GE2025 Urais wa zamu wakristo na waislamu ni kansa ya Chuki kwa Taifa na mfumo uliopitwa na wakati

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Kwenye mahojiano kati ya Polepole na Jenerali Ulimwengu
Polepole aliaambiwa ataje miiko sijui 10 ya CCM, halafu akaulizwa tokea wakati yeye yuko ndani na uongozi mkubwa, atoe ushahidi hata ya moja yake ilikuwa zinafuatwa na CCM, akabaki anaumauma maneno.....
Ccm wanaishi miaka ya ujima ya kutegemea huruma ya rais na sio utawala wa sheria yani wanaishi miaka ya Nyerere hilo ndo shida lakini yatafika mwisho haya
 
hakuna kitu zamu katika uraisi, wabongo mumezoea kukariri story za vijiweni tu
 
GT
Hiki ndo kirusi kikuu kinacholitafuna taifa na pengine kuzidi kurudi nyuma tena nyuma zaidi. Hatutaendelea kamwe na tutazidi kuchukiana milele ajenda kuu ya wanasiasa wetu ni wizi ila wanatuchonganisha kwa makusudi.

Akili za hawa waumini wetu wanazijua wao wenyewe bahati mbaya hata watawala wakizidiwa hoja wanajiweka karibu na watu wa dini yake kutafuta huruma. Ni wapi pameandikwa kwamba waislamu.na wakristo wapeane uraisi kwa zamu?

Hatuwezi kwenda mbele kwa akili hizi za kukaanga maandazi Never. Ifike mahali rais apatikane kwa uwezo wake madhubuti na uzalendo katika kulitumikia taifa bila upendeleo.
Hata sielewi ni kichaa gani aliye anza kuyatamka hayo maneno. Ndiyo maana hali ya nchi imekuwa ya hovyo kiasi hiki.
 
Ni wapi pameandikwa kwamba waislamu.na wakristo wapeane uraisi kwa zamu?
Ifike mahali rais apatikane kwa uwezo wake madhubuti na uzalendo katika kulitumikia taifa bila upendeleo.
Kwa hakuna mahali popote pameandikwa urais ni kupokeza kwa Mkristo na Muislamu Thread 'Kete ya Dhana ya 'Zamu za Kupokezana' ina turufu yoyote katika Mustakabali wa 'Urais' wa JMT?' Kete ya Dhana ya 'Zamu za Kupokezana' ina turufu yoyote katika Mustakabali wa 'Urais' wa JMT?

Ila tujifunze kuwa na shukrani,
bila huko kupokezana, kuna dini, urais wangeishia kuusikia tuu!. Thread 'Japo hakuna kupokezana: Kiukweli, kihaki, kihalali na ki-Muungano, 2015 Si Zamu ya Zanzibar?' Japo hakuna kupokezana: Kiukweli, kihaki, kihalali na ki-Muungano, 2015 Si Zamu ya Zanzibar?

Tena japo haijaandikwa popote, akiwa ni Mkristo, lazima awe Mkatoliki!.
Julius Mkatoliki
Ben Mkatoliki
JPM Mkatoliki
Emmanuel ni Mkatoliki!
Thread 'Mpeni Mungu yaliyo ya Kimungu na Kaisari yaliyo ya Kaisari! Hiki kinachofanywa na Baraza la Maaskofu Katoliki, sio kuchanganya dini na siasa?' Mpeni Mungu yaliyo ya Kimungu na Kaisari yaliyo ya Kaisari! Hiki kinachofanywa na Baraza la Maaskofu Katoliki, sio kuchanganya dini na siasa?

Na kwa taarifa yako, uchaguzi mkuu huu utakuwa salama kwasababu Thread 'Kanisa Katoliki Tanzania: Mkombozi wa Kweli wa Taifa. Leo tumefunga Novena; Tunakesha na Kuomba, kuiombea Tanzania - A Very Powerful Prayer!' GE2025 - Kanisa Katoliki Tanzania: Mkombozi wa Kweli wa Taifa. Leo tumefunga Novena; Tunakesha na Kuomba, kuiombea Tanzania - A Very Powerful Prayer!

Udini kwenye siasa ni sumu Thread 'Sumu ya Siasa za Udini, Ukanda na Ukabila, "Is It Real? au ni Dhana Tuu?."' Sumu ya Siasa za Udini, Ukanda na Ukabila, "Is It Real? au ni Dhana Tuu?."

Mwisho Thread 'Wajua Wakristo na Waislamu Watoto wa Baba Mmoja Ibarahim?Mungu Wao ni Mmoja?na Sheria yao n Moja ya Mussa?Amri Kuu ni Upendo!Uchaguzi Huu Tupendane!' Wajua Wakristo na Waislamu Watoto wa Baba Mmoja Ibarahim?Mungu Wao ni Mmoja?na Sheria yao n Moja ya Mussa?Amri Kuu ni Upendo!Uchaguzi Huu Tupendane!

P
 
GT
Hiki ndo kirusi kikuu kinacholitafuna taifa na pengine kuzidi kurudi nyuma tena nyuma zaidi. Hatutaendelea kamwe na tutazidi kuchukiana milele ajenda kuu ya wanasiasa wetu ni wizi ila wanatuchonganisha kwa makusudi.

Akili za hawa waumini wetu wanazijua wao wenyewe bahati mbaya hata watawala wakizidiwa hoja wanajiweka karibu na watu wa dini yake kutafuta huruma. Ni wapi pameandikwa kwamba waislamu.na wakristo wapeane uraisi kwa zamu?

Hatuwezi kwenda mbele kwa akili hizi za kukaanga maandazi Never. Ifike mahali rais apatikane kwa uwezo wake madhubuti na uzalendo katika kulitumikia taifa bila upendeleo.
Nimeshindwa kuondoka kwenye mada yako hii, kwa sababu ni mada nzito sana na mada yenye kubeba hatma ya taifa hili kwenda mbele.

Tutafanikiwa au tutashindwa kwa pamoja kama nchi kwa sababu ya mambo kama haya tuliyo nayo kwenye jamii.

Hili siyo swala geni, tumekuwa nalo toka siku nyingi; na hasa baada ya kupata uhuru wetu.
Juhudi kubwa sana zilifanyika katika jitihada za kujenga umoja wetu kama taifa la waTanzania kwanza; kabla ya kutafutana katika tofauti zetu za kidini, au kikabila.

Kwa miaka kadhaa tulisifika kwa kuweza kuujenga umoja wetu kama waTanzania, na tuliweza kuepukana na maswala mengi ya mgawanyiko yanayotokana na tofauti zetu hizi.

Pamoja na mafanikio hayo makubwa, ile hali ya kundi fulani la kidini lililokuwa limefifishwa enzi za mwanzo, wakati huu limeibuka likiwa na nguvu zaidi; na limeweza kukichukua chama cha CCM na kukitumia kufikia malengo yaliyokuwa yamedhibitiwa huko mwanzo.

Kwa hiyo sasa hivi ni halali kabisa kupeana vyeo, siyo kwa nafasi hiyo ya juu tu ya urais, bali hata huko chini na serikalini kote kwa misingi ya kidini na siyo uwezo wa muhusika.

Kwa hiyo hii mada yako; kuifanya kuwa tatizo ni la huko kuachiana tu kwa ngazi hiyo ya juu, siyo kweli. Hali yetu sasa ni mbaya zaidi karibu katika kila ngazi; na sasa ni wazi hata ndani ya jamii mambo yameanza kuwa ya kubaguana. Hali itazidi kuwa mbaya zaidi endapo kama hatutapata viongozi wazalendo kabisa, wanaojali uTanzania wao kuliko dini zao wanazo zishikilia wao.

Nina hofu kubwa sana na Tanzania yetu hii.
 
Kwa hakuna mahali popote pameandikwa urais ni kupokeza kwa Mkristo na Muislamu Thread 'Kete ya Dhana ya 'Zamu za Kupokezana' ina turufu yoyote katika Mustakabali wa 'Urais' wa JMT?' Kete ya Dhana ya 'Zamu za Kupokezana' ina turufu yoyote katika Mustakabali wa 'Urais' wa JMT?

Ila tujifunze kuwa na shukrani,
bila huko kupokezana, kuna dini, urais wangeishia kuusikia tuu!. Thread 'Japo hakuna kupokezana: Kiukweli, kihaki, kihalali na ki-Muungano, 2015 Si Zamu ya Zanzibar?' Japo hakuna kupokezana: Kiukweli, kihaki, kihalali na ki-Muungano, 2015 Si Zamu ya Zanzibar?

Tena japo haijaandikwa popote, akiwa ni Mkristo, lazima awe Mkatoliki!.
Julius Mkatoliki
Ben Mkatoliki
JPM Mkatoliki
Emmanuel ni Mkatoliki!

P
Hongera kwa andiko Pasko, Kweli hakuna palipo andikwa. Ila kwa mujibu wa CCM ki-vitendo na kwa maneno yao akiwemo Polepole na Bashiru kwa hivi karibuni, wamenukuliwa wakisema ccm ina mila na desturi, je hili laweza kuingia hapo?

Hoja ya kuwa bila utaratibu huo kuna dini isingepata rais mimi nadhani ktk siasa jambo hilo laweza kuwa si sahihi. Kwa kuanzie pengine tungejua kwanini Wazee waasisi waliona busara ya kuweka utaratibu huo (ni kipi kiliwasukuma), je ilikuwa ni favour kwa dini fulani? kurudisha shukran? kutambua ukweli wa hali ya kisiasa ya nchi? Pili tazama population ya nchi na distribution yake ktk mikoa, unaliona hilo kama factor? Uzoefu wa Nigeria ambapo huenda kuna demography yenye mfanano na Tz ukoje?
 
Nimeshindwa kuondoka kwenye mada yako hii, kwa sababu ni mada nzito sana na mada yenye kubeba hatma ya taifa hili kwenda mbele.

Tutafanikiwa au tutashindwa kwa pamoja kama nchi kwa sababu ya mambo kama haya tuliyo nayo kwenye jamii.

Hili siyo swala geni, tumekuwa nalo toka siku nyingi; na hasa baada ya kupata uhuru wetu.
Juhudi kubwa sana zilifanyika katika jitihada za kujenga umoja wetu kama taifa la waTanzania kwanza; kabla ya kutafutana katika tofauti zetu za kidini, au kikabila.

Kwa miaka kadhaa tulisifika kwa kuweza kuujenga umoja wetu kama waTanzania, na tuliweza kuepukana na maswala mengi ya mgawanyiko yanayotokana na tofauti zetu hizi.

Pamoja na mafanikio hayo makubwa, ile hali ya kundi fulani la kidini lililokuwa limefifishwa enzi za mwanzo, wakati huu limeibuka likiwa na nguvu zaidi; na limeweza kukichukua chama cha CCM na kukitumia kufikia malengo yaliyokuwa yamedhibitiwa huko mwanzo.

Kwa hiyo sasa hivi ni halali kabisa kupeana vyeo, siyo kwa nafasi hiyo ya juu tu ya urais, bali hata huko chini na serikalini kote kwa misingi ya kidini na siyo uwezo wa muhusika.

Kwa hiyo hii mada yako; kuifanya kuwa tatizo ni la huko kuachiana tu kwa ngazi hiyo ya juu, siyo kweli. Hali yetu sasa ni mbaya zaidi karibu katika kila ngazi; na sasa ni wazi hata ndani ya jamii mambo yameanza kuwa ya kubaguana. Hali itazidi kuwa mbaya zaidi endapo kama hatutapata viongozi wazalendo kabisa, wanaojali uTanzania wao kuliko dini zao wanazo zishikilia wao.

Nina hofu kubwa sana na Tanzania yetu hii.
Ndugu, andiko lako ni zuri, ila paragraph moja bado inanishughulisha kwa maana ya kutafuta objectivity ya hoja yako na maneno yako, hio hapo chini.

Pamoja na mafanikio hayo makubwa, ile hali ya kundi fulani la kidini lililokuwa limefifishwa enzi za mwanzo, wakati huu limeibuka likiwa na nguvu zaidi; na limeweza kukichukua chama cha CCM na kukitumia kufikia malengo yaliyokuwa yamedhibitiwa huko mwanzo.

Je hili kundi la dini lilofifishwa enzi za mwanzo - huku kufifishwa tuna kujustify vipi ktk misingi ya haki? walififishwa kwa maslah ya taifa? au kwa maslah ya kundi lingine la dini? na haki itakuwa kwa kundi lipi wakati ule na sasa? Na vipi kama taifa tunaweza pata usawa wa makundi yote bila kufifishana? How do we get there objectively?

Wakati huu limeibuka kwa nguvu zaidi - timeline ya kuibuka kwa kundi hili ikoje? wameanza lini kuibuka na nguvu yao ni ipi? Na tunatumia indicator gani kupata uwiano wa nguvu wa makundi ktk taifa, au upendeleo pengine? Na ratio gani au sifa zipi zinaweza tumika objectively kujustify haki kati ya makundi mawili bila kudhibitiana/kufifishana?

Hili la CCM-natamani kuwaacha wenyewe, lakini je lina uhusiano na kilio cha msingi cha Polepole ?

Mengine ktk post yako naweza kubaliana na wewe tunapaswa kuyakemea nau kuyazuia kama jamii, ila nadhani tukiweza kubalina ktk hayo yanayo nitatiza hapo juu ni rahisi kuona uelekeo sahihi wa taifa.
 
Pamoja na mafanikio hayo makubwa, ile hali ya kundi fulani la kidini lililokuwa limefifishwa enzi za mwanzo, wakati huu limeibuka likiwa na nguvu zaidi; na limeweza kukichukua chama cha CCM na kukitumia kufikia malengo yaliyokuwa yamedhibitiwa huko mwanzo.

Je hili kundi la dini lilofifishwa enzi za mwanzo - huku kufifishwa tuna kujustify vipi ktk misingi ya haki? walififishwa kwa maslah ya taifa? au kwa maslah ya kundi lingine la dini? na haki itakuwa kwa kundi lipi wakati ule na sasa? Na vipi kama taifa tunaweza pata usawa wa makundi yote bila kufifishana? How do we get there objectively?

Wakati huu limeibuka kwa nguvu zaidi - timeline ya kuibuka kwa kundi hili ikoje? wameanza lini kuibuka na nguvu yao ni ipi? Na tunatumia indicator gani kupata uwiano wa nguvu wa makundi ktk taifa, au upendeleo pengine? Na ratio gani au sifa zipi zinaweza tumika objectively kujustify haki kati ya makundi mawili bila kudhibitiana/kufifishana?
Hapo mkuu 'Ajuae_26' hakuna utata wa aina yoyote kabisa; na ninakuelewa vizuri sana unakoibukia. Huu ni mjadala ambao kila mara huibuka ndani ya nchi hii kwa sababu unapewa uhai na kundi hilo hilo lililoshikilia uamini wa hayo unayo yaeleza wewe.
Nimetumia neno "kufifishwa" kwa maksudi; kwa sababu hili kundi halisimamii usawa wa waTanzania bali maslahi ya imani yake. Hili ni kundi aina ya makundi yaliyopo kila nchi palipo na imani mbalimbali; na hata ndani ya nchi za dini hiyo, huibuka kundi lenye ulalamishi na kutaka maslahi yao ndiyo yawekwe mbele.

Kama umekubaliana nami huko kwingine, bali ukashindwa kunielewa kwa hayo maneno niliyo andika hapo; basi mimi ninakutambua kuwa wewe ni mpigania kundi hilo na siyo maslahi ya Tanzania kama nchi ya watu wamoja, bila ya kupendelea kundi lolote kwa misingi ya imani/dini.
 
Mkuu Kalamu, shukran kwa majibu, japo umefupisha (narrow down ktk sehemu ndogo).

Licha majibu yako, bado nahisi naweza rudia swali lile lile au linalo fanana, na lengo langu ni kuondoa any form of biasness ktk hoja au tatizo husika, ndio maana swali langu la msingi ni kuwa tunapima vipi objectively mambo haya ili tupate usawa. Hisia na malalamiko ya upendeleo wa kundi fulani ktk nchi yetu si mageni, yapo kwa kila kundi (nakusudia kila kundi lina malalamiko yake kuhusu serikali au mtawala fulani), swali linakuja ni vipi tunaweza thibitisha uhalali wa malalamiko husika kuwa halali na si hisia? Kwa hio lengo langu ni kuvuka mtego wa hisia kwenda kwenya uhalali/uhalisia wa issue, kama tutaridhika kuna genuine issue ndio tukabaliane kuhusu hatua za kuchukua, na katika hilo ndio sababu ya mimi kusema nitakubaliana na andiko lako lote la awali provided tumeza jiridhisha juu tatizo halisi dhidi ya hisia za mtu au za jamii fulani. Maana hata zile nyakati/tawala ambazo zinaweza rejewa kama palikuwa na halki/usawa/uzalendo bado lazima kuna kundi/makundi lina/yana malalamiko.

Kuhusu kunitambua kama mtu wa kundi fulani, maoni yangu hili ndio msukumo wa swali langu la msingi, ni vipi tunavuka toka mboni za identity zetu kwenda ktk uhalisia/ukweli, ni wazi hata wewe una identity yako, na ni jambo la asili watu kuvutia au kulinda maslah yake/yao (ubinafsi ni tabia ya mwanadamu) na wakati mwingine tunaweza tusijitambue kama tunafanya upendeleo au ubaguzi, swali litakuwa ni viwango gani vya tabia hii ya mwanadamu vinaweza zingatiwa kama tatizo na viwango gani tunaweza kusema hizi ni hisia zinazo sukumwa na identity zetu? Na nadhani ili kufikia hapo objectivity inahitajika kama kizio.

Marejeo ya kundi fulani kuwa na shida hata ktk mataifa yao, ndio yapo mataifa yenye kundi moja kwa kiasi kikubwa na yana shida, ila nitapata shida kuona hilo laweza kuwa hoja ya mjadala huu (maoni yangu hilo laweza fanana na wazungu/watu weupe kwa ujumla wao wanavyo tudhihaki watu weusi kwa ujumla wetu bila kujali dini/matabaka zetu/yetu), na wakati huo huo wakiwa na mahaba zaidi na baadhi yetu.
 
Niongeze swali au hoja, tukimpata huyo mwenye uwezo, je tuna sababu ya kumbadili kwasababu tu amemaliza miaka 10 ? Au tuendelee nae tutumie vipawa na uwezo wake kujenga nchi?

Kablya kufika huko, pia tuna fursa ya kutafakari ktk historia na mazingira yanayo tuzunguka. Mwl alihudumu kwa miaka si chini ya 20 ktk ofisi, je linaweza saidia kutupa somo lolote?
Baadhi ya majirani zetu, wana marais wa wa dini moja toka mataifa yao yaundwe, je wanakwama wapi kupata mwenye uwezo? Au wao wamefanikiwa kupata mwenye uwezo?
Ukijibiwa maswali haya kwa kina kabisa, bila unafiki, najipiga 'bani' ya siku 9
 
Niongeze swali au hoja, tukimpata huyo mwenye uwezo, je tuna sababu ya kumbadili kwasababu tu amemaliza miaka 10 ? Au tuendelee nae tutumie vipawa na uwezo wake kujenga nchi?

Kablya kufika huko, pia tuna fursa ya kutafakari ktk historia na mazingira yanayo tuzunguka. Mwl alihudumu kwa miaka si chini ya 20 ktk ofisi, je linaweza saidia kutupa somo lolote?
Baadhi ya majirani zetu, wana marais wa wa dini moja toka mataifa yao yaundwe, je wanakwama wapi kupata mwenye uwezo? Au wao wamefanikiwa kupata mwenye uwezo?
Achana na mawazo ya kuutazama urais kwa kutumia angle ya dini. Utazame urais katika uwezo wa mtu. Tume huru ndio itakayofuta hayo mawazo ya kijinga, mawazo ya rais kuwa zamu ya dini fulani au zamu ya bara au visiwani. Tusipo pata tume huru kwa maana ya tume inayo jitegemea ukiachana na hii inayotegememea amri za TISS na wakuu wa wilaya, hayo ya kuhusisha urais na udini au upande wa Tanzania yatakoma. Nchi kama kenya, zambia na Malawi zenye tume huru kwa maana ya uhuru huo ujima walishaachana nao. Ukija na mgombea wako kwa minajili ya 'dini fulani zamu yetu' hata kama mgombea anaonekana ana uwezo wa mashaka, wananchi watakunyoosha kwenye box la kura.
 
Sina shida na tume huru, japo nadhani hii ni ndoto au mazigazi...maoni yangu hapo Kenya unapo sema sioni kama tume huru imekuwa suluhu ya kumpata rais bora, japo nadhani kwa kiasi fulani imewavusha ktk kupigana kutokana na uchaguzi na kuhamisha conflict ya uchaguzi kuwa jambo la term nzima ya urais/utawala fulani.
Pia niweke controversial point hapa, Tume huru VS TISS/CCM control, moja ya weakness kubwa ya tume huru kwa nchi zetu hizi magenge ya watu wenye fedha/external pressure kuweza kusimika Rais. Wakati moja ya mazuri ya TISS/CCM control kwa tume ya uchaguzi ni kuwa tunao uwezo na tumekuwa tukifanikiwa kuzuia threats hizo na hali hio ipo mpaka sasa. Nirudie hoja hii ni controversial, na naongeza tahadhari maneno ya Polepole kuhusu wahuni kusimika rais/viongozi bado kwangu ni dhana ya kubumba hasa kwakuwa wanajua vizuri mfumo wa nchi waliamua kuibua hisia za watu. And yes kama taifa tukijiridhisha kwa haki kabisa bila majungu na chuki kuwa CCM wameshindwa dhibiti watu wasio wasafi, tuna haja ya kufikiri upya tunakwenda vipi mbele.

Urais kwa uwezo wa mtu ndio maswali niliyo hoji hapo. Japo kulingana na andiko lako, unahisi urais kwa desturi kupokezana kati ya dini tofauti unapelekea kupata rais asie na sifa? Au huwa anatafutwa mwenye sifa toka dini fulani? Je upo uwezekano wa dini fulani kukosa kabisa watu wasio na sifa ya kuwa Rais? Linawezekana hilo? Kama desturi hio inazaa watu rais wasio na sifa twende ktk hilo kwa kina, mifano, na tukichunga hisia, na tujue tatizo lina anzia wapi?
 
Licha majibu yako, bado nahisi naweza rudia swali lile lile au linalo fanana, na lengo langu ni kuondoa any form of biasness ktk hoja au tatizo husika, ndio maana swali langu la msingi ni kuwa tunapima vipi objectively mambo haya ili tupate usawa. Hisia na malalamiko ya upendeleo wa kundi fulani ktk nchi yetu si mageni, yapo kwa kila kundi
Mimi nilisha kuelewa toka mwanzo unapo simamia; na ninajuwa wazi mjadala huu unakoulenga uelekee.

Jibu langu ni lile lile, sina la ziada ya hili; kwamba, sote wananchi ndani ya nchi hii ni kwanza kabisa kabla ya jambo jingine lolote ni "waTanzania"
Hii ndiyo sifa muhimu inayoniongoza mimi.

Hizo 'objectivity' unazoniuliza mimi zielekeze kwenye maslahi ya "u-Tanzania" wetu sote kwanza.

Unapojitengenezea kundi unalotaka liwe juu ya maslahi ya uTanzania wetu; hapo moja kwa moja nina tatizo nalo.

Sasa ukitaka niende kwenye hayo makundi kadhaa nianze kuainisha mahitaji ya kila kundi na kulipa uzito unaovuka mipaka ya uTanzania wetu; kamwe sina jibu lolote la maana kwako.
 
Hongera kwa andiko Pasko, Kweli hakuna palipo andikwa. Ila kwa mujibu wa CCM ki-vitendo na kwa maneno yao akiwemo Polepole na Bashiru kwa hivi karibuni, wamenukuliwa wakisema ccm ina mila na desturi, je hili laweza kuingia hapo?

Hoja ya kuwa bila utaratibu huo kuna dini isingepata rais mimi nadhani ktk siasa jambo hilo laweza kuwa si sahihi. Kwa kuanzie pengine tungejua kwanini Wazee waasisi waliona busara ya kuweka utaratibu huo (ni kipi kiliwasukuma), je ilikuwa ni favour kwa dini fulani? kurudisha shukran? kutambua ukweli wa hali ya kisiasa ya nchi? Pili tazama population ya nchi na distribution yake ktk mikoa, unaliona hilo kama factor? Uzoefu wa Nigeria ambapo huenda kuna demography yenye mfanano na Tz ukoje?
Hoja kubwa ni kuwa ukiwa na Tume huru kwa maana ya uhuru wa tume kusimama yenyewe hizo tamaduni au mawazo ya kupokezana kwa mujibu wa dini yataisha tu. Kura ya mwananchi itaamua nani awe Rais, kutoka upande wowote au chama chochote ilimradi huyo mtu akuwa na uwezo. Sasa hivi tunapata tabu kwa sababu kura ya mwananchi haithaminiwi kwenye box.
 
Dawa ni katiba mpya na tume huru ya uchaguzi tu.
Katiba iliyopo haina utaratibu huo.
Tatizo kuu la watanzania ni watu (baadhi ya watumishi wa serikali na vyombo vya dola) na siyo katiba na sheria (pamoja na mapungufu yake).
Hata kama kuna katiba mpya, kwa watu wenye fikra zile zile ni sawa na kuwapa nguruwe lulu, watakanyagakanyaga tu.
Muhimu kwa kuanzia ni kuwaelimisha na kuwawajibisha watumishi wa uma na vyombo vya dola wenye upendeleo wa vya make kinyume na katiba, kwani wao ndiyo maadui wa taifa na siyo wanasiasa.
Sasa hivi lawama zinaelekezwa kwa chama tawala na Rais aliye madarakani kwa sababu ya upuuzi wa wachache.
 
Mimi nilisha kuelewa toka mwanzo unapo simamia; na ninajuwa wazi mjadala huu unakoulenga uelekee.

Jibu langu ni lile lile, sina la ziada ya hili; kwamba, sote wananchi ndani ya nchi hii ni kwanza kabisa kabla ya jambo jingine lolote ni "waTanzania"
Hii ndiyo sifa muhimu inayoniongoza mimi.

Hizo 'objectivity' unazoniuliza mimi zielekeze kwenye maslahi ya "u-Tanzania" wetu sote kwanza.

Unapojitengenezea kundi unalotaka liwe juu ya maslahi ya uTanzania wetu; hapo moja kwa moja nina tatizo nalo.

Sasa ukitaka niende kwenye hayo makundi kadhaa nianze kuainisha mahitaji ya kila kundi na kulipa uzito unaovuka mipaka ya uTanzania wetu; kamwe sina jibu lolote la maana kwako.
Sawa Mkuu Kalamu, nadhani kusomana si tatizo na nadhani hata mimi nilikuelwa na kukusoma toka mwanzo, na sikuwa na lengo kupeleka mjadala ktk angle fulani kama ulivyoweka, bali nilitaka chokonoa mambo madogo lakini muhimu ktk mijadala kama hii, mfano ni vipi tunatenga hisia za jamii na ukweli wa tatizo husika?. Tunaweza kuwa objective ktk mambo haya? hasa katika malalamiko haya.

I do agree, U-Tanzania kwanza, mimi sina shida na hili, japo swali muhimu je mimi na wewe tunaliweza hilo? huenda wewe na mimi tukaweza, je watanzania wangapi wanaliweza hilo na kuishi nalo? Tunao uwezo wa kujenga jamii ya kuishi ktk misingi hio kwa ukweli kabisa?

Ni kweli si sahihi kuunda kundi lilo juu ya wengine, japo tafsiri ya umma/wananchi inaweza kuwa ngumu na isiyo tabirika, huku kiongozi akiwa na malengo mengine na changamoto nyingine za kiuongozi na akafanya maamuzi kwa kuzingatia hayo., wananchi wao kwa upande wao wanaweza tazama kigezo kimoja tu na kusimama nacho kumhukumu kiongozi wao.

Lakini pia ni muhimu kukumbushana ktk mambo haya ya kijamii na uongozi, ukisema unasimama na u-Tanzania tu au sifa tu za mtu husika ni kujidanganya, Na katika hili marejeo yangu ni Mwl Nyerere (na hili ni ktk hali chanya si hasi). Zipo nukuu alipinga baadhi ya viongozi wasipewe nafasi/cheo fulani kwasababu tu ya dini yake, kwa maana alisema ipo haja ya kuweka uwiano ktk uongozi ili kujenga umoja wa taifa. Kama utahitajia marejeo naweza tafuta nilete. Hivyo nakubali u-Tanzania kwanza, mwenye haki yake apewe, lakini hatupaswi kupuuza mambo ya matabaka yetu, kwasababu wapo watu ktk tabaka zote wanajali hilo, na hata wasipo jali wewe kiongozi ukipuuza au kubagua utawapa maswali wafuasi wako.
 
Back
Top Bottom