USAID yatangaza kusitisha misaada nje ya nchi

USAID yatangaza kusitisha misaada nje ya nchi

Vp kuhusu ARV's aka Njugumawe?

Sio poa kabisa kuwasengenya Batanzania wenziwako.
You can do better.
Umeona ARV ndicho kipo kwenye Mada?

Naona ww ni Platinum member ikiwa na maana unachangia JF. CHANGIA ARV bandugu.
Mkuu.
Sio kwamba nasengenya mtu, U.S ndio mtengenezaji, muuzaji na msambazaji wa ARV's chini ya PEPFAR, usitishwaji wa misaada ni wazi pia PEPFAR itaathirika.

Mimi ni Platinum member ndio, na nipo hapa JF toka enzi za jamboforums. 😁
 
Ww ni muzeyi. Shikamoo.

Shida yangu haiko na ww muzeyi, shida iko na hii narrative(internet trolls narrative) ambayo inawasengenya, na inawazodoa wenye Ukimwi. Hilo sio nzuri. Hakuna sehemu yeyote ile katika kampeni ya Dictator Trump ambayo aligusia wagonjwa wa Ukimwi. Unafikiri kwanini? Ametuita Shitholes Countries but not or anything in regards to kumeza njugumawe?

As a Platinum member I expected more than what you said.

Shikamoo mukulu, but kusitisha ile misaada has so many nuances. Trump anataka kuonekana kana yy ndie anayeweza kutatua kila kitu, kumbuka, hivi karibuni Biden aliweza kususha bei za madawa kwa kutumia mswada wa bunge pamoja na ezakativ action, Trump ameondoa hiyo ezakativ action na nini uhakika anatumia hili la kuondoa misaada kuwatengeneza ,as a bargaing chip, wale Pharmaceuticals wapunguze bei, kwani hata hizo Dawa ArV n.k zinanunuliwa full Price na Serikali ya Marekani. Nimesoma pahali dawa hizo zinauzwa between US$1500 na 350 kwa dozi ya siku 30 tu, kuna wangapi wanaoathirika na Ukimwi Duniani amabo wanategeme misaada ya Marekani? Sio Tanzania tyu.m

Dictator Trump anatafuta kila sehemu panapovuja, anakamata anakamua mpaka kieleweke. Kwahiyo sio tu kwasababu za ARV tu he is casting a wide net na kama mfanyabishara anatumia kila mbinu za kuwafanya makampuni yanayopata fedha kutoka serikalini wapige kwata na yeye na ajenda zake.

Mkulu, hilo swali ulilouliza only perpetuates Unyanyapaa.

Ha ha wakati wa Jamboforums nilikuwa mdogo sana.l Sikuruhusiwa kuingia humu.
 
Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) limetangaza kusitisha utoaji wa fedha mpya na usambazaji wa fedha chini ya makubaliano ya malengo ya maendeleo (DOAGs) hadi uhakiki wa programu za msaada wa nje zinazofadhiliwa na USAID utakapokamilika.

Wakati mchakato wa kuhakikisha msaada wote wa nje unalingana na ajenda ya sera ya nje ya Rais Donald Trump ukitarajiwa kutolewa ndani ya siku 30, uhakiki huu unatarajiwa kukamilika ndani ya siku 85 kuanzia Januari 24, 2025.

Kutokana na hilo, USAID imewaagiza maofisa wote kusimamisha kazi, mishahara, na safari kwa asasi na taasisi zote zilizopokea misaada kupitia shirika hilo.

Hayo yamebainishwa kupitia barua rasmi kwa maofisa wa mikataba na makubaliano ya USAID na washirika wake, iliyotolewa na shirika hilo Januari 24, 2025.

Barua hiyo, iliyosainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Manunuzi wa USAID, Jami J. Rodgers, imeeleza uamuzi huo unatokana na utekelezaji wa agizo la Rais Trump la kurejelea na kurekebisha misaada ya nje ya Marekani.

Soma kwa undani katika tovuti ya Mwananchi.

View attachment 3215692
Waende zao tu, Dr Samia anao uwezo wa kuziba hilo pengo la misaada kwani anagharamia kila kitu nchini bila kutetereka, BIG UP MAMA.
 
Waende zao tu, Dr Samia anao uwezo wa kuziba hilo pengo la misaada kwani anagharamia kila kitu nchini bila kutetereka, BIG UP MAMA.
1738028260799.jpg
 
Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) limetangaza kusitisha utoaji wa fedha mpya na usambazaji wa fedha chini ya makubaliano ya malengo ya maendeleo (DOAGs) hadi uhakiki wa programu za msaada wa nje zinazofadhiliwa na USAID utakapokamilika.

Wakati mchakato wa kuhakikisha msaada wote wa nje unalingana na ajenda ya sera ya nje ya Rais Donald Trump ukitarajiwa kutolewa ndani ya siku 30, uhakiki huu unatarajiwa kukamilika ndani ya siku 85 kuanzia Januari 24, 2025.

Kutokana na hilo, USAID imewaagiza maofisa wote kusimamisha kazi, mishahara, na safari kwa asasi na taasisi zote zilizopokea misaada kupitia shirika hilo.

Hayo yamebainishwa kupitia barua rasmi kwa maofisa wa mikataba na makubaliano ya USAID na washirika wake, iliyotolewa na shirika hilo Januari 24, 2025.

Barua hiyo, iliyosainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Manunuzi wa USAID, Jami J. Rodgers, imeeleza uamuzi huo unatokana na utekelezaji wa agizo la Rais Trump la kurejelea na kurekebisha misaada ya nje ya Marekani.

Soma kwa undani katika tovuti ya Mwananchi.

View attachment 3215692

Trump yupo sahihi, kila nchi ianze kujitambua na kuanza kujitegemea wao wenyewe Sasa, wasiendelee kuitegemea Marekani. Safi Sana hii, hii itawalazimisha Watu wengine waliopo duniani kote hususani Watu weusi kuanza kujitambua na kupata akili nzuri ya kuweza kujitegemea. Hatua hizi za Utawala wa Trump ni Kama 'Black Consciousness Campaign' kwa Watu weusi wote kabisa hapa duniani ili waache kutegemea Misaada kutoka Marekani. Ni mwanzo mzuri.

Kwanza Watawala wengi sana wa kutoka katika nchi za Afrika pamoja na Vibaraka wao daima wamekuwa wakiwasema vibaya sana Wazungu hususani Watu wa Marekani kuwa ni Mabeberu na Wapenda Ushoga, Sasa kwa hatua hizi za Utawala wa Trump zitasaidia Sana kukomeshwa kwa hiyo Misaada inayodaiwa kuwa eti 'imetoka na Mabeberu na Wapenda Ushoga.'
Watu wa Afrika (Watu weusi) hususani waTanzania sasa wanatakiwa waelekeze maombi yao ya Misaada kwenda kwa Marafiki zao wa nchi za Mashariki ambao wanawaona kuwa siyo Mabeberu na Wasiopenda Ushoga, nchi za China, Urusi, Korea ya Kaskazini, Belarus, n.k ili waweze kupatiwa Misaada kutoka huko.
 
Saa 100 ajiandae kugawa hii nchi maana amegawa bure redilimali zote .....bado mlima tu....
 
Hakutakuwa na ArVs za bure tena huko mbele ya safari

Kuna hatari maambukizi mapya ya HIV kushamiri miongoni mwa Watanzania

Hii itapelekea Serikali kutumia gharama kubwa kuyanunua hayo madawa, otherwise tutarajie ule Ukimwi aliouimba Ferouz kwenye nyimbo ya "Starehe" kurudi tena Mtaani
Tufe tu
Watakaobaki watakuwa makini zaidi
 
Safi sana,wakati tunampigia debe Kamala,mkasema mwanamke hafai kuongoza kabisa,sasa jiandaeni kuanguka kwa H..IV na kufa kama kuku wa kideri
Naona mmarekani mweusi umetoa la moyoni. We ulimpigia kura uyo kamala?
 
Back
Top Bottom