Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

''Sisi watanzania'' hao kina sisi unamaanisha nani na nani??? Maana unajumuisha watu as if tulikaa watz wote tukaamua huyo ugoro wako ulouleta...siku nyingine andika wewe na mke wako na familia yako sio..''SISI WATANZANIA''
Watanzania wote wamemchoka jiwe

Huenda wewe ni mrwanda
 
Ccm ipi? Mwenyekit gan atampitisha kwenye KAMATI KUU?
CCM imeshagawanyika vipandevipande,kuna CCM maslahi (ya Magufuli) na CCM original isiyompenda Magufuli kwa ukatili wake na udikteta na jinsi anavyoharibu maisha ya watu,nyie mnaopenda Magufuli mna akili za watu wa sayari ya Pluto.
 
Halafu uzuri wa membe taarifa za kutekwa kwake anazipata mapema, spymaster.
Mambe hana resource nyingi kuliko alizokuwa nazo Marehemu Kombe ambae alikuwa Chief wa Spymasters.
Msimponze Membe akajaribu kupinduka sarakasi kwenye wild fire huku kavaa spandex ya nailoni.

Mirija yote na masalia ya awamu mbili zilizopita imekatwa huko kwenye mfumo. Hawana informer yeyote huko jikoni.
 
CCM imeshagawanyika vipandevipande,kuna CCM maslahi (ya Magufuli) na CCM original isiyompenda Magufuli kwa ukatili wake na udikteta na jinsi anavyoharibu maisha ya watu,nyie mnaopenda Magufuli mna akili za watu wa sayari ya Pluto.
Jidanganyeni, tu, ikiwa upinzan unakufa ,je kwenye urais ndio mtatoboa?
 
Tunaomba tu CCM mtuletee huyu ndugu maana ana mikono yenye baraka na ataleta mahusiano mapya ndani na nje ya TZ.. Hana uadui wa kikabila wala wa kishangazi. Ni msomi na mwenye utashi wa kiuongozi na hekima.. Kwa kweli Anatufaa sana .. CCM mtupe raha 2020 kupitia Membe
Mkuu Jana niliandika na Leo narudia muujiza wa Members kuwa rais,ni mpaka JPJM atangaze kuwa hatagombea urais means 2020.
Lakini JPJM akigombea,mwaka 2025 Members umri utakuwa umemtupa mkono.
Hawa CCM Kila wakati wanaleta rais kijana kuliko aliyemaliza muda wake.
Nyerere alikuwa mkubwa kwa Mwinyi,Mwinyi alikuwa mkubwa kwa Mkapa .Mkapa alikuwa mkubwa kwa Kikweye.Kikwete alikuwa mkubwa kwa Magufuli.
Sasa trend Kama no hiyo unategemea Members aje awe rais kwa tiketi ya ccm?
Anaweza kugombea 2020 kupitoa opposition lakini Sio ccm.
Mimi naamin katika ukweli kwamba Kila kitu hupangwa na Mungu,Magufuli hata kabla hajazaliwa Mungu alishampa urais,wengi wanaoutafuta leave nguvu kubwa Mungu hakuwadhiria,hivyo hawawezi kuupata.
 
Sometimes muwe mnaacha kujitoa ufahamu. Kauli ya Membe itakufariji vipi? Membe huyu si lolote si chochote. Magufuli keshaiteka CCM yenu na hata kina Mkapa hawapumui. Mnae tu atleast until 2025
Acha wamjaze upepo akianza kushughulikiwa nje ndani wasilalamike ooh anaonewa
 
Kwa taarifa yako, JPM anapendwa sana ma wananchi kuliko unavyodhani. Hasa wale wananchi wa kipato cha chini, ambao wanajihisi hawana la kupoteza, na ambao wana uwezo wa kuingia barabarani kushinikiza lolote. Wananchi hao wenye mapenzi na JPM hawapo kwenye mitandao ya Kijamii, hawana uwezo wa kumiliki simu janja, ila utakutana nao mtaani kwenye mabox ya kupiga kura. Hao ndio waliopanga foleni na kupiga kura kumchagua JPM, na ndio hao WATANZANIA ambao Rais ameapa kuwasimamia na kuwatetea kwa nguvu zote.

Nikupe mfano, hivi karibuni ulikuja msukumo wa kimtandao wa MANGE, kushawishi watu waandamane. Watu wengi humu kwenye mitandao walichangia kwa mtazamo kwamba wapo tayari kufa, lakini wataenda kuandamana. Lakini, hakutokea hata mmoja wao kuandamana hapa Tanzania, na hata huko nchi za nje pia hawakutokea kujionesha barabarani.

Wengi wenu, ambao wanaleta mada kama hizi hapa, hawana ujasiri wa kusimamia haya wanayoyaandika hapa, wanajificha nyuma ya keyboard. Wengine wanaleta haya mabandiko kutokana na nguvu ya pesa, wamelipwa kufanya hivo, na pengine hata myoyo yao ina mapemzi na JPM. Wengine wanapenda tu kuona nchi yetu inapata msuko suko, na tunapoteza muda wetu mwingi kuongelea maswala ya SIASA na kuacha kujadili mambo ya msingi kama vile bei nzuri ya KOROSHO kwaajili ya wakulima wa KiTanzania.

Haihitaji elimu kubwa kugundua kwamba Mh. Membe hakuwa na uwezo wa kulitoa Taifa pale alipokua ametuacha Mh. JK. Hata kama Membe angepata nafasi ya kuwa Rais asingeweza kufanya hata robo ya haya aliokwisha fanya JPM ndani ya miaka hii 3. Ili lipo wazi, hata wale waliokua mawaziri katika kipindi cha JK ukiwauliza hili wanalijua. Walikua wanafahamiana kiwango cha ubora wao, na JPM alikua anafahamika kwa utendaji kazi.JK alikua anajua na hata wananchi pia wanajua. Alikuwa wapi Membe?? isitoshe uwezo wake dhaifu wa uongozi na udhalimu wake pia unafahamika na wenzie na hata wananchi ( tusifukue makaburi).Ni dhahiri Mh. Membe asingetufaa kwa nafasi ya Rais, na hatufai sasa na hatufai kamwe. Achilia mbali 2020, hata ikifika 2025 CCM inayo hazina ya viongozi vijana, na bora zaidi ya Membe , itatupatia Mgombea atakaetupeleka mbele zaidi.

Ndani ya hi miaka 3, wananchi tumeshudia mengi yametekelezwa kwa vitendo. Tanzania hii sio ile ya zamani. Serikali imekua karibu zaidi na wananchi kutatua kero na kusikiliza shida zao. Mawaziri wa Serikali hii kila siku wapo njiani kuzungukia wananchi. Hamna waziri anaesafiri nje hovyo, kama tulivyokua tukishuhudia zamani. Ingefaa, wananchi tumuunge mkono Rais wetu ili apate nguvu zaidi ya kufanya makubwa zaidi katika kipindi chake cha mika 7 iliobaki kikatiba.

Kuna watu tukisema Membe aongoze nchi 2020 wanabeza
Wengine wanatuita sisi ni vibaraka Wa Membe kitu ambacho sio cha kweli, Mimi sio kibaraka Wa Membe wala mheshimiwa Membe Mimi hanijui

Kitu ninachoamini ndicho nitaendelea kuamini, kwa sasa watanzania tumebadilika japo tume ya uchaguzi na vyombo vya Dora ndio hawataki kubadilika wanaturudisha nyuma

Ile kanuni ya kwamba Raisi lazima atawale miaka kumi imepitwa na wakati
Tukikupa miaka mitano ikakushinda basi kaa pembeni waachie wengine wanaoweza

Kwa miaka mitatu tu hii mambo yanaenda kombo

Vijana hawana ajira, tangu nchi kupata Uhuru awamu hii ya tano ndio awamu ambayo vijana wengi wamerandaranda mitaani bila ajira hata zile ajira za ualimu, nursing, udaktari hazipo tena

Ndani ya miaka hii mitatu watu wamefukuzwa kazi hovyo hovyo wamekua tegemezi, watu wamerudishwa kwenye Lindi la umaskini, watumishi Wa umma hawajapanda madaraja wala kuongezwa mishahara, kila siku uhakiki uchwara usio na kikomo

Ndani ya miaka mitatu ahadi zimeshindwa kutekelezeka zimebaki ni ahadi hewa, milioni hamsini kila kijiji imekua longolongo tu, ajira kwa vijana kama mnavyojionea mwenyewe,

Ndani ya miaka mitatu tumeshuhudia kauli za kibabe zisizo na mashiko kwa wananchi na viongozi wengine, wananchi wananangwa, viongozi wanatishwatishwa hovyo hovyo kama watoto wadogo

Kwa miaka hii mitatu tumeshuhudia mtu mmoja kuwa one man show, kila kitu anataka awe fonti fedi sijajua ni kupenda sifa au ni nini

Ndani ya awamu hii ndio tumeshuhudia taifa linaingia kwenye gharama za mauchaguzi uchwara yasiyo na tija kodi za wananchi zinachezewa, wananchi tumefanywa wajinga kupindukia,

Kwahayo machache yapo mengine mengi japo yapo na mambo mazuri yaliyofanyika lakini tunasema asante na yatosha sasa

2020 yafaa kwenda na mtu mwingine naye ni Bernard Membe

Bernard Membe unafaa kutuongpza
Iwe mvua liwe jua tutakua nyuma yako

Hatuwezi tena kuwasapoti watu wasio na shukrani

2020 Twende na BENARD MEMBE[emoji818]

#MEMBE_FOR_PRESIDENT2020
 
Kwahiyo mkuu unatushauri tuendelee kutawaliwa na hawahawa ccm?

Jitafakari upya tatizo siyo Magufuli ba li tatizo ni ccm, ukikaa na ukatuliza akili utaelielewa hili vizuri, Magufuli ana kura moja tu hata kama ni ya veto, veto huwa haina nguvu ya kushindana na kura nyingi.

Ccm ni mashetani akiwemo huyo Membe, mateso tunayopitia leo hayaletwa na Magufuli bali ni mashetani wa ccm kuikataa rasimu ya katibsa mpya ya Warioba.

Someni biblia mtaelewa vizuri Mungu aliwachapa Waisrael pale walipokengeuka, na Watanzania wanastahili kuishi maisha magumu ili akili ziwarudie.
Mkuu Matola sidhani kama umenielewa!
 
Ana wananchi wenye machungu na kupoteza kazi zao, machungu ya kudhalilishwa, machungu ya kubomolewa nyumba zao, machungu ya kutukanwa vilaza, machungu ya kutoona local chanel, machungu ya kutoona bunge live, machungu ya kupigiwa shangazi zao, machungu ya gharama za maisha kuwa juu, machungu ya sukari kugoma kushuka bei. Huku mtaani wanamachungu sana. We acha tu mzee
Kwa point hizo tu,kuna haja gani ya kuwa na Magufuli?
 
Mkuu hivi unadhani hao waliousuka huu mpango wanasubiri hadi 2020 ndio mtu wao agombee?. Acha kukariri ndugu, chochote kinaweza kutokea hakuna ajuae kesho.
 
Habari wakuu

Kutokana na hali inavyoenda ya uendeshaji wa nchi ni wazi rais anatakiwa abadilishwe kupitia sanduku la kura mwaka 2020

Hivyo sisi watanzania tunapenda na tunatamani kusikia sauti ya kiongozi wetu mpendwa mwenye nia ya kulivusha taifa kwa hapa lilipokwamia, ndugu, mheshimiwa na mwanadiplomasia Benard Membe

Jitokeze wazi tusikie kauli yako watanzania tufarijike kwani mwaka 2020 ni jirani sana

Nawasilisha


Usiombee kijana, Membe hafai kwa taifa letu. He is as useless as Kikwete.....Tanzania tulimuhitaji Magufuli tu aje kunyoosha hii nchi.
 
Mambo ya kutekana tekana hatutaki kuyasikia tena
Uhai wa mtu mmoja una thamani sana kuliko kujenga reli toka Zanzibar hadi Marekani kupitia Tanganyika.
Mungu aliupenda ulimwengu, akawaumba Binadamu na kuwapa nchi waitawale na kula matunda yake.
Ingekuwa Reli ni Bora kupita uhai wa binadamu basi Mungu angetengeneza njia za Reli ya kuziunganisha nchi zote duniani
Lakini badala yake akamwumba Adamu na Hawa.
Mtu akikatika mguu mmoja na kubakia kilema, hata ukiyauza madini yote ya dunia hii huwezi kununua mguu mmoja wa mtu mmoja na kumrudishia.
Hata ukiamua kuiuza dunia yote huwezi kununua spea ya mkono wa mtu mmoja.
Ni vipi leo tunathamini vitu vya kutengenezwa na binadamu na kumdunisha binadamu mwenyewe aliyetengeneza hicho kitu ?
Tunamtaka Raisi ambaye.
Kipaumbele chake namba moja ni=

" Kumthamini Binadamu "

[emoji117] Nchi iliumbwa kwa ajiri ya mtu na sio mtu kwa ajiri ya nchi.
Mtaimba Ngonjera na mashairi na tenzi zote Mwaka huu, Hizo siasa chafu haziepukiki Africa, what matters is Nchi ijengwe kwanza hizo siasa badae.
 
Naona kama mnajifurahisha, yaani naona kama Maigizo, watu na akili zenu mnakaa mnadanganyana Membe anaenda kuchukua nchi 2020.

Mimi na akili zangu za kuvukia barabara nauliza ATAPITIA NJIA GANI?

Ndani ya CCM , Mwenyekiti ndiye mgombea urais na ndiye mwenye sauti ya mwisho ,

Kupitia Upinzani ,ndio kabisa hawezi kushinda , Tuliona kwa LOWASSA,.
Labda kama ana hela za kuchezea,

Kupitia Uhaini, hapa atadakwa mapema sana..

NAWAULIZA NYIE MLIOKULA HELA ZAKE NA KUTUMWA MITANDAONI , MNAJUA ATAKUWA RAIS KWA NJIA GANI?

Mtuambie, sio mnasumbua mitandaoni lakini hamtuambii atapitia njia gani , ya golgotha au kaanani,

JIWE ameshajizatiti ana JESHI, TISS, UHAMIHAJI, POLIS , TUME YA UCHAGUZI,N.K

MEMBE ana nini? Au anataka kuliwa hela zake kama Lowassa?
Vipi hakuwa na JESHI, UENYEKITI WA CHAMA NA TISS YA HUKO KWAO??
 
Back
Top Bottom