Nakubaliana na kukataa pia. Tanzania hatuna watu wabovu kwa maana ya uwezo wao akili na kutenda, hili sioni tatizo. Ila naona tatizo/ubovu ktk wa-Tanzania wanataka nini? wanataka kwenda wapi? Wanasimamia nini? Uniwie radhi na watu wanie radhi si kwa maana ya kutweza watu, lakini lile jambo na tabia ya unafiki kwa wa-Tanzania ni moja ya ubovu wetu unao tugharimu sana.
Nakubali Nyerere aliweza shawishi watu, na nadhani wengi wa Wa-Tanzania walikuwa tayari na wali-msikiliza na kumfuata. Ila
Nakubaliana na kukataa pia. Tanzania hatuna watu wabovu kwa maana ya uwezo wao akili na kutenda, hili sioni tatizo. Ila naona tatizo/ubovu ktk wa-Tanzania wanataka nini? wanataka kwenda wapi? Wanasimamia nini? Uniwie radhi na watu wanie radhi si kwa maana ya kutweza watu, lakini lile jambo na tabia ya unafiki kwa wa-Tanzania ni moja ya ubovu wetu unao tugharimu sana.
Nakubali Nyerere aliweza shawishi watu, na nadhani wengi wa Wa-Tanzania walikuwa tayari na wali-msikiliza na kumfuata. Ila sioni hilo kwa Hayati JPM, japo niko tayari kukubali tofauti zetu ktk hili.
sioni hilo kwa Hayati JPM, japo niko tayari kukubali tofauti zetu ktk hili.
Umekosa tu kuwekea maanani maneno niliyotumia katika kuwaweka pamoja Mwalimu Nyerere na Magufuli kwa utofauti wao juu ya kuwavuta waTanzania waelewe uongozi wao ulicho kilenga..
Magufuli njia zake zilikuwa za maguvu mengi kuliko ushawishi. WaTanzania walielewa alilenga nini kipatikane katika uongozi wake, ambacho watu walikiona kuwa cha manufaa kwa taifa zima. Njia zake za kufikia huko zilikuwa za maguvu, na hazikutumia taraibu zinazoeleweka, lakini watu walijuwa ni kwa manufaa yao.
Kwa mfano:
Utendaji kazi maofisini; kusimamia raslimali za nchi hii ziwainue wananchi zaidi; kupambana na rushwa; ile hali tu ya kumfanya mTanzania ajiamini kuwa tunaweza kufanya mambo mengi sisi wenyewe hapa bila ya utegemezi ili kusukuma mbele maendeleo yetu;, ni mtu gani huyo asiyeona faraja ya taifa letu kuwa na ujiamini kama huo!
Hatukona maamuzi na mambo mazito yakifanyika ndani ya miaka mitano? Rufiji, Barabara, meli, SGR, kuhamia Dodoma,,n.k. Haya mambo huoni yakimtofautisha sana na hawa wengine, licha ya ushetani wake na kupenda kusifiwa sana?
.... Ni mTanzania gani ambaye hakuziona juhudi hizi na kuzipenda; hata kama kuna mambo mengi mabaya ambayo hakuyapenda yaliyofanywa na kiongozi huyo!
Sasa angalia, hata maswala madogo ya kutunza mapori yetu kwa biashara ya ukaa, waTanzania wanaambiwa hawana uwezo! Tunaandaliwa tu kuwa watwana wa watu wenye uwezo; hii ndiyo Tanzania tunayoitaka kweli?
Haya yote yanatokana na uongozi. Kama kiongozi hana dira ya kujuwa ni wapi taifa lake linahitaji kuelekea, ni wazi wananchi wataswagwa tu na kuelekea huko anakotaka yeye; na hasa kama hata muundo wa elimu yenyewe umetengenezwa kuwalaza akili wananchi.
Ndiyo maana elimu yetu ya mwanzo baada ya kupata uhuru iliwekea mkazo katika kumfumbua mTanzania akili kujuwa mwelekeo wa dunia unakokwenda. Sasa tunajipigia tu, bila ya lengo lolote maalum..
Na mbaya zaidi tunazidi kuchanganywa akili tuvurugane sisi wenyewe ndani ya nchi yetu, ili tutawaliwe kirahisi zaidi.
Usifikiri Somalia, Sudan. au hata DRC zipo mbali sana na sisi.