.
Sasa trend Kama no hiyo unategemea Members aje awe rais kwa tiketi ya ccm?
Anaweza kugombea 2020 kupitoa opposition lakini Sio ccm.
Mimi naamin katika ukweli kwamba Kila kitu hupangwa na Mungu,Magufuli hata kabla hajazaliwa Mungu alishampa urais,wengi wanaoutafuta leave nguvu kubwa Mungu hakuwadhiria,hivyo hawawezi kuupata.
 
Sometimes muwe mnaacha kujitoa ufahamu. Kauli ya Membe itakufariji vipi? Membe huyu si lolote si chochote. Magufuli keshaiteka CCM yenu na hata kina Mkapa hawapumui. Mnae tu atleast until 2025
Acha wamjaze upepo akianza kushughulikiwa nje ndani wasilalamike ooh anaonewa
 
Kwa taarifa yako, JPM anapendwa sana ma wananchi kuliko unavyodhani. Hasa wale wananchi wa kipato cha chini, ambao wanajihisi hawana la kupoteza, na ambao wana uwezo wa kuingia barabarani kushinikiza lolote. Wananchi hao wenye mapenzi na JPM hawapo kwenye mitandao ya Kijamii, hawana uwezo wa kumiliki simu janja, ila utakutana nao mtaani kwenye mabox ya kupiga kura. Hao ndio waliopanga foleni na kupiga kura kumchagua JPM, na ndio hao WATANZANIA ambao Rais ameapa kuwasimamia na kuwatetea kwa nguvu zote.

Nikupe mfano, hivi karibuni ulikuja msukumo wa kimtandao wa MANGE, kushawishi watu waandamane. Watu wengi humu kwenye mitandao walichangia kwa mtazamo kwamba wapo tayari kufa, lakini wataenda kuandamana. Lakini, hakutokea hata mmoja wao kuandamana hapa Tanzania, na hata huko nchi za nje pia hawakutokea kujionesha barabarani.

Wengi wenu, ambao wanaleta mada kama hizi hapa, hawana ujasiri wa kusimamia haya wanayoyaandika hapa, wanajificha nyuma ya keyboard. Wengine wanaleta haya mabandiko kutokana na nguvu ya pesa, wamelipwa kufanya hivo, na pengine hata myoyo yao ina mapemzi na JPM. Wengine wanapenda tu kuona nchi yetu inapata msuko suko, na tunapoteza muda wetu mwingi kuongelea maswala ya SIASA na kuacha kujadili mambo ya msingi kama vile bei nzuri ya KOROSHO kwaajili ya wakulima wa KiTanzania.

Haihitaji elimu kubwa kugundua kwamba Mh. Membe hakuwa na uwezo wa kulitoa Taifa pale alipokua ametuacha Mh. JK. Hata kama Membe angepata nafasi ya kuwa Rais asingeweza kufanya hata robo ya haya aliokwisha fanya JPM ndani ya miaka hii 3. Ili lipo wazi, hata wale waliokua mawaziri katika kipindi cha JK ukiwauliza hili wanalijua. Walikua wanafahamiana kiwango cha ubora wao, na JPM alikua anafahamika kwa utendaji kazi.JK alikua anajua na hata wananchi pia wanajua. Alikuwa wapi Membe?? isitoshe uwezo wake dhaifu wa uongozi na udhalimu wake pia unafahamika na wenzie na hata wananchi ( tusifukue makaburi).Ni dhahiri Mh. Membe asingetufaa kwa nafasi ya Rais, na hatufai sasa na hatufai kamwe. Achilia mbali 2020, hata ikifika 2025 CCM inayo hazina ya viongozi vijana, na bora zaidi ya Membe , itatupatia Mgombea atakaetupeleka mbele zaidi.

Ndani ya hi miaka 3, wananchi tumeshudia mengi yametekelezwa kwa vitendo. Tanzania hii sio ile ya zamani. Serikali imekua karibu zaidi na wananchi kutatua kero na kusikiliza shida zao. Mawaziri wa Serikali hii kila siku wapo njiani kuzungukia wananchi. Hamna waziri anaesafiri nje hovyo, kama tulivyokua tukishuhudia zamani. Ingefaa, wananchi tumuunge mkono Rais wetu ili apate nguvu zaidi ya kufanya makubwa zaidi katika kipindi chake cha mika 7 iliobaki kikatiba.

 
Mkuu Matola sidhani kama umenielewa!
 
Kwa point hizo tu,kuna haja gani ya kuwa na Magufuli?
 
Mkuu hivi unadhani hao waliousuka huu mpango wanasubiri hadi 2020 ndio mtu wao agombee?. Acha kukariri ndugu, chochote kinaweza kutokea hakuna ajuae kesho.
 


Usiombee kijana, Membe hafai kwa taifa letu. He is as useless as Kikwete.....Tanzania tulimuhitaji Magufuli tu aje kunyoosha hii nchi.
 
Mtaimba Ngonjera na mashairi na tenzi zote Mwaka huu, Hizo siasa chafu haziepukiki Africa, what matters is Nchi ijengwe kwanza hizo siasa badae.
 
Vipi hakuwa na JESHI, UENYEKITI WA CHAMA NA TISS YA HUKO KWAO??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…