Unanipoteza. Ulisema nikupe mfano mmoja tu wa mashambulizi ya anga kabla ya hiyo dec. 2015 ulikuwa una uhakika kuwa hakuna mashambulizi kwa kuwa bunge lilizuia 2013. Nimekupa huo mfano unaleta sarakasi nyingine.
Hiyo maana yako ya covert operation na direct military intervention ina mapungufu pia kwa sababu zifuatazo,
1) serikali ya Uingereza haihitaji kura za wabunge ili kufanya shambulio lolote la kijeshi.
2) hata inapotokea wabunge wakapiga kura ya hapana bado serikali inaweza kufanya shambulio la kijeshi sababu serikali haifungwi na kura za wabunge.
3) bunge liliporuhusu mashambulizi syria dec. 2015 haina maana kuwa hiyo ruhusa ni endelevu kwa kila shambulizi.
How the recent strikes on Syria undermine UK constitutional controls on military action - The Law of Nations
Inaelezea ukomo wa nguvu za bunge kwa jeshi, wameelezea kuanzia 2013.
Syria action – UK government legal position
Taarifa rasmi ya serikali ikielezea uhalali wa mashambulizi yaliyofanyika 2018. ruhusa ya bunge ya dec. 2015 haijarejewa kwenye hii taarifa badala yake wametumia sheria za kimataifa kujustify hilo shambulizi.
britain approves airstrikes in syria Jeremy Corbyn akilalamika bunge kutotaarifiwa.
Nilikuomba unipe mfano mmoja tu wa "operation ya wazi" ya mashambulizi ya anga ya Uingereza nchini Syria kabla ya approval ya bunge 2015, mpaka sasa haujaleta hapa, badala yake, umeleta covert operation. Ni nani anayeleta sarakasi hapo?
Hakuna mahali niliposema kuwa serikali ya Uingereza haijawahi kufanya shambulizi lolote la kijeshi bila ridhaa ya bunge. Kwanza hakuna sheria inayoizuia serikali kufanya hivyo. Ila, shambulizi ni pale tu ambapo kutakuwa na justification ya kufanya hivyo kulingana na sheria ya kimataifa.
Nilisema, kilichokuwa kikifanyika Syria kabla ya approval ya bunge 2015, kilikuwa ni covert operations ambazo huwa hazina[ga] hata uhitaji wa ku-deploy majeshi ya nchi kwa maana ya military intervention. Ni operations za serikali ambazo ni za siri. Taarifa zimekuja kuletwa baadaye! Na nilishukuru sana pale ulipoleta ile taarifa ambayo imeonesha mfano wa covert operation.
Nafahamu kuna mjadala mkubwa kuhusu mamlaka ya bunge kuhusiana na masuala ya kijeshi, lakini huo ni mjadala ambao hauendani na siasa na uhusika wa Uingereza katika mgogoro wa Syria katika uhalisia wake.
Katika issue ya military intervention nchini Syria, bunge la Uingereza limekuwa likifanya debate na kuamua kwa kura kuhusiana na masuala ambayo tumekuwa tukijadili hapa. Huo ndio uhalisia wa mambo! Hivi ndivyo ambavyo siasa za Uingereza zimekuwa zikifanyika hususani katika kipindi cha mgogoro wa Syria.
Hii hapa ni ripoti ya operations za Iraq pamoja na Syria ya hadi mwezi Machi, 2017:
An update on the military campaign in Iraq and Syria is available in CBP8011, Syria and Iraq: update June 2017. This document will no longer be updated but serves as a useful summary of the military campaign against ISIS to March 2017.
commonslibrary.parliament.uk
Katika hiyo ripoti kuna mahali panasema hivi, nanukuu:
"On 30 September 2014 Tornado aircraft carried out their first airstrikes on ISIS targets in Iraq (Operation Shader). RAF Tornado aircraft conducted the first offensive operation in Syria on 3 December 2015. RAF aircraft had, however, been conducting non-offensive surveillance operations over Syria since 21 October 2014."
Mwisho wa kunukuu.
Zingatia sana hapo panaposema: "first offensive operation".
Ni hivi! Baada ya lile azimio la Cameron la 2013 la kutaka Uingereza kupeleka majeshi Syria kushindikana bungeni, serikali ilisema wazi kuwa itayaheshimu maamuzi ya bunge.
Ndio maana hatukusikia deployment yoyote ile ya majeshi ya Uingereza nchini Syria ukiachana na hizo covert operations. Deployment ya kwanza ilifanyika mwaka 2015 baada ya kupigiwa kura bungeni. Muda mchache baadaye, tulianza kuona majeshi yakipelekwa Syria kwenda kupiga mabomu.
Pia, pitia taarifa hii:
MoD confirms that jets carried out ‘first offensive operation over Syria and have conducted strikes’ hours after MPs voted in favour of military action
www.theguardian.com
Narudia! Mashambulizi ya kwanza kabisa ya majeshi ya Uingereza dhidi ya ISIL ama ISIS nchini Syria ni baada ya approval ya bunge mwezi Disemba mwaka 2015. Nilikuomba ulete ushahidi wa shambulizi moja tu la wazi la Uingereza nchini Syria dhidi ya ISIL kabla ya approval ya bunge mwaka 2015. Kwa kifupi tu, hakuna!