USA hata kama akasimama pekeake dhidi ya dunia nzima kivita, bado tutapigwa tu

Sasa ushindwe vita kwasbabu ya treaties za miaka ya 40s
Kinachozifanya nchi kuwa hivi zilivyo bila kuvuragana sana katika kuvamiana na kubadilisha mipaka kwa vita na nguvu ni treaties za miaka ya 40s.
 
Alinacha na ndoto zake
 
Vita vyote vya uvamizi huwa vinaisha kwa kukaa chini na kuafikiana kati ya mvamizi na anayevamiwa kwa hiyo haisaidii sana ukiwaua hao viongozi ambao mtatakiwa mkae nao chini baadaye kuafikiana.
Sio kwamba ukiwaua viongozi ndio vzr mana kunakuwa hakuna order kwenda kwa Watu wa chini/jeshi?
 
ana uwezo wa kuiangamiza dunia nzima kutokana na vifaa vyake. na USA amejipanga na kujiandaa vizuri kwa hilo. ila kupigana vita kama vita hataweza hata kidogo. labda akae ndani ajifungie then atume makombora ya nyuklia
 
wacha utoto...japo utoto raha sometimes
Watoto ni nyie ambao mnadhani mnayoyaona kwenye movie za akina rambo ndio uhalisia. Utoto ni kukataa data zao wenywe zinazoonyesha walipeleka personel zaidi ya milion 3 vietnam na bado vita ikawashinda wakaondoka bila kutimiza kilichopeleka.
tatizo utoto unawafanya mdhani mnayoyaona kwenye movie ndio ukweli
 
Kushindwa kivipi

Unalijua lengo la marekani Vietnam au Afghanistan , vita siyo ngumi za kuku kwamba anayezidiwa anakimbia! Kuna long run effect ! So Nani anaumia kati ya Vietnam na USA, Mwaka Jana nimekuwa Vietnam 🇻🇳 nimeshuhudia uchumi wao unavyo lag nyuma Kama Mkia wa kondooo !

Tatu Marekani alifaniliwa kusafirisha baadhi ya mambo nyeti toka Vietnam Hanoi na Ho chin min Kwenda USA , hivi mnaelewa malengo ya vita au ?

Britanicca
 
Zile filamu za Rambo,Missing in action zimeathiri ubongo wako.
 
Nimeamini Ashki ni wazimu!
Kwa taarifa Hadi Sasa MMarekani Hana mpinzani dogo!
 
Dogo movi za Hollywood za marekani kuibuka kidefea vimekufukirisha mpaka umekuja na huu upuuzi wako..

Dogo vita ni uhalisia sio mambo ya ku act. Marekani angekuwa na ubavu huo angeshakwenda kumtandika m north Korea na mu Iran
 
Begining jeshi la Hitler halikua na branches yaani bases au?
Are you serious.
Kwa kipindi hicho Ulaya nzima aliyekuwa na upinzani wa kweli kwenye technology, military technology, civiliantech nk dhidi ya Nazi German alikuwa ni mwingereza tu.
Ndio maana Kwa ukubwa na organized army ya Hitler iliweza kumkalisha ufaransa , ubelgiji na Poland Kwa miezi kadhaa. Eg ufaransa alisarenda baada ya miezi sita ya kichapo hapo June 1940. Poland alinukishiwa mwaka wa 1939 akapigwa akakalishwa, vilevile Ubelgiji na Balkan countries zote zikasanda game.

Wajerumani mwaka wa 1941 walivunja mkataba wa kuisogelea Soviet Russia. Kumbuka mpaka mwaka wa 1940 wakati Poland anatandikwa German na usoviet walikuwa pamoja wakimla Poland.
Ghafla Ujerumani ikaanza kuipiga Soviet Russia. Wakaisogelea Urusi Hadi karibu kabisa na Moscow inasemwa ilikuwa umbali wa km 22 kufika mjini hapo. Ghafla upepo ukabadilika Ujerumani ikaanza kupigika nyuma na mbele. Mashariki Mrusi magharibi alipotoka Marekani na Alies wake. Vita hii ikapiganwa Kwa miaka Minne.
Mataifa zaidi ya 20 yakaligana na Ujerumani ilivyokuwa na allies kadhaa.
Eti Leo wasema Ujerumani haikuwa na branch. Au ulimaanisha nini
 
Ebu tuanze alikuwa na bases kwenye nchi zipi??
 
Movie za John Rambo akiua Kijiji kizima Cha VietCong zinampotosha mtu. Huko Vietnam Wamarekani walikimbia wakaacha Kila kitu Hadi ndege , Hadi watu wao. Aliyeweza kukimbiza alikimbia. Hadi Leo Kuna Wamarekani ni missing in action hawajulikani walipo miaka 53 sa hivi.
Hapo Kwa machizboti Afghanistan Wamarekani kama ivyokuwa Vietnam walishindwa vibaya . Yaani wakati mikataba ya kuondoka Afghanistan inafanyika huko Uarabuni Taliban I wakaanza kuhodhi Kila kilicho Cha Wamarekani. Majeshi ya NATO wakaona isiwe shida wakaanza kukimbia. Hebu fikiria walienda kuwatoa Taliban lakini Bado wakati wa kuondoka aliyeAchiwa serikali ni Taliban.
 
Yaani ni kama alivyoenda Afghanistan, Iraq na Libya.
 
😂😂😂Walikuwa wapi kujiokoa kabla Japan hajaanza kuwa bize kupigana na wakubwa?
Kuna sino- japanese war mbili unless unadhani China kaanza kupambana na Japan baada ya marekani kushambuliwa.

So far Japan kaangia baadhi ya maeneo ya China kwa vita kakaa kwa vita na kaondoshwa kwa vita na wachina wenyewe.

Marekani alihusika baadae kwenye vita vya China na Japan baada ya marekani naye Japan kuwa adui yake.

Marekani kawakuta China na Japan wanatandikana sana tu.
 
Ukweli ni kuwa China alikuwa anatandikwa unaikumbuka manchukuo😂😂
 
Ukweli ni kuwa China alikuwa anatandikwa unaikumbuka manchukuo😂😂
Hiyo Sino- Japanese war imegawanyika pande mbili kutandikwa kwa China na kutandikwa kwa Japan na China kuwa fukuza Japan.

So far Japan aliivamia China iliyokuwa imejichokea China ya Qing dynasty kitu ambacho hata U.K hiyo chance aliitumia na kuipata Hongkong.

Wareno, wafaransa nao walitumia uchovu wa China chini ya Qing dynasty kukalia maeneo ya China.

Huyo Japan karne za nyuma alijaribu mara kadhaa kuivamia China aliishia kupigwa tu.

Ni wa Mongolia ndio walioweza kuitawala China
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…