Usafiri wa daladala ni kipimo cha kiwango cha roho mbaya cha wakinamama na wadada

Nilishasema, kuna mengine tusifanyiane mzaha kabisa
 
Mkuu usiwaadhibu watu wengine kwa makosa ambayo ulifanyiwa na watu ambao huwakumbuki.
 
hahahahha wadada mmechafukwa!mm sijui npoje hata dent nikimuona uson kachoka nampisha!ila sio akae tenna ntu mwingne...kama siumwi napisha sana tu!nakumbukaga nimetendewaga wema na watu baki acha na mm nitende wema!
 
Kweli wanawake wengi wana roho mbaya, mm yuko mmoja nilikutana safarini toka mwanza to arusha tuko siti moja tukawa tumezoeana, tulipofika arusha kila mmoja akashika hamsini zake ila tukawa tunaendelea kuwasiliana, basi siku moja akanipigia simu kuwa nimsaidie ana shida na hela na vilio vingi mm kwa vile ilikuwa ndani ya uwezo wangu nikamsadia sasa tangia hapo ndio nikawa kama nimenunua uadui nikimpigia simu hapokei wakati mm nilikuwa sina hata mpango wa kumdai hiyo hela
 
Ukifanya hvo huna utakachogain ila ukimsaidia mwenzio utapata thawabu... na kama ni kufika unapoenda utafika tu.
 
Ukifanya hvo huna utakachogain ila ukimsaidia mwenzio utapata thawabu... na kama ni kufika unapoenda utafika tu.
Sihitaji kugain chochote na sitaki thawabu za kinafiki ntowe msaada kisha nchukie ndo maana siwapishagii...!
 
[emoji17] [emoji17] [emoji17] yaani wamelibeba hilo kama mzigo wa miba
I don't care[emoji2] [emoji2] shauri zao wenyewe...!!!yashanikuta halafu pata picha gari za mbagala zinavojaza...!!!Mimi wanijudge wanavyojua but kuna mtu kanishauri vzr hapo juu !!ntaanza kujirekebisha..kuna mmoja nilimsaidia mtoto ananuka kinyesi gooshh!!!
 
Hili jambo nimekutana nalo sana mpka nimeamua kutompisha mwanamke kwenye siti labda awe mzee sana au mjamzito or anamtoto mchanga
 
Dunia ina watu wazuri sana kama hujabahatika kuwaona basi kuwa mmojawapo. pole sana
 
Wanaume tuna upendo sana, wanawake hawapendanagi wenyewe kwa wenyewe
 
[emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28] wengine jamani hapana jamani, sasa ndugu huko ukokuwa unaenda si nishida, mie nitamsaidia mtu kwa uwezo wangu sio natoa msaada huku naumia hapana, mie nasafari zangu napewa kupakata mtoto maweee hapana maji sh.ngapi wabebane tu mama yake,

Pole sana kwa yaliokukuta
 
Hii tabia nimeishuhudia sana kwenye madaladala, unakuta wadada walio wengi akiingia mmama mjamzito au mwenye mtoto mchanga kwenye daladala unakuta wanajifanya wako bize na vi-smartphone vyao utadhani hawatokuja kushika mimba wala kuzaa watoto,
Mnafikiri mtaendelea kuwa vibinti milele? Itafikia kipindi na nyie mtakuwa mimama mijitu mizima na itafikia kipindi unaingia kwenye daladala na mimba yako kubwa hakuna mtu hata mmoja anaye kupisha utadhani waliziona takataka zako ulizokuwa unazifanya ujanani........,
 
Anaelipiza baya kwa baya ni shetani, na wanaomuunga mkono nao ni mashetani pia.
 
Kati ya vitu huwa nawashangaa wamawake ni katika hili la kuachiana siti..

Utakuta kimdada kimekaa na vikucha vimechongoka kama vya panya kinachezea simu huku mdada mwenye mtoto anayumbishwa huko na huku kwenye daladala
 
Hivi uzani wale wasiopisha hawana watoto hapana mkuu wengine wanao sana na wanajua uchungu wa mwana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…