Urusi kuwa na mji wa Bakhmut na Soledar, hasara ni kubwa kuliko faida

Kushinda vita ingekuwa ni rahisi kama hii kauli yako, Urusi ingekuwa aliishaikamata Ukraine ndanibya masaa 72 kama alivyotamka Putin.
Unaweza kutuwekea hapa kauli ya Rais Putin kuwa atamaliza SMO ndani ya masaa 72
 
Hii ndo aina ya watu tulionao. Na yeye hapo alipo anajiona katoa bonge la analysis ya hii vita.

Kwa hiyo baada ya Kuchukuliwa Soledar na Bakhmut vikapandisha uchumi wa Russia. Ama kweli vichwa vingi vimebeba urojo tu.
 
Hii ndo aina ya watu tulionao. Na yeye hapo alipo anajiona katoa bonge la analysis ya hii vita.

Kwa hiyo baada ya Kuchukuliwa Soledar na Bakhmut vikapandisha uchumi wa Russia. Ama kweli vichwa vingi vimebeba urojo tu.
Ona ulivyo kiazi ndio maana mnaitwa wapumbavu onesha sehemu nimesema kua urus kachuku bakhmut sasa uchumi wake umepanda?
Ukishindwa jipige kifuani jiite wew ni kiazi
 
Unaweza kutuwekea hapa kauli ya Rais Putin kuwa atamaliza SMO ndani ya masaa 72
Usiwe mvivu. Putin haongei kiswahili au English hata ukipewa usikilize hotuba yake hutaambulia kitu. Kama unakijua Ki Russia sikiliza hotuba yake ya kutangaza SMO. Tafuta mtu anayejua kirusi akutafasirie. Ndiyo maana kazi ya media ni kukuletea taarifa kwa lugha unayoijua
 
Ulijificha kwenye uchambuzi usio na upande lakini naona umeshindwa kudumu kwa muda mrefu umerudi kwenye rangi yako.Tulikujua tangu zamani...
Unaposema Russia kapeleka resources nyingi unatumia criteria gani mpaka kufikia hitimisho hilo,Kama upande wa personal Ukraine ndo amefanya rotation ya reserve nyingi ya wanajeshi hapo Bukhamut kuliko Russia.
Kwa upande wa Urusi walioshiriki hapo kwa kiasi kikubwa ni Musician pmc na Russia regular army walikuwa kwenye atelar na aviation tu.
2: kama hoja ni vifaa nadhani unajua nani ambaye analilia vifaa kila kukicha.Hivi unajua kwanini kumeitwa meat grinder.
 
[emoji1019][emoji1019][emoji1019][emoji1019]
 
Sasa kama hakuna anayejua wewe mwenzetu umejua Je kama alitangaza atamaliza vita ndani ya masaa 72.
Kila mmoja kwa wakati wake alipata kuiona ile hotuba ya Putin wkt anatangaza kuanza kwa SMO na aliweka malengo ya hii operation nini.Katika malengo hakuna sehemu alisema ana mpango wa kuitwaa kiev au kuikalia Ukraine kama unakataa leta kauli yake hapa.
Uzuri ile hotuba ili tafsiriwa kwa ki ingereza
 
1. Malengo ya SMO yalikuwa yapi. ? Na yalikuwa yakamilike lini? Tutajie.

2. Kama hakuwa na malengo ya kuitwaa Kiev majeshi yake yalienda Kiev kufanya nini?

3. Kwa nini mpaka leo wanahangaika kurusha missile Kwenda Kiev?
 
Alisikika mrusi moja wa kwa Tandele kwa mtogole akisema Urus imepata hasara
 
Wabongo bwana eti una siri huwezi kuziandika hapa! Daah! Acha kamba Mkuu.
 
6 HOURS AGO

Russian mercenary fighters from the Wagner Group have been depleted after months of combat in the eastern Ukrainian city of Bakhmut, the Institute for the Study of War said in its latest assessment.

Source: Moscow Times.

Hiyo ni taarifa toka kwa Warusi wenyewe kuwa Wapiganaji wa Wagner group wameteketea huko Ukraine. Ndiyo maana wametangaza kuwa maeneo waliyokuwa wanayashikilia huko Ukraine, wanayakabidhi kwa wanajeshi wa Urusi, wao wanaenda 'kupumzika'. Kumbe ukweli ni kwamba hawaendi kupumzika bali ni njia ya kujiondoa kwenye mapigano kwa sababu hawana wapinaji wa kutosha, wengi wao wameteketezwa huko Ukraine.

Habari zaidi, tafuta kupitia vyombo vya habari vya huko huko Russia, vya Magharibi utasema ni propaganda.

 
Ukraine wanaendelea kuifundishwa Russia mbinu za kivita.
Wazivyo na akili wamekubali kujitangazia ushindi kwenye mji usi na raia hata mmoja na sasa wamebaki wenyewe wakishangilia 'Ushindi' huo.
Hata hawajiulizi yalipopotelea wale mgambo wa Ukraine waliokua wakiwawashia mtiti. Tena wamepotea gjafla baada ya Russia kuganikiwa kuingiza wanajeshi wengi zaidi.
kifutacho ni hekaheka Mtoni...simulizi ya vijito vya damu kutoka Bakhmut
 
Inaelekea hata hujui kinachoendelea ila na wewe unataka uonekane unajua kumbe unajiaibisha mbele za watu.
Punguza hasira Mkuu. Mpaka sasa hali halisi ya uwanja wa mapambano inajulikana. NATO wanaisaidia Ujkraine kwa silaha na kila kitu lakini hakuna cha maana walichofanikiwa zaidi ya kuharibu uchumi wa nchi za Magharibi.
 
Kwa akili yako unadhani ni Urusi pekee inayopoteza rasilimali kwenye hii vita. Vipi Marekani na nchi nyingine za NATO hawapotezi rasilimali na kuharibu uchumi wao kwa kutuma mabilioni ya fedha na silaha Ukraine yaliyo nje ya bajeti zao?
 
Bro acha uongo! Hivi Leopard tanks siyo advanced weapon ya NATO? Patriot Missile System haimo kwenye NATO arsenal?
 
Lini NATO uliwauliza wakakwambia Urusi ana nguvu? Natamani watu wawe wanakuja na reasoning kama hii ya jamaa aliyeweka mambo logically kwamba kama Urusi imetumia muda mwingi kwa eneo dogo kama hilo, je kwa eneo kubwa zaidi itakuwaje? Hiyo ndo logic. Siyo mtu anakuja na ushabiki tu ambao hatuwezi kupima physically wala logically!
 
Alisikika mrusi moja wa kwa Tandele kwa mtogole akisema Urus imepata hasara
Ukitaka kukimbiza Warusi wa kwa mtogole anzisha uzi wa kingereza hutawaona au waulize maswali magumu hutawaona kuyajibu.

Wanachungulia tu wanasepa. Maana porojo wanazoziongea hawataweza kuziandika kwa kwa kiingereza.
 
Kupitia uchangiaji kwenye jukwaa hili (jamiiforums) nimejifunza mambo yafuatayo;

1. Watu wengi wapiga propaganda na porojo (Both Pro Russia and Pro Ukraine) wanaojifanya wanaijua hii vita hawana military skills na hawajui hata uwanja wa vita huwa ukoje? Wanafikiri ni kama sinema za Rambo.

2. Hawajui kwa nini USA, German, UK & Allies waliamua kumuunga Ukraine na kumsaidia kwa kumpa silaha na maarifa (Skills) za kivita.

3. Hawajui lengo la Putin kuivamia Ukraine kuanzia Crimea na sasa Ukraine yote. Pro Russia wengi wamekalili Special Military Operation (SMO) na hawajui hata SMO ni nini kwa muktadha wa Kijeshi na malengo yake huwa ni nini hasa.

4. Pro Russia wengi wanaamini kuwa majeshi ya NATO yanapigana Ukraine, kumbe ni propaganda tu za Russia. NATO hajapeleka hata silaha moja ya NATO wala wanajeshi wa NATO zaidi ya kushiriki kwenye vikao vya maamuzi ya nchi washirika (joint coordination committee) kutengeneza strategies (strategic level)

5. PRO Russia wengi wanaamini kuwa USA imepeleka wanajeshi wake frontline kupigana. Wakisikia Raia wa marekani kafa wanaamini kuwa mwanajeshi ambaye yuko in service. Hawajui kuwa Ukraine naye ana wanajeshi wa kujitolea (waliostaafu) kwenye majeshi ya nchi mbali mbali na wameenda kuomba ajira ili wapigane. Hawajui kuwa Ukraine nao wana mercenaries kama walivyo wagner.

6. Hawajui kuwa USA, German & allies wanapeleka wanajeshi wao (in service) si kwa ajili ya kupigana la hasha ni kwa ajili ya kutoa technical support yaani knowlege transfer ili Ukraine wapate uzoefu kuanzia installation, maintenance and support.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…