Pendekezo, naona umetumia neno ushetani dhidi ya Hayati JPM, ikikupendeza usitumie maneno hayo kwasababu ya nafasi yake kama kiongozi wetu, lakini pia ni marehemu. Kama alikuwa shetani au na ushetani, je na sisi ni nani, shetani pia?Umekosa tu kuwekea maanani maneno niliyotumia katika kuwaweka pamoja Mwalimu Nyerere na Magufuli kwa utofauti wao juu ya kuwavuta waTanzania waelewe uongozi wao ulicho kilenga..
Magufuli njia zake zilikuwa za maguvu mengi kuliko ushawishi. WaTanzania walielewa alilenga nini kipatikane katika uongozi wake, ambacho watu walikiona kuwa cha manufaa kwa taifa zima. Njia zake za kufikia huko zilikuwa za maguvu, na hazikutumia taraibu zinazoeleweka, lakini watu walijuwa ni kwa manufaa yao.
Kwa mfano:
Utendaji kazi maofisini; kusimamia raslimali za nchi hii ziwainue wananchi zaidi; kupambana na rushwa; ile hali tu ya kumfanya mTanzania ajiamini kuwa tunaweza kufanya mambo mengi sisi wenyewe hapa bila ya utegemezi ili kusukuma mbele maendeleo yetu;, ni mtu gani huyo asiyeona faraja ya taifa letu kuwa na ujiamini kama huo!
Hatukona maamuzi na mambo mazito yakifanyika ndani ya miaka mitano? Rufiji, Barabara, meli, SGR, kuhamia Dodoma,,n.k. Haya mambo huoni yakimtofautisha sana na hawa wengine, licha ya ushetani wake na kupenda kusifiwa sana?
.... Ni mTanzania gani ambaye hakuziona juhudi hizi na kuzipenda; hata kama kuna mambo mengi mabaya ambayo hakuyapenda yaliyofanywa na kiongozi huyo!
Sasa angalia, hata maswala madogo ya kutunza mapori yetu kwa biashara ya ukaa, waTanzania wanaambiwa hawana uwezo! Tunaandaliwa tu kuwa watwana wa watu wenye uwezo; hii ndiyo Tanzania tunayoitaka kweli?
Haya yote yanatokana na uongozi. Kama kiongozi hana dira ya kujuwa ni wapi taifa lake linahitaji kuelekea, ni wazi wananchi wataswagwa tu na kuelekea huko anakotaka yeye; na hasa kama hata muundo wa elimu yenyewe umetengenezwa kuwalaza akili wananchi.
Ndiyo maana elimu yetu ya mwanzo baada ya kupata uhuru iliwekea mkazo katika kumfumbua mTanzania akili kujuwa mwelekeo wa dunia unakokwenda. Sasa tunajipigia tu, bila ya lengo lolote maalum..
Na mbaya zaidi tunazidi kuchanganywa akili tuvurugane sisi wenyewe ndani ya nchi yetu, ili tutawaliwe kirahisi zaidi.
Usifikiri Somalia, Sudan. au hata DRC zipo mbali sana na sisi.
Ni vyema umeweka ufafanuzi huu, Ni kweli nakubaliana nawe ktk utawala wa JPM watu walielewa au walijua rais anataka fanya nini, hili sipingi, na ni kweli JPM alifanya maamuzi magumu kwa mradi kama wa Rufiji na kuhamia Dodoma. Na ukweli alitumia nguvu kupitiliza. Swali muhimu la kuunga mambo yote mawili ni je kuna mahusiano kati ya watu kuelewa Rais anataka nini na matumizi ya nguvu? Kama nimeelewa post yako, ni kuwa mahusiano hayo yapo, na mimi nakubaliana na wewe ktk hilo. Lakini uelewa huo umekuja kwa gharama ya watu kuzibwa midomo ya kukosoa au kushauri pengine, maana ni wazi ukirihusu hilo watu hawawezi kukuelewa, hivyo hapa ndio panajengeka hali ya Mtawala ndio mkweli na mwenye ukweli, na always yuko sahihi. Je ndio uongozi tunao taka? Na ni kweli viongozi wengine wanashindwa tumia hizo nguvu na mabavu kuhakikisha wananchi wanaelewa yeye anataka fanya nini? Au wameona njia hio sahihi, kwa maana ni vyema kuruhusu watu waseme wanavyo jisikia? Maoni yangu hawa wengine hawakuona umuhimu wa hilo, kwasabau vinginevyo uwezo wa na vyombo vya kudhibiti watu vipi chini ya mamlaka yao wangeweza toa maelekezo hayo.
Sina pingamizi na utendaji na usimamizi wa utendaji makazini, hii ilikuwa sifa kwake, japo toka akiwa hai na mpaka sasa nilitamani angeliwekeza nguvu kuyafanya yale yawe ni ktk mifumo rasmi na si kwasababu ya kivuli chake.
Rasilimali za nchi, mimi imani yangu nchi na viongozi/CCM wapo ktk mtanziko, hatujui sisi ni wajamaa au wabepari, ukiwatazama wengi wetu ni kama tunapenda ujamaa (uhafidhina wa rasimali zetu). Lakini kwa maoni yangu jambo hilo ni kama tumekwama na halitikelezeki na pengine halina uhalisia ktk dunia ya sasa (kwa ufupi yaliyo jiri ktk utawala wa Nyerere na JPM ktk eneo hili yanatoa majibu njia hii bado hatujaiweza, na nahisi hatutaweza hasa kwa kuzingati jinsi dunia inavyo kwenda). Hivyo binafsi, naamini njia sahihi ni uwekezaji (naona ipo siku tunaweza pata kiongozi sahihi wa kujenga msingi ktk hili) lakini njia hii nayo tulishindwa na bado pengine inahitajia maboresho zaidi. Tulishindwa ktk uwekezaji kwa mapungufu yalitokea ktk awamu ya Mzee Mkapa kama alivyo jieleza mwenyewe maana nadhani jambo hili ni kama lilishika hatamu chini ya utawala wake. Na bado tunashindwa ktk njia hii kaswababu bado wengi wetu tunaona mikataba tunayo ingia ingeweza kuwa bora zaidi ili kuongeza faida ktk upande wetu.
Ama baadhi ya mafanikio uliyotaja, mimi naona hayo yapo kwa viongozi wengine pia..japo tunaweza tofautina pia ktk hili.
Hio biashara ya ukaa sijui kama nakuelewa, labda ufafanue zaidi hasa ni vipi wa-Tanzania wanaambiwa hawa uwezo.
Napata shida kuhusu dira, na hapa pananirudisha ktk lile jambo la wa-tanzania tunataka nini? Kwa uelewa wangu maoni mengi ya hivi karibuni na ya muda mrefu ni kuwa watu wanataka nchi iwe na dira kisha viongozi waje kutimiza dira hio. Hayati Mzee Mkapa alilia sana na hili akitumia maneno muendelezo kati ya awamu na awamu, Juzijuzi wakaibuka kina Askofu Gwajima wakitaka tumia dira kama karata ya kisiasa. Sasa tujikite kwa lipi kutafuta mwenye dira? au mwenye uwezo wa kutekeleza dira? Kuna mengi nafikri ktk hili la dira ila niishie hapo pengine.
Tujinenee na kuwaza mema, tuzungumze kasoro zetu na kutafuta suluhu. Hatuna sababu ya kuwaza mabaya.