Mmhhh,jamaniii hata wakaka/wababa wanaroho mbaya sana kwenye haya madala-dala, siji kusahau siku kwenye daladala ya kwenda muhimbili mkaka kaingia na chupa yake na kikapu hivi bila shaka alikuwa anaenda kumpelekea mgonjwa chochote kitu,katika kuwahi wahi bahati mbaya alimgusa mkaka aliyekaa kwenye siti kwa ile chupa yake ya chai heeee jamanii ndio nilijua kumbe kuna wakaka sio poa aseee aliongea,alimdhalilisha,alimpa kejeli za kutoosha,alimtusi mwenzie mpaka moyo wangu ulipata moto kisa tuu ile chupa imemgusa,dah!! basi ngonja tuu niishie hapo..