Richard spencer
JF-Expert Member
- Feb 22, 2021
- 1,225
- 1,993
Nilikuomba unipe mfano mmoja tu wa "operation ya wazi" ya mashambulizi ya anga ya Uingereza nchini Syria kabla ya approval ya bunge 2015, mpaka sasa haujaleta hapa, badala yake, umeleta covert operation. Ni nani anayeleta sarakasi hapo?
Hakuna mahali niliposema kuwa serikali ya Uingereza haijawahi kufanya shambulizi lolote la kijeshi bila ridhaa ya bunge. Kwanza hakuna sheria inayoizuia serikali kufanya hivyo. Ila, shambulizi ni pale tu ambapo kutakuwa na justification ya kufanya hivyo kulingana na sheria ya kimataifa.
Nilisema, kilichokuwa kikifanyika Syria kabla ya approval ya bunge 2015, kilikuwa ni covert operations ambazo huwa hazina[ga] hata uhitaji wa ku-deploy majeshi ya nchi kwa maana ya military intervention. Ni operations za serikali ambazo ni za siri. Taarifa zimekuja kuletwa baadaye! Na nilishukuru sana pale ulipoleta ile taarifa ambayo imeonesha mfano wa covert operation.
Nafahamu kuna mjadala mkubwa kuhusu mamlaka ya bunge kuhusiana na masuala ya kijeshi, lakini huo ni mjadala ambao hauendani na siasa na uhusika wa Uingereza katika mgogoro wa Syria katika uhalisia wake.
Katika issue ya military intervention nchini Syria, bunge la Uingereza limekuwa likifanya debate na kuamua kwa kura kuhusiana na masuala ambayo tumekuwa tukijadili hapa. Huo ndio uhalisia wa mambo! Hivi ndivyo ambavyo siasa za Uingereza zimekuwa zikifanyika hususani katika kipindi cha mgogoro wa Syria.
Hii hapa ni ripoti ya operations za Iraq pamoja na Syria ya hadi mwezi Machi, 2017:
![]()
ISIS/Daesh: the military response in Iraq and Syria - House of Commons Library
An update on the military campaign in Iraq and Syria is available in CBP8011, Syria and Iraq: update June 2017. This document will no longer be updated but serves as a useful summary of the military campaign against ISIS to March 2017.commonslibrary.parliament.uk
Katika hiyo ripoti kuna mahali panasema hivi, nanukuu:
"On 30 September 2014 Tornado aircraft carried out their first airstrikes on ISIS targets in Iraq (Operation Shader). RAF Tornado aircraft conducted the first offensive operation in Syria on 3 December 2015. RAF aircraft had, however, been conducting non-offensive surveillance operations over Syria since 21 October 2014."
Mwisho wa kunukuu.
Zingatia sana hapo panaposema: "first offensive operation".
Ni hivi! Baada ya lile azimio la Cameron la 2013 la kutaka Uingereza kupeleka majeshi Syria kushindikana bungeni, serikali ilisema wazi kuwa itayaheshimu maamuzi ya bunge.
Ndio maana hatukusikia deployment yoyote ile ya majeshi ya Uingereza nchini Syria ukiachana na hizo covert operations. Deployment ya kwanza ilifanyika mwaka 2015 baada ya kupigiwa kura bungeni. Muda mchache baadaye, tulianza kuona majeshi yakipelekwa Syria kwenda kupiga mabomu.
Pia, pitia taarifa hii:
![]()
Britain carries out first Syria airstrikes after MPs approve action against Isis
MoD confirms that jets carried out ‘first offensive operation over Syria and have conducted strikes’ hours after MPs voted in favour of military actionwww.theguardian.com
Narudia! Mashambulizi ya kwanza kabisa ya majeshi ya Uingereza dhidi ya ISIL ama ISIS nchini Syria ni baada ya approval ya bunge mwezi Disemba mwaka 2015. Nilikuomba ulete ushahidi wa shambulizi moja tu la wazi la Uingereza nchini Syria dhidi ya ISIL kabla ya approval ya bunge mwaka 2015. Kwa kifupi tu, hakuna!
Jibu lako linaonesha hujasoma chochote kwenye hizo links nilizokupa sababu ungesoma usingerudia kuleta hiyo habari ya guardian ambayo pia imeelezewa tayari.
Pia Unajichanganya mno, kama ulikuwa unajua hakuna sheria inayozuia serikali kufanya mashambulizi kwanini ulisema baada ya december 2015 mashambulizi yote ni direct military intervention kwa kuwa bunge lina taarifa? Ok tufanye hukusema au kumaanisha hivyo sasa kuna utofauti gani wa hilo shambulizi lililofanyika 2018 na hayo yaliyofanyika kabla ya dec. 2015.
Unasema hili la 2018 walitoa justification ya shambulizi kwani yaliyokuwa yanafanyika kabla ya dec. 2015 kulikuwa hakuna justification?. Au hata hili lililofanyika muda mfupi baada ya bunge kuidhinisha mashambulizi, hiyo idhini siyo sehemu ya sababu kuhalalisha shambulizi.
Kwenye link ya kwanza umequote sehemu wanasema hiyo dec. 3 2015 ni first offensive operation lakini unachosahau ni kwamba kinachozungumziwa hapo ni ndege hiyo ya Raf tornardo. Lakini pia tuseme wanamaanisha jeshi la uingereza hiyo ndio first offensive operation yao na kilichokuwa kabla ya hapo ni defensive operations, je hii inabadilisha nini juu ya ushiriki wa jeshi la Uingereza nchini Syria.
Nitafupisha maelezo ya kilichomo kwenye Link ya kwanza maelezo yapo wazi kuwa Cameroon hakuwa na ulazima wa kulisikiliza bunge kwenye maamuzi ya kura zilizopigwa 2013 alichofanya yeye ni kuamua kuheshimu tu mawazo ya bunge ila sheria haimlazimishi afate maamuzi ya bunge. Theresa May kwa kutambua hiyo sheria ndomaana hakuangaika na mambo ya bunge.
Ile idhini ya dec. 2015 sio sheria kuwa inahalalalisha kila shambulizi, ilikuwa halali kwenye lile shambulizi walilolifanya muda mfupi baada ya kupiga kura basi.
Soma kwanza hizo links, ni taarifa rasmi na zinaeleza sheria za uingereza kuhusu hayo mambo ya kijeshi. Wameelezea kuanzia Iraq hadi kikao cha bunge mwaka 2013, 2015 na tukio la 2018.