USA hata kama akasimama pekeake dhidi ya dunia nzima kivita, bado tutapigwa tu

kwa wajinga kama nyiny mtachukua miaka 100 kuja kuwahelewa USA
 
Umejitahidi kufafanua vyema sana, lakini kuna sehemu unahitaji kusahihisha takwimu zako, ni kweli kabisa Usa ana uchumi mkubwa kuliko Russia, lakini kwenye upande nguvu za kijeshi mataifa hayo haya utofauti mkubwa, kuna baadhi ya vyanzo huonyesha Russia ana jeshi kubwa kulio Usa na vyanzo vingine huonyesha Usa ana jeshi kubwa kuliko Russia.
Lakini unapokuja kwenye swala la nguvu za Nuclear Russia ana siraha nyingi sana za Nuclear kuliko Usa tena mbali sana.
Lakini pia unaposema kwamba Usa anaweza kupigana na dunia nzima na akashinda hapo nadhani umeongea kwa kutanguliza mapenzi kwa nchi hiyo, hicho ni kitu ambacho hakiwezekani.
Kuna nchi kama china ambazo haziimbwi sana zina nguvu sana kijeshi hata Usa mwenyewe anajua.
 
😂😂😂Walikuwa wapi kujiokoa kabla Japan hajaanza kuwa bize kupigana na wakubwa?
Mwanajf unaweza kuwa na hoja ila kiukweli China ya WWII sio kama ya leo. Sipo katika mjadala wa mleta uzi, ila narekebisha hapo.
 
Acha ujinga haikuwa vita kamili! Ilikuwa vita ya kiitikadi kati ubepari na ukommunist!
Mwanajf "vita kamili" ni nini? Sijaelewa hapa. Vita kuu ya pili ya dunia haikuwa vita kamili? Na wala haikuwa ya kiitikadi?
Kwa takwimu USA ana nuclear warhead zaidi ya million 100 mpaka UN ikapiga kelele kuhusu wingi wa stocks za nukes.
Mwanajf naona hapa unatunywesha chai sasa. Namba ya Nuclear warheads sidhani kama iliwahi kuzidi Elfu 65. Labda utupe source. Kwa sasa inakadiriwa kuna Nuclear warheads 12500 na kiasi worldwide, U.S. akiwa anakadiriwa kuwa na nuclear warheads Elfu 5 na kiasi.

 
Bora wewe unajua mkuu hawa walamba soli wa USA hakuna wanachokifahamu mtu hajapitia OPERATION PAPER CLIP ambapo USA alichukua wanasayansi wa GERMANY zaidi ya 1600 akawapa na uraia .

Kuna wakina Wernher von Braun ambaye aliwekwa nasa , Albert Einstein, Hans Bethe, John von Neumann, Leo Szilard, James Franck, Edward Teller, Rudolf Peierls, na Klaus Fuchs ambao wamehusika kwenye secret projects nyingi sana na wamefanya vumbuzi ambazo zilifichwa kwa muda mrefu na USA na nyengine nadhani hadi leo hazijatolewa.

Kuna wakina oppenheimer ambaye wazazi wake walikuwa wahamiaji kutoka ujerumani angalia jamaa alichounda mpaka leo hii japan wamebaki na kumbukumbu mbaya sana kutoka USA.

GERMANS NI HATARI SANA TUKIJA KWENYR ISHU ZA TECHNOLOGY SIJAJU KWANINI KWA SASA HAKUNA VICHWA VINAVYOTOKEA KULE.
 
Ngoja nikuelezew kwa mfano ambao utaweza kuelewa maana huu mfano ndiyo unaendana na akili yako

Chukulia kuna mtu mmoja ana misuli kweli kweli na anajua kupigana halafu akapambanishwa na watu 100 kwa pamoja waje kumvamia unadhani ngumi zake na misuli vitamsaidia?
 
Alikimbizwa na Farah Aidid huko Somalia akaishia kumuuzia msala kenya mpaka leo.
 
stormryder punguza kuangalia movie za kina Rambo.USA ana uchumi mkubwa kuliko Russia haina ubishi lakini kwenye Vita baina ya mataifa haya mawili hakuna mshindi.Wote wana silaha za kuangamiza dunia nzima,hakuna mwenye akili timamu anayetamani kuona mpambano wa hawa miamba wawili kwani hakuna atakayebakia kuhadithia yaliyotokea.
Napenda kukushauri ujaribu kuchuja source zako za habari.Hawa wenzetu wa magharibi wamebobea kwenye propaganda kiasi ambacho taarifa zao zimekuwa zinapuuzwa na watu makini.Kama unakumbuka kabla ya SMO ya Russia kwa Ukraine tulibebeshwa uongo mwingi juu ya ubora mkubwa wa silaha za USA dhidi ya za Russia,matokeo kwenye battle field ni tofauti kabisa.
 
Germany na Japan [emoji557] baada ya WWII, walipigwa Pini juu ya masuala ya kijeshi, badala yake USA ndo anebaki kuwa mlinzi wao. Uwekezaji wao katika jeshi, pamoja na enrollment iko very limited kutokana na mikataba waliosainiana na USA.
 
Kitendo cha marekani kuweka military base kila kona ya dunia maana yake hakuna wa kupigana naye akamshinda
Ujinga mtupu, watu wakiamua hizo base wanazichapa vizuri tu na hakuna kitu atafanya huyo Mmarekani. Vita ya Nako 2 Nako hao Marekani hawatoboi hata kwa majeshi ya kiafrika
 
Germany na Japan [emoji557] baada ya WWII, walipigwa Pini juu ya masuala ya kijeshi, badala yake USA ndo anebaki kuwa mlinzi wao. Uwekezaji wao katika jeshi, pamoja na enrollment iko very limited kutokana na mikataba waliosainiana na USA.
Na wao wakakubali kabisa😁
 
Wajapan walikuwa na roho za kikatili zaidi ya Wakurya 😁 ila Nuclear ziliamua ugomvi!
 
We jamaa ni mjinga kiasi chake kwa sababu unaleta hoja ila wakati huo huo unajichanganya. Uchumi wa dunia ni zaidi ya $100 Trillion wakati wa US ni $25T, sasa hizi pande 2 zikiingia vitani unasemaje upande wenye 25 utaushinda upande wenye 70+

Pili kijeshi mfano mdogo US ana siraha za nuclear karibu 5400 wakati siraha zote zilozoko duniani ni zaidi 13000 sasa unasemaje upande wenye siraha 5000 unaweza kuushinda upande wenye siraha 6000 plus.

Hapo huajaongelea vifaa kama vifaru vya vifaru, drones, artillery nk ambazo kila siku tunaona zina flop battlefield.

Tusiwaabudu sana US huenda tukawashangaa siku likitokea la kutokea.
 
September 11 ilitosha kusema Marekani inaweza kupigwa kabisa! Shukuru tu katika tukio hilo moja ya ndege zilizotekwa na Magaidi haikuangukia Pentagon huenda mifumo yake ya Ulinzi inge collapse kabisa.
Afghanstan,Vietnam,Somalia kote huko alipigwa akakimbia!
Ambacho nakubaliana na wewe kwa uchumi wake anaouwezo wa kuhimili vita kwa muda mrefu tu lakini siyo Vita!
Kila teknolojia yake aliyonayo imeshaibiwa!
 
Wajapan walikuwa na roho za kikatili zaidi ya Wakurya 😁 ila Nuclear ziliamua ugomvi!
Kuna movie inaitwa "HACK SAW RIDGE" nadhani mkuu unaifaham.
Aliigiza yule kijana aliyeigiza "Amazing spider man".
Ile movie ilikua dedicated kwaajili ya kusifia mchango wa mwanajeshi mmoja ambaye alipigana WW2 ila alifanikiwa kuokoa zaidi ya 70+ US soldiers ambao walioumia na hakushika bunduki wala kufyatua risasi.
Yule mzee sasa hivi anakaa katika wheel chair ana zaidi ya 80+ years,mwishoni mwa ile movie walimrekodi na alikiri akisema" kama haikuwa ile nuke iliyopigwa Nagasaki na Hiroshima,tusingewaweza Japan hata kama tumewazunguka".
Maana wale askari wa Japan walikua wanafanya hadi SUICIDE BOMBING.
Halafu kuna mpuuzi anakwambia eti Japan ilishindwa kabla.
Na kuna mjinga mwingine anakwambia USA inaweza kusimama hata na dunia nzima.
Aiseeeeee!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…