Kwa taarifa yako, JPM anapendwa sana ma wananchi kuliko unavyodhani. Hasa wale wananchi wa kipato cha chini, ambao wanajihisi hawana la kupoteza, na ambao wana uwezo wa kuingia barabarani kushinikiza lolote. Wananchi hao wenye mapenzi na JPM hawapo kwenye mitandao ya Kijamii, hawana uwezo wa kumiliki simu janja, ila utakutana nao mtaani kwenye mabox ya kupiga kura. Hao ndio waliopanga foleni na kupiga kura kumchagua JPM, na ndio hao WATANZANIA ambao Rais ameapa kuwasimamia na kuwatetea kwa nguvu zote.
Nikupe mfano, hivi karibuni ulikuja msukumo wa kimtandao wa MANGE, kushawishi watu waandamane. Watu wengi humu kwenye mitandao walichangia kwa mtazamo kwamba wapo tayari kufa, lakini wataenda kuandamana. Lakini, hakutokea hata mmoja wao kuandamana hapa Tanzania, na hata huko nchi za nje pia hawakutokea kujionesha barabarani.
Wengi wenu, ambao wanaleta mada kama hizi hapa, hawana ujasiri wa kusimamia haya wanayoyaandika hapa, wanajificha nyuma ya keyboard. Wengine wanaleta haya mabandiko kutokana na nguvu ya pesa, wamelipwa kufanya hivo, na pengine hata myoyo yao ina mapemzi na JPM. Wengine wanapenda tu kuona nchi yetu inapata msuko suko, na tunapoteza muda wetu mwingi kuongelea maswala ya SIASA na kuacha kujadili mambo ya msingi kama vile bei nzuri ya KOROSHO kwaajili ya wakulima wa KiTanzania.
Haihitaji elimu kubwa kugundua kwamba Mh. Membe hakuwa na uwezo wa kulitoa Taifa pale alipokua ametuacha Mh. JK. Hata kama Membe angepata nafasi ya kuwa Rais asingeweza kufanya hata robo ya haya aliokwisha fanya JPM ndani ya miaka hii 3. Ili lipo wazi, hata wale waliokua mawaziri katika kipindi cha JK ukiwauliza hili wanalijua. Walikua wanafahamiana kiwango cha ubora wao, na JPM alikua anafahamika kwa utendaji kazi.JK alikua anajua na hata wananchi pia wanajua. Alikuwa wapi Membe?? isitoshe uwezo wake dhaifu wa uongozi na udhalimu wake pia unafahamika na wenzie na hata wananchi ( tusifukue makaburi).Ni dhahiri Mh. Membe asingetufaa kwa nafasi ya Rais, na hatufai sasa na hatufai kamwe. Achilia mbali 2020, hata ikifika 2025 CCM inayo hazina ya viongozi vijana, na bora zaidi ya Membe , itatupatia Mgombea atakaetupeleka mbele zaidi.
Ndani ya hi miaka 3, wananchi tumeshudia mengi yametekelezwa kwa vitendo. Tanzania hii sio ile ya zamani. Serikali imekua karibu zaidi na wananchi kutatua kero na kusikiliza shida zao. Mawaziri wa Serikali hii kila siku wapo njiani kuzungukia wananchi. Hamna waziri anaesafiri nje hovyo, kama tulivyokua tukishuhudia zamani. Ingefaa, wananchi tumuunge mkono Rais wetu ili apate nguvu zaidi ya kufanya makubwa zaidi katika kipindi chake cha mika 7 iliobaki kikatiba.
Kuna watu tukisema Membe aongoze nchi 2020 wanabeza
Wengine wanatuita sisi ni vibaraka Wa Membe kitu ambacho sio cha kweli, Mimi sio kibaraka Wa Membe wala mheshimiwa Membe Mimi hanijui
Kitu ninachoamini ndicho nitaendelea kuamini, kwa sasa watanzania tumebadilika japo tume ya uchaguzi na vyombo vya Dora ndio hawataki kubadilika wanaturudisha nyuma
Ile kanuni ya kwamba Raisi lazima atawale miaka kumi imepitwa na wakati
Tukikupa miaka mitano ikakushinda basi kaa pembeni waachie wengine wanaoweza
Kwa miaka mitatu tu hii mambo yanaenda kombo
Vijana hawana ajira, tangu nchi kupata Uhuru awamu hii ya tano ndio awamu ambayo vijana wengi wamerandaranda mitaani bila ajira hata zile ajira za ualimu, nursing, udaktari hazipo tena
Ndani ya miaka hii mitatu watu wamefukuzwa kazi hovyo hovyo wamekua tegemezi, watu wamerudishwa kwenye Lindi la umaskini, watumishi Wa umma hawajapanda madaraja wala kuongezwa mishahara, kila siku uhakiki uchwara usio na kikomo
Ndani ya miaka mitatu ahadi zimeshindwa kutekelezeka zimebaki ni ahadi hewa, milioni hamsini kila kijiji imekua longolongo tu, ajira kwa vijana kama mnavyojionea mwenyewe,
Ndani ya miaka mitatu tumeshuhudia kauli za kibabe zisizo na mashiko kwa wananchi na viongozi wengine, wananchi wananangwa, viongozi wanatishwatishwa hovyo hovyo kama watoto wadogo
Kwa miaka hii mitatu tumeshuhudia mtu mmoja kuwa one man show, kila kitu anataka awe fonti fedi sijajua ni kupenda sifa au ni nini
Ndani ya awamu hii ndio tumeshuhudia taifa linaingia kwenye gharama za mauchaguzi uchwara yasiyo na tija kodi za wananchi zinachezewa, wananchi tumefanywa wajinga kupindukia,
Kwahayo machache yapo mengine mengi japo yapo na mambo mazuri yaliyofanyika lakini tunasema asante na yatosha sasa
2020 yafaa kwenda na mtu mwingine naye ni Bernard Membe
Bernard Membe unafaa kutuongpza
Iwe mvua liwe jua tutakua nyuma yako
Hatuwezi tena kuwasapoti watu wasio na shukrani
2020 Twende na BENARD MEMBE[emoji818]
#MEMBE_FOR_PRESIDENT2020