KERO Usafiri wa Arusha Mjini – Loliondo umepanda kutoka Sh 18,000 hadi 28,000, LATRA hii ni sawa?

KERO Usafiri wa Arusha Mjini – Loliondo umepanda kutoka Sh 18,000 hadi 28,000, LATRA hii ni sawa?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Jamani sisi Wanangorongoro tunateseka sana wakati wa kusafiri kutoka Arusha Mjini kwenda Loliondo, kinachotusumbua ni upandashwaji wa nauli kiholela bila ya kufuata utaratibu uliowekwa na LATRA.

Kampuni ya Loliondo Coach ndiyo kampuni pekee inayotuhudumiwa.

Nauli ilikuwa ni TSH 18,000, wakapandisha mpaka 23,000, ikapanda tena hadi 25,000 na sasa wamepandisha mpaka 28,000.

Ikiwa abiria atapandia gari from kilometer zero bei inakuwa sawa na mtu atakaye pandia kilometer 100 mbele, hakuna utofauti wa nauli kati ya kituo na kituo.

Jamani tunaomba hili lifike kwa LATRA ikiwezekana tupate muongozo wa nauli per kilometers kwa Barabara za vumbi though bei za mafuta zipo juu lakini hawa loliondo coach wamekuwa too much.
 
Watanganyika kwa utawala huu w chura aka kizimkazi mpk mchanganyikiwe Hana time na watanganyika na pia ss mafukala hatuna chetu. Yy kachagua upande wa matajiri.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Huku gesi imepanda, nauli zimepanda,bidhaa zote za chakula zimepanda hii nchi imebakiza kupandisha majini tu!. hapa mpaka kende zangu zinachemka zimekuwa zamotoooooooooo!.
 
Juzi nilipanda boda boda ya baisikeli kule simiyu maswa lalago huko..... jamaa wakaniambia bei imepanda sababu ya vita ya Iran, kutoka 200 hadi 300 🤣
 
Bei ya unga wa sembe ikifika elfu 5 kwa kilo ndio hapo heshima itaongezeka kati ya mfanyabiashara na mteja, mpiga kura na kiongozi, mtoto na mzazi, bosi na mfanyakazi
 
Watu wanatumia fursa haswa kipindi hiki cha uhaba wa mafuta, na ubaya serikali na mamlaka zake ni kama zimelala vile
 
Bei ya unga wa sembe ikifika elfu 5 kwa kilo ndio hapo heshima itaongezeka kati ya mfanyabiashara na mteja, mpiga kura na kiongozi, mtoto na mzazi, bosi na mfanyakazi
Maana kwa sasa dharau zimezidi😂😂
 
Back
Top Bottom