Hii vita mwambie Russia itakuwa active hata Kwa miaka 10 ijayo. Russia alipga hesabu zake vibaya.
Biden kama Putin angejua kinachofuatia asingejiingiza kwenye hii vita. Kwa hizi fedha zinazotokewa na USA kusuport hii vita Russia ajiandae uchumi wake kuporomoka vya kutosha !
Wanachokifanya westerners ni kumuharibia Putin uchumi wake kupitia vita!
Wiki hii Jeshi la Urusi limepita Hadi mitaaani kushinikiza vijana waingie jeshini lakini wamekutwa wengi hawana sifa za Jeshi. Sasa itakuaje baada ya miaka miwili au mitatu ?
Sent from my SM-A032F using
JamiiForums mobile app
Bahati mbaya umeliangalia kwenye angle moja.
Hii vita imekusanya vita ya aina 2.
(1) Ni vita ya kuvunja unipolar system
(2) Ni vita ya kuvunja uchumi
Na gurudumu ya hayo ya juu ni hii SMO Russia anayoiendesha. Lengo la Russia ni hayo yote 2. Hivyo operation haiwezi kwenda haraka. Kwa vikwazo alivyowekewa Russia kwa short term hasara kwa Russia kwa long term ni faida kwa Russia. Kwa sababu Russia ina vitu ambavyo dunia inavihitaji. Kwa namna yoyote tu mtarudi kwake.
Aliwekewa vikwazo kwenye fertilizer wamerudi kwake na wananunua tani kwa tani. US bado ananunua Uranium kwa kiasi kikubwa Russia kwani ndipo uhai wa vinu vyake vya nuclear. EU wamemuwekea vikwazo kweenye gas haijapita muda wamerudi kwake na kuilipia kwa pesa ya Russia. Walimwekea vikwazo kwenye mafuta mpaka sasa hakuna watu wanaoongoza kununua mafuta Russia kama nchi zilizomwekea vikwazo.
Kwa kuona Russia anapata faida zaidi kwenye mafuta wakapanga kuweka bei elekezi kwa mzalishaji ambaye ni Russia. Jana OPEC wametoa tamko lao wamepunguza kiasi cha uzalishaji wa mafuta kwa siku pipa million 2. Bado itakuwa ni faida kwa Russia! Bei elekezi haina maana kwa namna hiyo!
Hivyo huu mtanange kadri unavyozidi kwenda ndivyo unavyozidi kuwa faida kwa Russia. Kwa nini auwahishe kuumaliza wakati faida zaidi inakuwa kwake na EU uchumi wake unazidi kuporomoka?
Russia amewapa EU gas ndogo sana! Viwanda vikubwa vinafungwa, ni uchumi kuporomoka.
Ngoja niishie hapa nina majukumu mengine. Ila Russia ana clock na time kwenye huu mgogoro!
Ila kingine ambacho unachopaswa ujue: Nchi zilizopitia Ukomonisti au ujamaa zina uzalendo zaidi kuliko unavyofikiri. Raia wengi wamejitokeza kwa mapenzi yao kujiunga na jeshi baada tu ya kutangazwa. Na kwa nchi ya Russia kama hujui raia anapitia jeshini kama kwetu JKT. Walikataliwa ama kutokuwa na sifa ni wanafunzi waliyoko mavyuoni. Hawa ilitangazwa hawatoruhusiwa kujiunga katika jeshi inawabidi waendelee na masomo.