Huo umasikini na mpango vinatoka wapi? Wakati hayo madude yanaanza kuundwa,ni miaka mingapi? Na lengo lilikuwa nini! Leo hii hata USA ikiacha kihelehele,inayapeleka yakafanye nini? Kila ndege inayotua hapo,kuna uwezekano wa kuitungua.
Karibia kila kona,ina base za kijeshi kuhifadhia. Kwa maana kutoka kila kona,ina uwezo wa kurusha ndege au makombola na ndege zikarudi.
Hata wapinzani wake wako hivyo. North Korea ana ngapi? Mbona ameshakuwa moto wa kuotea mbali? Hayo ni mavitu,yapo na yameshapitwa na wakati. Sasa unapoongelea ubora,au uwingi,hautakuwa na msaada. Sasa hivi wababe,kila kona ya dunia wanaweza kurusha kitu wakiwa wamekaa kwao. Gharama zote, si la kutengeneza miaka chini ya 5,au na zaidi? La nini? Hayo yanafaa TZ kupigia picha tu. Sasa hivi wote wanahangaika kuweka ulinzi wa ardhi tu,maana kila mmoja ameshaona kila akijaribu hili,mwenzake anaibuka na mtambo balaa. Kama alivyosema mdau mmoja, USA bila NATO yake,si chochote. Na ilivyosemekana sijui kitu gani kilitoka Russia,kikaenda Poland,kikageuza kurudi Ukraine, huo si uvamizi tayari? Mbona hawakuyapeleka! NATO si wanayo mengi! Hangaikeni na unga na mchele, mengine tuyaachie wanaoyataka.