Urusi kuwa na mji wa Bakhmut na Soledar, hasara ni kubwa kuliko faida


Wachangiaji na Pro Russia wengi wanashindwa kuelewa dhana hii kuhusu NATO na ushiriki wa nchi zilizojiunga NATO kuisaidia Ukraine.

NATO ni entity inayojitegema na ina resources zake (Financing, Military equipment na Human resources). Inachangiwa financing na wanachama wake tu. Inanunua vifaa vya kivita kwa mahitaji yake kwa technology inayoitaka kwa mazingira ua wakati husika. Siyo kwamba inapewa donation ya silaha kama nchi zinavyofanya kwa Ukraine la hasha.

Watu wengi wanafikiri USA, German, UK and allies kuisaidia kifedha, kujenga uwezo na vifaa vya kivita Ukraine kuwa ndo NATO anapigana na Russia. Hakuna kitu Russia anachokiogopa kama akiingia battle direct na NATO, hiyo mistake Russia hatakuja aifanye maana anajua hatachukia round. Russia anajua High precision equipment with high technology millitary equipments anazotumia NATO. Hakuna military equipment ambayo NATO anazitumie zimeenda Ukraine. Hata USA, German vifaa anavyotoa vina technology ya chini kuliko anavyotumia NATO.

Ushiriki wa NATO ni kutoa wataalam wa kuwafundisha Wanajeshi wa Ukraine kwenye vifaa vinavyotolewa kwa Ukraine maana yeye NATO amevitumia sana siku za nyuma ana uzoefu mkubwa sana kuhusu hivo vifaa. Pia kuwapa military tactical. Lakini siyo kwamba NATO anapeleka majeshi yake au vifaa vyake kwa Ukraine.
 
Hapo kwenye SQM uko sahihi kweli!!!?? Yaani mji uwe na SQM 53!!!???
Kama unaona takwimu haiko sawa tupe ya kwako ili watu walinganishe. Hoja hujibiwa kwa hoja siyo porojo. wewe unaona ni issue ya typo error ndogo hivo ya SQM badala ya SQKM.

Mimi nimetoa takwimu ya Bakhmut na Soledar zina ukubwa kiasi gani. Jumla ni 53.9SQKM
 
Nashukuru kwa maoni na mtazamo wako. Ila kwenye hoja #3 imenipa ukakasi sana. Ngoja niulize maswali haya unipe majibu.

"Umesema kwamba lengo la Russia siyo kukalia maeneo ya Ukraine bali kuondoa silaha zote za NATO na kuifanya Ukraine isijiunge na NATO"

1. Russia alipoikalia kwa mabavu Crimea ambayo ni mkoa wa Ukraine tangu 2014 mpaka sasa ameondoa silaha zipi za NATO?

2. Unataka kutuaminisha kuwa Russia kuivamia Ukraine ni njia ya kuondoa silaha za NATO. Je, Ukraine kuna ghala au store ya silaha za NATO. ?

3. NATO ana military base Ukraine?

4. Russia anawezaje kuondoa silaha za NATO ambazo ziko kwenye Military base zake mbali mbali ikiwemo base ya Romania. Kwa nini hajaivamia Romania ambaye ni mwanachama wa NATO na kuna military base ya NATO pale?

5. Russia ana uwezo wa kuizuia Ukraine isijiunge EU au NATO?

6. Kama lengo la Russia siyo kukalia maeneo ya NATO mbona Crimea kaikalia kwa ubabe.
 
Majibu yangu kuhusu maelezo yako ya #1 &2.

1. Hoja yangu ni kwamba Bakhmut ni Military strategic position na Russia kaichukua. Je, ni kweli ataweza kusonga mbele kwenda kwenye miji mingine niliyoitaja kama lengo kuu la kuikamata Bakhmut.

2. Kama counter attack iliyofanywa na Ukraine kuanzia tarehe 09 - 15/05/2023 imeleta mafanikio makubwa kwa Ukraine kuchukua eneo kubwa alilokuwa amelishikiria Russia tangu January 2022 kwa lengo la kukata logistic supply ya Russia. Je, counter offensive inayosubiliwa kwa hamu ikianza ataweza kumudu kuendelea kuikalia Bakhmut na Soledar?
 
Ufutwe tu, hauna hadhi ya kubaki jf...kama mtoa mada kashindwa kutofautisha sqm na sqkm kuna haja gani ga kubaki na uzi wa ovyo namna hii!!??
Ufutwe kwa sababu huna hoja au unataka kusikia kuwa Russia ni super power anayeichakaza USA na NATO?

Ulipozimulia itakuwa ni ile gongo ya mwanzoni.
 
.
 
Mkuu jaribu kufuatilia page ya YouTube ya mtu anaitwa Alexander Mercouris, ni pro-Russia lakini ana habari za uhakika sana hizi MSM zote naona kama hawamfikii.
Leo nilikua naangalia, alisema counter offensive yoyote ya Ukraine Bakhmut, itashindwa vibaya sana na itawaachia Ukraine majeraha ambayo hawataweza kuyatibu.

Sent from my SM-A135F using JamiiForums mobile app
 
Boss No buddy knows ni ipi hasa aim ya Russia kufanya hii anayoita Special Ops ... Ingawa wana aminisha ulimwengu juu ya hizo sababu zao but maswali unayouliza hakuna mtu atakaeweza kukujibu directly isipokuwa Uongozi wa Russia pekee na hii ni Kwasabab naamini wao wanataka tusikie tunachotaka kusikia na kuamini pia bt kwa mtazamo wangu naona kuna zaidi ya hizo sababu zao ingawa czijui ni zipi hasa
 
Unaulizwa maswali. Tunategemea ujibu badala yake unakuja na porojo. Kama huna hoja bora ukae kimya kuliko kuanika hadharani uwezo wa uelewa wako ulivyo na ukomo wa fikra zako
 
Tayari umeshasema ni Pro Russia (Propagandist) then unategemea output ipi?. Unaweza kupata embe kwenye mti wa mpera?

What facts he laid down?
 
Unaulizwa maswali. Tunategemea ujibu badala yake unakuja na porojo. Kama huna hoja bora ukae kimya kuliko kuanika hadharani uwezo wa uelewa wako ulivyo na ukomo wa fikra zako
😆🤣
 
Maswali nayouliza yana very simple logic.
1. kupima uelewa (understanding) na level of thinking ya mhusika.
2. Kuweza kutenganisha porojo na facts. Porojo na facts ni kama maji na mafuta. Ndiyo màana wanashindwa kujibu hoja na akijibu unaona anaelea kama mafuta.
 
Ni mapema sana kusema kuwa Ukraine ataizunguka Bakhmut sijaziona hizo dalili zaidi ya propaganda.

Labda naye anaweza ikamchukua miezi kadhaa kuizunguka Bakhmut kama muda aliochukua Urusi. Counter offensive ikianza itatupa majibu
Dalili utazionaje nawe upo Chole, Kisarawe ndani ndani?
Tuachage ujuaji wa kibongo
 
Madam umekiri kuondoka kwa bakhmut na soledar basi tulia uchumi wa urusi watu waliudharau tangu zamani tu lakin wanaona aibu leo wao kwahiyo na wewe huna tofauti na wao ambao wanapenda kufanya propaganda mwisho wanaumbuka jengine ukileta idadi ya warusi wanaokufa bila kuleta na wa ukraine ni sawa na uzombi tu maana utakua umelinganisha wapi ili kupata idadi iliyo pungua zaidi
 
Boss hapo hamna facts isipokuwa kama utakuwa neutral lakin kama upo biased na sehemu moja hata wew ukipewa fact za upande wa pili hauwez kukubali so kwa nikuonavyo wew upo tayar biased hivyo hata understanding level yako usha i-limit tayar
 
Dalili utazionaje nawe upo Chole, Kisarawe ndani ndani?
Tuachage ujuaji wa kibongo
Kwa hiyo unafikiri watu wote wako Chole au Buza. Pole sana. Usichokijua ni kama usiku wa giza.

Muhimu endelea kuelimika kuhusu hii vita. Nimeona watu wengi ni ushabiki umewajaa badala ya kujawa na facts. Propaganda ndo zina drive watu kuliko facts.

1. Mfano mdogo ni kwamba jana Ukraine walikanusa kuwa Bakhmut haiko under full control ya Russia. Hizo ni propaganda, lakini ukweli Bakhmut city kwa 100% iko under control ya Russia.

2. Mfano mwingine. Russia walipiga propaganda kuwa wameziteketeza HIMARS, lakini hawajawahi kujeruhi hata HIMARS moja. Majuzi wakaja na propaganda na ili trend sana kwa pro Russia kuwa wame destroy Patriot. Lakini ukweli Machine ilikuwa inafanya kazi na Russia walijaribu kujiridhisha kwa kutuma missile zingine zikawa intercepted. USA wako very transparent sana hawafichi ukweli. Waliposema kuwa ni very minor damage na kwamba system bado inafanya kazi.

3. Kuna watu walianza kupiga porojo kuwa eti uchumi wa Russia umepanda kuliko hata baada ya vita. Lakini Putin akawaumbua kwa kusema kuwa Uchumi umeshuka na akataja sababu ni vita na vikwazo ambayo Russia imewekewa na West. Hata kama Putin asingesema hadharani kwa logic ndogo tu huwezi kusema eti uchumi wa Russia umepanda. This is Ridiculous!!!. Labda kwa mtu ambaye hajaenda shule ndo ataamini hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…